MAONI: CCM imeingia vita vya anga bila ndege za kivita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAONI: CCM imeingia vita vya anga bila ndege za kivita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jingalao, Jun 10, 2012.

 1. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,263
  Likes Received: 10,455
  Trophy Points: 280
  Kwa wiki kadhaa sasa Chama Cha Mapinduzi kimeamua kupambana na CHADEMA kwa kutumia mikutano, maandamano na mitandao ya kijamii.

  Mfumo huu wa mapambano umekuwa ukitumiwa na wanaCHADEMA kwa mafanikio makubwa sana.
  Ukweli ni kwamba CCM haina utaalamu katika aina hii ya mapambano. CCM imekosa wasemaji wenye vipaji na uwezo wa kuwavuta vijana, wasomi na wafanyakazi ukilinganisha na CHADEMA, mbinu hii mpya ya kuendesha siasa ni muhimu lakini inahitaji wataalamu wa hali ya juu.

  CCM ingefanikiwa sana kama ingeendelea kutumia mbinu zake za kawaida kama vile kuhakikisha mabalozi wa nyumba kumi, wenyeviti wa vijiji au mitaa na wakuu wa wilaya wanawajibika ipasavyo kurudisha imani ya chama kwa wananchi na kuhakikisha CCM inashinda kwenye chaguzi mbalimbali.

  Hakika ni kosa kubwa kutumia style iliyowatowa CHADEMA kimasomaso huku tukijua CCM ni mbabe wa vita ya mtaa kwa mtaa au nyumba kwa nyumba.

  Nape umetuingiza katika vita vya anga bila kuwa na maandalizi ya kutosha na matokeo yake yatakuwa mabaya sana kwa upande wa CCM.

  TAHADHARI KWA MODS-Naomba thread hii isifutwe au kuunganishwa na thread nyingine kama mlivyonifanyia jana.


  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 2. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ccm wameona hizo siasa za kibabe na ukiritimba hazieleweki tena kwa kizazi cha leo.

  wewe ulitumainia kuwa wadanganyika wataishi kwa unyenyekevu wa woga milele???? advantage waliyokuwa nayo ccm ni kuwa waliendeleza ushenzi wa kikoloni wa mzungu na mwarabu dhidi ya ndugu zao.
  Mfano hai nilioshuhudia mimi miaka ya 70's nikiwa bado mtoto ni watu wazima wenye wake na watoto wakikimbia baada ya landrover ya mkuu wa wilaya kuonekana inakuja kijijini. Mkuu wa wilaya siku hizo alikuwa kama sultan au governor wa malkia alikuwa na uwezo wa kumkamata mtu yeyote kijijini na kumpeleka gerezani bila kuulizwa. Sasa mambo kama hayo ccm waliarithi kutoka kwa wakoloni na wameyaendeleza katika kipindi chao chote cha kutawala. Walikuwa wanabadilisha majina tu mara kigogo, mara kingunge mara mtu mkubwa mara mtu mzito nk wakimaanisha vijisultani na vi governor vi mungu mtu.
  Miaka ya 80's baada ya vita kulikuwa na shida za bidhaa, maji na umeme wa mgao ukaanza, ukubwa wa mtu ulikuwa ni kuwa na huduma zote muhimu wakati wananchi wengine hawana, walikuwa hawapangi mistari ya foleni ili kupata mahitaji kama wananchi wengine bali walikuwa wanapelekewa majumbani mwao na watumishi wa mashirika au serkali, wakienda hospitali au kukata ticket za usafiri nk wao wanaruka foleni ukinung'unika unaambiwa kwani wewe humjui huyo ni nani?? mtu mkubwa huyo!!!

