Maombi ya kazi ya kujitolea JamiiForums

Maombi ya kazi ya kujitolea JamiiForums

issa ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
1,319
Reaction score
260
Ndugu viongozi wa JamiiForums, mimi ni mtanzania mwenye umri wa miaka 29 nikiwa nina elimu ya chuo kikuu, naomba kuwasilisha maombi ya kuomba kazi ya kuwa MODERATOR wa KUJITOLEA katika kampuni yenu ya Jamii Media upande wa JamiiForums.

Sina uzoefu wa kutosha katika kazi hii lakini ninaahidi kuwa nitajituma kwa uwezo wangu wote na kujifunza kwa wafanyakazi nitakaowakuta bila kuwaangusha.

Nina uzoefu na elimu ya kutosha kuhusu maswala ya computer pia nimejifunza na nina uwezo mkubwa katika uandishi wa lugha za kiswahili na kingereza. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu nyote mtakao pitia maombi yangu na kuyatolea maamuzi chanya.

Wenu mtiifu ISSA RAMADHANI
 
Kumbuka zamani ulikuwa unajifanya pung@(samahani mods) tulikuonya uache utoto hukusikia sasa ww kwa tabia hiyo usizani mods wamekusaau..
 
Elimu Ya "Brain Resting Now" (BRN) Ni tatizo, hujui hata umri wako?
 
Kumbuka zamani ulikuwa unajifanya pung@(samahani mods) tulikuonya uache utoto hukusikia sasa ww kwa tabia hiyo usizani mods wamekusaau..

mkuu kuna kitu nimekieleza hapo juu kuwa ni mtaalam katika maswala ya lugha,hivyo naweza kuandika tukio lolote lile kutokana na mazingira husika na kuuvaa uhusika
 
We nshakustukia,shida yako ni kunipa ban mimi,najua ukishafanikiwa lengu lako utaachana na hiyo kazi unayoomba...
 
Elimu Ya "Brain Resting Now" (BRN) Ni tatizo, hujui hata umri wako?

Kuwa waelewa msikurupuke kumshusha hadhi mwenzenu kumbe mnajishusha nyie,
Mtu akisema umri wangu ni kati ya miaka 25 mpk 30 sio kama haujui mwaka wake ila hataki kukutajia mwaka wake moja kwa moja,
Kwa muelewa atajua watu wa rika hilo hua wako vp,
Km watafaa kwa jambo husika ama laa,

Mwngn husema nipo 20's
Akimaanisha miaka 30 hajafika so yupo kati ya 20 mpk 29.

Hope umenipata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom