Maombi ya kufunga kwa ajili ya kwaresma

Maombi ya kufunga kwa ajili ya kwaresma

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,023
Reaction score
36,865
NIFUNGE NINI KWARESIMA.?
Funga dhambi upate utakatifu.
Funga huzuni upate furaha.
Funga majivuno upate utukufu.
Funga wivu upate baraka.
Funga kinyongo upate faraja.
Funga uchoyo upate neema.
Funga dharau upate heshima.
Funga hofu upate imani.
Funga kiburi upate unyenyekevu.
Funga hasira upate upole.
Funga ujinga upate hekima.
Funga umbea upate amani.
Funga matusi upate uchaji.
Funga aibu upate ujasiri.
Funga chuki upate marafiki.
Funga uvivu upate mafanikio.
Funga ulevi upate afya.
Funga uzinzi upate wongofu.
Funga roho mbaya upate upendo.
Funga starehe upate muda wa sala.

Mpendwa! Mkristo Mwenzangu,Mtu wa Mungu Yatupasa kipindi hiki cha Kwaresima tufunge yote yaliyo mabaya, ili tupate mema tusiyoyatarajia kutoka kwa Muumba wetu. Hivyo Kwaresima ya mwaka huu, ikawe ya tofauti sana maishani mwetu 'Kwa Moyo wangu wenye shukrani na Unyenyekevu Kwa Mungu, Naomba wale Wote Ambao niliwakosea Kwa kukusudia Ama Kwa kutokusudia Naomba Mshushe Nguvu ya Msamaha juu yangu naianza siku hii njema ya Kupakwa Majivu. Nami Ninawasamehee wote mlionikosea Kwa kukusudia Ama kutokusudia Mungu ambariki Kila mmoja wenu Kwa jina lake
 
Back
Top Bottom