  Miaka ya 90's siyo tu waliendeleza ushenzi wao bali pia wakaanza kujilimbikizia mali, kupeleka watoto wao ng'ambo nk wakaanza kuigawa jamii katika matabaka ya walionacho na wasionacho, hali iliyofanya watu waanze kulalamika lakini kwa ajili ya kutokuwepo kwa elimu na hofu iliyojengeka kwa muda mrefu ya wananchi kwa serkali, basi ccm waliendelea kujihakikishia umilki wa serkali na kuendelea kutawala kwa hiari au mabavu, kwa hadaa au kwa chochote kile

  Sasa watu wameamka wanataka ukombozi wa kweli, wawe huru kutoa maoni na kuwaajibisha viongozi uchwara wanaorudisha nyuma maendeleo ya nchi yao. Hapa tulipofika haogopwi mtu tena siyo mjumbe, mtendaji wala mkuu wa wilaya au mkoa, waziri wala mtoto wa raisi, muda wa ukoloni umeendelea sana na sasa saa ya ukombozi imewadia, wenye akili wameliona hilo!!
   
 3. a

  andrews JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CCM HAWAACHI KUOTA MCHANA KWEUPE,KATIKA KAMPENI ZAO ZA KUWAPUUZA WATANZANIA WAMEANDAA ULAGHAI MWINGINE ILI WAPATE KURA ZA WAPUMBAVU.
  1.KUANZISHWA BENKI YA WAKULIMA
  2.KUANZISHA BENKI YA VIJANA
  KATIKA UANZISHWAJI BENKI HIZO SERIKALI INA MPANGO WA KUWAHADAA WATZ KWA KUWAAMBIA WATAWAKOPESHA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU,KUANZIA MILLION 1MPAKA 15.LAKINI KATIKA UOMBAJI HUO UNAHUSISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI KAMA MAWAKALA WAO ILI UPATE MKOPO,CHA KUCHEKESHA ZAIDI INAAMINIKA CCM IMEJIPANGA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA URAIA NA HASA CHA KUPIGIA KURA KAMA MTAJI WA KUWAPATA HAO WALENGWA.NA KUHAKIKISHA WANAOCHUKUA MIKOPO WOTE WATAIPIGIA CCM UCHAGUZI KUANZIA UDIWANI WA 2014 NA UCHAGUZI MKUU 2015.LAKINI WAJUMBE WENGI WANA WASIWASI KUWA VIJANA WALIO WENGI WAMEELEVUKA SANA NA WATAKULA PESA ZAO NA KUWAPIGIA WAPINZANI.CCM ILITUMIA MKUTANO WA JANGWANI KAMA KIPIMA JOTO SASA WAMEANZA KUINGIWA NA WASIWASI MAANA MKUSANYIKO ULE HAUKUKAMILIKA BILA YA PESA SASA WANAJIULIZA BILA VIKINDI VYA SANAA KWELI WATAKUBALIKA,MJUMBE ALIYE KARIBU NA NAPE KASEMA CHADEMA INAWANYIMA USINGIZI KULIKO HATA MAGONJWA YA WAZAZI WAO AU WANANDOA WAO.
  BINTI MREMBO LUMUMBA CCM
  :confused2:
   
 4. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Bado wanaendelea kutumia mtaji wao mkubwa, ambao ni umaskini wa waTZ!! Safari hii sidhani kama watafanikiwa
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  andrews ukiandika bila kuweka hiyo mifont yako inayotuumiza macho utaeleweka tu, otherwise mbwembwe nyingine hizi ni za kijinga tu. nimevumilia lakini nimeshindwa ni kweli tu ndio umuweka mtu huru.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unategemea nini kwenye chama ambacho wazee ndo kila kitu hawataki vijana na ndio maana hata mbinu zao niza karne ya 13. hawasomi nyakati kwao ccm madaraka ni kuiba mpaka mwisho, unategemea watawachia vijana? ambao sasa ndo wako CDM kuongoza UKOMBOZI
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  vijana wa ccm lazima watoke kwenye ukoo wa kiongozi ndio apate madaraka
   
 8. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,263
  Likes Received: 10,455
  Trophy Points: 280
  naona bado ccm inaamini kufanikiwa kupitia mbinu za chadema!


