Maoni;- Katika hili, Wazanzibari wanahaki kulalamika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni;- Katika hili, Wazanzibari wanahaki kulalamika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Julius Kaisari, Oct 18, 2011.

 1. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kwanza nina- declare interest,Mimi ni Mtanganyika,na naipenda Tanganyika. Baada ya hayo,turudi kwenye mada. Nimekuwa natafakari kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya Tanganyika, kuanzia maandalizi,matangazo, ushiriki na kila kitu, nikajikuta naona kama " haya maadhimisho yanafanywa na Tanzania, ambayo na Zanzibar wamo.

  Sijui kwa upande wa gharama ikoje,lakini kubwa zaidi ni ile dhana ya ushiriki kama TAIFA, huku ikiwa dhahiri inatuhusu Watanganyika, lakini ikifanywa na Tanzania. Sijui kama huko Zanzibar kuna hata kibwagizo kinachosikika,kuhusu Uhuru huo wa Tanganyika /tanzania/tanganyika /tanzania.....???? Je Ikifika Jubilee ya uhuru wa Zanzibar, itakuwa vipi?

  Tanzania itahusika? walau hata kupiga Promo???? Nidhahiri huu muundo wa Serikali hautufai tena.

  Mnaionaje jambo hili Wanajamvi?
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  wazanzibar hawaeleweki
  mwanzoni ilionekana hawautaki muungano ila Tundu Lissu alipouchokonoa na kuonesha ni kwa namna gani kuna maswali yasiyojibika kuhusu huu muungano ni haohao wazanzibar walimshambulia kuwa anataka kuvunja muungano.
  zanzibar waache hivyohivyo
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Ni sawa, lakini hilo haliondoi uharamu huu wa mambo yanavyokwenda/endeshwa.
   
 4. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wazanzibar ni kama mwanamke aliyeolewa kwa kufuata pesa, kutoka anataka, akikumbuka mshiko anavumilia mateso. Iliyobaki kulalama tuuuu!
   
 5. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Katika huu Muungano ni Tanganyika inayobena gharama 90%
  Kwa hiyo jambo lolote la Tanganyika ni la Tanzania wote, ila jambo la Zanzibar ni lao Wazanzibar
  Hivyo sherehe hizi za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ni za Tanzania wote, ikifika miaka 50 ya mapinduzi watafanya wao
  Haya ni maono yangu ktk muungano huu
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ukweli upo palepale Muungano unamatatizo unajua zanzibar kinachowasumbua ni NDOA YA CCM NA CUF!
   
 7. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  UmenifuraHISHA NDUGU! Hawa watu ni kichekesho, anyway ndio maana Nyerere alimuingiza mkenge Karume.
   
 8. M

  MUGESH Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwel wazanzibar they always complain about Mungano lakini wao mchango wao katika huu Muungano ni mdogo, compared to wanachokipata. But tuwabebe hivyo hivyo.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hakuna kubebana hapa kama zanzibar ni nchi basi ni lazima tuuimalishe muungano tena kwa kuanzia tuiludishe TANGANYIKA,
  KUUKOSOA NA KUREKEBISHA MUUNGANO SI DHAMBI!
   
 10. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Hakika. au Iwepo serikali moja. kwani serikali tatu kwa maana ya kuirudisha Tanganyika itatugharimu zaidi watanganganyika katika kuendesha serikali ya Muungano,ama sivyo Muungano upigwe panga. Hekima inahitajika zaidi ya ushabiki. Pia pamoja na yote,Wazanzibar waache majigambo,na mbwembwe.
   
 11. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tuwachie waende zao! Watuache na Tanganyika yetu nao wabaki na Zanzibar yao labda kelele zitapungua! Wao kuwanyanyasa wabara waishio visiwani wanaona sawa, ngoja nasi tuwaambie wahame au waombe vibali vya kuishi na kufanyabiashara bara muone watakavyo lialia na kulalama!
   
 12. D

  DONALD MGANGA Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dawa ni Tanzania moja tu basi. Tanganyika au Zanzibar huo ni upotevu wa resources ambazo zingetumika kwa watoto kwenda shule.
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Muungano una matatizo na hakuna Nchi inaitwa Tanganyika Duniani .Pia hakuna Nchi Duniani inaitwa Tanzania inatimiza miaka 50.Kosa kubwa ila wana siasa wamejiandaa kula nchi na pesa ukihoji mhaini .Leo wanasema uhuru wa Tanganyika kesho Lissu atahoji watakuja juu .
   
Loading...