Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,106
- 9,272
Kam kweli wataka panyooke hapo ni kumpeleka Spora Liana.
Tusameheane kidogo ila nimefatilia sana toka mwanzo mchakato mzima nimegundua hawa wabunge ni waongo sana wanadanganya wananchi na kwa kuwa hatuna uwezo wa kuhoji na sisi tunaendeleza mijadala kama vipofu.mimi nina maswali machache kama mwenyekiti aliweza kuwataja hadharani mtandao wa wakurugenzi mafisadi kwa majina Mbona Leo hatuambiwi ni nani amewatishia maisha CAG? ni mwongo huyo MZee anawapoteza huyo.atutajie na atuthibitishie Huyo aliyetishiwa maisha ni nani na katishiwa na nani.mwenyekiti mwongo sana na hata hizi taarifa anazotembea nazo nashindwa kuziamini ukweli wake.
Njoo Mwanza habari hiyo inajulikana wazi na vyombo vyote husika. External Auditors waliopo hapa wanaishi kwa wasiwasi hivyo taarifa siyo ya uongo.
Mkuu achana na huyo kilaza, huyo ni miongoni mwa wanufaika wakuu wa ufisadi huo
Kwanza anashangaa nini mkaguzi kutishiwa maisha kwa kusema ukweli dhidi ya mafisadi? Mbona kule Maswa OCD mzima alitwangwa makofi na mgombea Ubunge wa CCM eti kwa vile anauhusiano na magogoni? Au majuzi tuu ndani ya Bunge AG Werema alimwambia Kafulila atamkolimba yeye ni kama Tumbili tuu?
Vitisho vya mafisadi sio jambo geni kwa serikali inayoongozwa na kuwekwa mfukoni na watu wachache. Huu ni udhaifu ambao ni adimu sana kuupata hapa duniani. Ungepaswa kuingizwa kwenye vivutio vya utalii kuwa njooni muone mahali raia anavyoweza kuibwaga makofi serikali na ika Ufyata.
hivi yule mkurugenzi so alihamishwa?arudishwe awajibishwe ..kiboko take wenje.