Maoni - Katiba Mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni - Katiba Mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Goodrich, Jun 20, 2012.

 1. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  [FONT=&amp]Naamini mchakato wa Katiba Mpya utakuwa makini kwa kuwa tume iliyoteuliwa ni makini.

  Maoni yangu ni kwenye masuala ya msingi kama ifuatavyo;

  Katiba mpya itenganishe kabisa mihimili mitatu ya dola, yaani Bunge, Mahakama na Serikali. Mihimili hii isiingiliane kwa namna yoyote ile, wala muhimili mmoja usiwe juu ya mingine kama ilivyo sasa ambapo Rais ambaye ni mkuu wa serikali, ana madaraka juu ya Bunge na Mahakama.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hili ni la msingi kwa kuwa litaipa uhuru mihimili mingine ya dola, pia litaepusha mambo mengi ikiwamo wabunge kuwa mawaziri jambo ambalo linaondoa uwajibikaji wa wabunge kwa wananchi, litaepusha majaji kuwajibika kwa serikali au kuteuliwa na Rais jambo ambalo linaondoa haki.

  Kila Chombo cha Dola (Bunge, Mahakama na Serikali) kiwe na mfumo wake chenyewe.[/FONT]
  [FONT=&amp]Pia, kwa maoni yangu, vema Miundo ya Bunge, Serikali na Mahakama iwekwe kwenye katiba. Hii itadhibiti mtu mmoja kuwa na nyadhifa tatu au zaidi, itaweka muundo rasmi wa baraza la mawaziri na serikali kwa ujumla, itaepusha teuzi zisizo na maana na pia itaongeza ufanisi na kuleta matokeo yenye tija. Aidha, Tume ya Uchaguzi inaweza kuwa ni idara iliyo chini ya muhimili wa Mahakama.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Aidha, wananchi wanataka mfumo bora wa Muungano. Mpaka sasa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inapingana kabisa na Katiba ya Zanzibar. Wananchi wanataka kero hizi zipatiwe ufumbuzi kupitia Katiba.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mambo hayo yakizingatiwa tutapata serikali inayowajibika kwa wananchi, na hivyo kujenga taifa jipya lenye heshima, demokrasia ya kweli, amani, na maendeleo ya kiuchumi.[/FONT]
   
 2. M

  Martinez JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  True !!!!
  Haya ndio maoni yanayopaswa kufanyiwa kazi na tume ya katiba.
  Msingi wa matatizo ya nchi yetu ni kukosekana kwa uhuru Bunge na Mahakama.
  Pia tume ya uchaguzi iwe taasisi chini ya mhimili wa mahakama.
   
 3. M

  Martinez JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 518
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  Swali la kujiuliza ni kama JK atakuwa na uwezo wa kusimamia mapendekezo yatakayokusanywa na Tume ya Katiba !
   
 4. I

  Ibnu Mussa Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zanzibar huru kwanza, katiba ya muungano baadae
   
 5. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Zanzibar haiwezi kuwa huru hadi itakapojitambua na kujua historia yake na kuwaenzi mashujaa wake akiwemo Okello.
   
Loading...