Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,831
Maonesho ya biashara yanayojulikana kama Sabasaba yalianza mwaka 1962 yakiwa ni maonesho ya Kilimo yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Wizara ya Biashara na Ushirika. Maonesho hayo yalikuwa na lengo la kukuza kilimo na ushirika
Mwaka 1978 serikali iliunda Bodi ya Biashara ya nje kupitia sheria yake namba 5 ya mwaka huo. Bodi ya Biashara ya nje ilipewa dhamana ya kukuza ushirikiano wa biashara ya kimataifa kupitia maonesho ya kibiashara, kufanya utafiti kuhusiana na biashara
Miaka ya hivi karibuni maonesho hayo yamekuwa yakishirikisha nchi takribani 20 kutoka Kusini mwa Afrika (SADC) vilevile yamejulikana kama maonesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na viwanja vinajulikana kama viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilianzishwa na Sheria ya Bunge Na. 4 ya mwaka 2009 na kuanza shughuli zake rasmi tarehe 3 Septemba, 2010 (GN Na 338). Uanzishwaji wake ulitokana na kufutwa kwa Sheria ya Bunge Na. 15 ya 1973 iliyoanzisha Bodi ya Biashara ya Ndani (BIT) na Sheria ya Bunge Na. 5 ya 1978 iliyoanzisha Bodi ya Biashara ya Nje (BET). TanTrade ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya udhibiti, utendaji, na ushauri wa kuendeleza na kukuza biashara ya ndani na nje ya nchi