Maombi ya kazi yoyote . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maombi ya kazi yoyote .

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by MAKALA, May 15, 2009.

 1. M

  MAKALA Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Guys
  kutokana na ugumu wa maisha nimeombwa na binti wa kama miaka 20 kazi yoyote ile kwenye ofisi yoyote ile.
  So naomba msaada wenu. Naomba utani usiwepo ni very serious.
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Kazi ya ofisini lazima useme ana elimu/ujuzi gani. Mambo ya kazi yeyote ya ofisini sijui kama bado yapo.

  Anatafutwa msaidizi wa nyumbani.

  Sifa:
  - Awe mwanamke.
  - Awe na ujuzi wa house keeping na at least cookery haimpigi chenga. Ajue kupanga bajeti ya nyumbani na kuifuatisha.
  - Awe mpenda watoto, ajue kusoma na kuandika ili awasaidie watoto homework pale itakapobidi.
  - Awe mwaminifu na awe mtu wa kujituma na aweze kuchukulia nyumba na familia kama yake (Kuchukua nafasi ya baba na/au mama kwani muda mrefu hawapo nyumbani).
  - Asiwe wa kuja asubuhi na kuondoka.
  - Likizo ya siku 28 itatolewa mara moja kwa mwaka.
  - Ruhusa panapokuwa na dharura kama ugonjwa au msiba pale Baba na/au Mama watakapokuwepo nyumbani na siku zitakatwa kwenye likizo.
  - Asiwe kaolewa.
  - Matibabu yake juu ya mwajiri.
  - Ujuzi katika maswala ya intanet, MS excel na outlook ni added advantage lakini si lazima kama vigezo vyote hapo juu vitatimizwa.
  - Mshahara negotiable na atakatwa makato ya NSSF. No PAYE.


  Tuma maombi na vithibitisho vya ujuzi pamoja na majina ya watu wawili wanaokufahamu (weka namba za simu na anuani zao) kwenda kwa mama@jamiiforums.com.

  Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni 30.06.2009.
  Kuanza kazi 01.08.2009.
   
 3. M

  MAKALA Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Okey mama, nimekupata elimu ni form four amesoma ana kozi kozi za computers . Ok ntampa hayo maelekezo.
   
 4. M

  Mama JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Ujumbe huu sio kwa huyo anayetafuta kazi ya ofisini, maana yeye tayari na interest na kazi yeyote ya ofisini.

  Ujumbe huu ni kwa mtu anayetaka kazi ya usaidizi nyumbani.
   
 5. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Lakini unaposema kazi yoyote ile ya ofisini inakuwa vigumu kidogo huyo mtu kuipata! Inabidi u-specify hata section zipi ambazo unaona ata-fit.
   
 6. M

  MAKALA Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  kutokana na kwamba anakozi za computer so usecretary ungemfaa zaidi ila yeye anasisitiza kazi yoyote maana hata hela ya matumizi hana.
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sasa mama kama ujumbe wako si kwa yule aliyeomba, kwa nini uchomeke tangazo lako kwenye thread hii, si ungeanzisha an independent tangazo mama?
   
 8. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ninayo kazi elfu 45,000 kwa mwezi,kulala bure,chakula cha mchana bure. aje na mashuka tu.Sehemu ya kazi-Makete. Aina ya kazi ni mhudumu. Ili mradi anajua kiswahili na ajue kupika vitu vya kawaida kama wali,maandazi,chapati,birian,pilau etc. Ujuzi sio muhimu. Awe amemaliza standard 7 au zaidi. Awe na marefa 2 .
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama upo clear sana hapo.......Kulala bure,.......lunch...bure..aje na mashuka tu????

  Kulala bure....nilifikiri ingejumuisha chakula cha mchana na jioni pia,....na mbona mwambii aje na blanket? ....mashuka tu Maketi mkubwa?
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu wasiliana na Fidel80 anaweza saidia hii!
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  May 16, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...binafsi roho imeniuma sana mama hapo ulipobainisha compassionate leave, na sick leaves zitakatwa kwenye likizo ya mwaka. Anyway, kila nyumba ina taratibu zake, ila labda pia kina mama muwe wawazi kuwafahamisha (house girls/boys) masaa yao kazi kwa wiki, na siku za mapumziko ili kuboresha productivity.
   
 12. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ingesaidia sana kama ungemwacha huyo job seeker ajitangaze hapa mwenyewe. Itaonyesha prospective employers kwamba 1) ni proactive 2) computer savvy 3) ana initiative 4) anajua kuuza ujuzi wowote alionao

  Wewe kumuuza huwezi. Anatafuta kazi kwa "sababu ya ugumu wa maisha," hivyo naturally yeye asingependa kazi? Binti huyo anamwambia muajiri nimepigwa na jua ndio nimeamua kutafuta kazi. Ukipata bwana mwenye pesa hapo ofisini utaacha kazi, au? Anatafuta kazi yeyote ya ofisini, kazi gani ya ofisini, kupika chai? Matokeo yake ndio anajibiwa akapike chai kwa kina Mama hapo juu wanaotangaza vacancy za domestic slavery:

  Basi anzisha thread nyingine, alright Mama?

