MAONI: CCM imeingia vita vya anga bila ndege za kivita

Mbona kama mnawapa promo la kiana hivi manake scandal make some body famous, bora kuwa chunia vinginevyo wanashinda hiyo vita na silaha mnawapa wenyewe bila kujua.
 
CCM ingefanikiwa sana kama ingeendelea kutumia mbinu zake za kawaida kama vile kuhakikisha mabalozi wa nyumba kumi, wenyeviti wa vijiji au mitaa na wakuu wa wilaya wanawajibika ipasavyo kurudisha imani ya chama kwa wananchi na kuhakikisha CCM inashinda kwenye chaguzi mbalimbali.

Hapana Mkuu.. CCM ingefanikiwa sana kama icingeacha lengo la kuundwa kwake la kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi (hapa maana nzima ni walala hoi).. Huwezi kurudisha imani ya chama kwa walala hoi wakati wanaona umacikini wao unasababishwa na viongozi walio madarakani wa chama chao..!

Mfano:.. Leo mlala hoi anajua Chenge alichukua rushwa ili Tanzania iuziwe rada mbovu kwa bei ya juu.. Badala ya kuadhibiwa na chama ndio kwanza akapewa uenyekiti wa tume ya maadili CCM na sasa mwenyekiti kwenye kamati moja ya bunge..! Unategemea ni nani atakaekuwa na imani tena..? Huo ni mfano mmoja kati ya mifano hai milioni ya uongozi mbovu na wa rushwa wa chama tawala..!
 
nimewaona vijana wa nape walivyonwagwa humu jamvini.mwisho wa siku wote wataishia chitchat
 
bado naendelea kumuonya nape kuwa ccm haiwezi vita vya mtandaoni!
Ukifuatilia posts ndani ya jamvi hili utaona ccm inavyozidi kubomolewa.
 
Jingalao enzi akiwa na akili!
Kwa wiki kadhaa sasa Chama Cha Mapinduzi kimeamua kupambana na CHADEMA kwa kutumia mikutano, maandamano na mitandao ya kijamii.

Mfumo huu wa mapambano umekuwa ukitumiwa na wanaCHADEMA kwa mafanikio makubwa sana.
Ukweli ni kwamba CCM haina utaalamu katika aina hii ya mapambano. CCM imekosa wasemaji wenye vipaji na uwezo wa kuwavuta vijana, wasomi na wafanyakazi ukilinganisha na CHADEMA, mbinu hii mpya ya kuendesha siasa ni muhimu lakini inahitaji wataalamu wa hali ya juu.

CCM ingefanikiwa sana kama ingeendelea kutumia mbinu zake za kawaida kama vile kuhakikisha mabalozi wa nyumba kumi, wenyeviti wa vijiji au mitaa na wakuu wa wilaya wanawajibika ipasavyo kurudisha imani ya chama kwa wananchi na kuhakikisha CCM inashinda kwenye chaguzi mbalimbali.

Hakika ni kosa kubwa kutumia style iliyowatowa CHADEMA kimasomaso huku tukijua CCM ni mbabe wa vita ya mtaa kwa mtaa au nyumba kwa nyumba
 
Back
Top Bottom