Nifunge nini Kwaresma? Mambo ya kufunga kipindi cha Kwaresma

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
26,202
68,545
Wale tuliokua tunajiuliza tufunge nini majibu haya hapa.

Funga huzuni upate furaha,
Funga ulabu upate siha,
Funga majivuno upata utukufu,
Funga uzinzi upate wongofu,
Funga kisirani upate utakatifu,
Funga umbea upate fanaka,
Funga wivu upata baraka,
Funga unafiki upate uchaji,
Funga kinyongo upate faraja,
Funga kwaresima wakati ni huu
Funga kiburi ujazwe hekima,
Funga jeuri ujawe rehema,
Funga hofu ujazwe imani,
Funga kinywani ujazwe moyoni,
Funga kisirani ujazwe rohoni,
Funga dharau ujazwe heshima,
Funga majungu, ujazwe neema,
Funga usiri ujawe wafuasi,
Funga tamaa ujazwe kiasi,
Funga kwaresima wakati ni huu.

KWARESMA NJEMA WAKUU
 
Aina za funga hizi hapa- funga ya danieli, funga ya yohana mbatizaji, funga ya yesu, funga ya yona. Yohana mbatizaji alifunga kwa kula chakula cha aina moja tu, nzige na asali. Danieli alifunga kwa kutokula vyakula vitamu, alikula mtama na maji. Yona alilazimishwa kufunga siku tatu akiwa tumboni mwa samaki mkubwa. Wengine hufunga kwa kula masaa 12, 24, 48, 72, Yesu alifunga siku 40, kuna wanaojaribu kuvunja rekodi hiyo ila bado haijavunjwa. Anyway maombi ya kufunga ni muhimu ila hutegemea na imani ya mtu anaamini nini. Wengine wana dini yao na wana mfungo wao unaitwa swaum, huko wanajua wenyewe wanafunga kwa muda gani kula. Ziko aina mbalimbali za kufunga
 
Hakuna mfungo unaitwa swaum
Swaum ni neno la kiarabu lenye maana ya “mfungo”

Kwahiyo hakuna mfungo unaoitwa mfungo

Waislam tunafunga mwezi unaoitwa Ramadhan

Nduguz zetu Wakristo fungeni muimarishe afya, fungeni zipate tiba nyoyo zenu, fungeni muongeze imani na fungeni mpate radhi za Bwana Mungu wenu

Kila la kheri.
 
Back
Top Bottom