  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Aliyeiroga ccm alishafariki, sasa ni ngumu kupata dawa ya kuzingua zindiko.
  Njia hiyo waliyoamua kuitumia ndiyo itawamaliza.
  Watu wenyewe wababu wataweza kuhimili aibu za uzeeni?
  Nilicho na uhakika nacho ni kwamba njia hiyo wataiacha baada ya muda mfupi kwa kuchemsha vibaya. Kuna maeneo watarushiwa mawe, believe itg
   
 10. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,263
  Likes Received: 10,455
  Trophy Points: 280
  siku zote chadema ilipenda kuona mnaiga style yao
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kuna makada wa ccm wameamza kuamini haya unayosema
   
 12. b

  blueray JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi CCM ni chama kisicho rasmi cha upinzani, kila kitu wanajipima na CHADEMA.

  Wataendeshwa mchakamchaka hadi wenyewe watachoka. Watarudi kwenye wizi wa kura, lakini safari hii wizi utakumbana na nguvu ya umma.
   
 13. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #13
  Nov 26, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  kama kweli mikakati wanayotumia hivi sasa ccm watashindwa vibaya tunalalamika nini??? kwanini mnamuamsha aliyelala/[ kama kweli amelala?] au ni uoga fulani kuwa pengine watashinda??? vinginevyo adui wako muombe njaa.
  kama mkakati wao wa sasa ni mbovu basi iwe furaha kwa upinzani maana uhakika wa upinzani kuingia ikulu uchaguzi ujao ni wa uhakika zaidi vinginevyo jamaa kama wataendelea na 4w-drive huko mbele maajabu yanaweza kutokea kwa kuingia tena ikulu by wider margin than before sasa sijui ikitokea hivyo mtasusa?????[haya ni maoni tu]
   
 14. the challenger

  the challenger Member

  #14
  Nov 26, 2012
  Joined: Nov 14, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi kwao walioanzisha hiyo vita, tunachotaka mujue, sisi watanzania tumechoshwa na namna CCM wanavyoliendesha hili Taifa kama vile wanagawana maandazi juu ya rasilimali zetu............. kazi ni moja tu kuwaweka pembeni sasa..... Tunawaomba wajiandae kisaikolojia kukabidhi Nchi hii kwa watu wengine kwa usalama na amani yetu kama ilivyo.........Freedom is coming tomorrow(2015)
   
 15. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #15
  Nov 26, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  Mkuu una ujumbe mzuri, ila tusaidie wasomaji wako kutoweka rangi, na pia herufi ndogo zinasomeka kwa raha zaidi.

  Thanks kwa mchango wako.
   
 16. B

  Bob G JF Bronze Member

  #16
  Dec 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm wanachokifanya ni kama kuigiza. Hakuna mabadiliko ya msingi yanayotegemewa na hii secretariert mpya. Tatizo la ccm ni mfumo hata nyerere angefufuka na kupewa uenyekiti angeshindwa. Ni siku zimefika ni lazima ccm ife kifo cha kawaida 2
   
 17. Sonofthemajesty

  Sonofthemajesty Member

  #17
  Dec 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  'Chama Cha Migogoro'...xo wat z ajabu abt that? Wao wanaona fahari kuwa na migogoro na vyama vya upinzani kavile ndio mfumo wa maisha ya kila siku... Yaan wameshafulia na xaxa wanaanza kuozeana na kutokwa na funza huku vilio vikitawala madomo yao...
   
 18. Mzalendo wa ukweli

  Mzalendo wa ukweli JF-Expert Member

  #18
  Dec 3, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 562
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wataalamu wa kucopy na kupaste!!!!!!!
   
 19. Kitoabu

  Kitoabu JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 5,765
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Muhongo
   
 20. Kitoabu

  Kitoabu JF-Expert Member

  #20
  Dec 3, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 5,765
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Hivi wana jf wenzangu mnajua tatizo la nchi ye2 nimfumo na si chama? Mm bado nina wasi wasi na hao cdm ina weza kuwa chupa nyengine ila mvinyo ni uleule, sababu cdm ina ongozwa na watu tena wengiwao wame toka humohumo ccm sasa tujiulize nijambo gani jema walili fanya wakiwa huko?
   
Loading...