  Unless una home office. Fungua thread nyingine utangaza home office ya kulea watoto, na kufanyisha home work za watoto, na ku act kama Mama ya nyumbani "kwani muda mrefu Mama hayuko nyumbani."

  Utangaze hiyo kazi ya ambae "hajaolewa." Maana unajiita Mama, nadhani una watoto, ila wewe watoto wako umewapa kwa artificial insemination, hukuolewa. Ndio maana mfanyakazi wako, mwanamke mwenzako pia hutaki aolewe. Una wasiwasi kwamba hata akiwa kazini muda wote anaotakiwa, atakuwa bado anawaza mumewe, atakuletea matatizo ya ndoa, ndio maana pilipili ya shamba, mambo ya nyumbani kwake, yanakuhusu mwajiri.

  Ueleze vizuri hiyo kazi ambayo unampa siku 28 za livu lakini unataka alalie, aamkie hapo hapo kazini. Ukimaliza kutuhesabia likizo tuhesabie pia masaa ya kazi. Kwa siku. Umehesabu time off, tuambie na time on.

  Au, uweke wazi kwamba anafanya kazi from can't see in the morning to can't see at night. Kwamba ni domestic slavery, woman on woman subjugation. Maana hata wewe mwajiri wako akikwambia kuanzia leo unalala kazini hutanibishia ni incredible exploitation. Unaamkia kazini, unalalia kazini. Hamna kuolewa, hamna kufanya mapenzi zaidi ya ku repiwa na watoto wa bosi. Mkimpa mimba - that is wewe mwajiri, na watoto wa bosi, na house boy, na mumeo - mkimpa mimba fire her behind, rudisha Iringa. Sio mwanao, who gives a rat's tail?
   
 13. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Dilunga bana.... maneno meengi ..
  Sasa huyo dada anataka kazi yoyote hata ya Udirector ataweza?maana kuna position hapa kwetu ila ni ya udirector.Huwezi kusema unataka kazi yeyote .. ma HR walivo na fitna wakiona unataka kazi yeyote wanajua we hauko serious unataka kazi kwa kuwa una shida ukishapata vijihela utawakimbia...
   
 14. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #14
  May 16, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280

  Ohhhh Mama...utakuta mwana si wako......unataka awe na uwezo wa kumsaidia mzee kama haupo?...shauri lako.....Duh.....Haki ya nani wewe unacheza.....Akichukua nafasi yako..mzee akanogewa....utajistukia unakuwa foreignber kwenye nyumba yako..
   
 15. m

  mnozya JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  NI MAKOSA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA KAZI No. 6 & 7 OF 2004 PAMOJA NA KANUNI ZAKE KUZIKATA COMPASSIONATE LEAVE NA SICK LEAVE KWA NAMNA YOYOTE ILE. KUMBUKA HIYO NI HAKE YAKE INALINDWA KWA MUJIBU WA SHERIA ILIYOPITISHWA NA BUNGE.

  TAFADHALI NAOMBA KAMA KUNAWAFANYAKAZI WANAOFANYIWA HUO UNYANG'ANYI NA UNYANG'AU TUWASILIANE KWA EMAIL lcccea@yahoo.co.uk
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Saa hizi niko huku Makete na nina mtu mwenye sifa hizo,je Makete kitongoji gani ili nimlete mkuu?
   
 17. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...naona kuna haja ya kuweka na umri, wasije wakakuletea kabinti ka miaka 13 kwakuwa tu kamemaliza darasa la saba!
   
 18. B

  Baba Shalom New Member

  #18
  May 17, 2009
  Joined: May 17, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani acheni utani huu mtandao tunaueshimu sana na tunataka uwe very professional effective na efficient for the future of our nation, so tusaidiane kikweli kweli
   
 19. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Achana naye Katabazi hayupo serious huyo! Alishatangaza kazi ya accountant, mi nikaMP he never responded to that PM na hakutoa feedack ya ile kitu iliendaje!
   
 20. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Malila,
  Tafadhali ni PM nitakueleza ila nitakupa hiyo nafasi kama ndg Makala hatoitaka.
  Mbu huo umri mbona ni mkubwa?Vitoto vyetu vya kiswahili mbona vinapika vitu vyote hivyo na kuwaangalia wadogo zake vikiwa hata darasa la 4/5?
  Next Level nina imani nilikupa feed back na hata kama hukuipata angalia kwenye ile thread niliandika kuwa nimempata na kuwashukuru wote.Niwie radhi usinitumbukize huko unakonisukumia.Na kama kweli hukupata huo ujumbe niwie radhi mkuu.
  Pia nawaomba nilio wajibu mnitetee kwa Next Level ili anitoe huko anakonipeleka.
   
Loading...