Maofisa ofisi ya CAG watishiwa kifo

Maofisa ofisi ya CAG watishiwa kifo

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
mwanza_300_182.jpg

​
SAKATA la ubadhirifu wa bilioni 40 katika halmashauri ya jiji la Mwanza limechukua sura mpya baada ya maofisa wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) walioibua sakata hilo kudai kutishiwa maisha.

Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Rajab Mohammed Mbarouk wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yao mkoani hapa ambacho hakikuendelea kufanyika kutokana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia au mwakilishi wake kutofika katika majumuisho hayo.

"Tumepokea taarifa ya kutishiwa amani kwa baadhi ya wakaguzi, tunasema ofisi ya CAG ipo kisheria na kikatiba na wanafanya kazi kwa kufuata sheria na Katiba," alisema Mbarouk na kuongeza kuwa, kama wabunge watahakikisha wanatunga sheria na kuzisimamia na kwamba wakaguzi waendelee na kazi yao bila ya hofu.

Mbarouk alimpongeza Mkaguzi Mkazi pamoja na timu yake kwa kuwa na uzalendo wa kitanzania wa kutaka kuokoa uchumi wa Mwanza ambao kwa asilimia 90 unahujumiwa.
Alisema uchumi wa Mwanza unatokana na mapato na miradi ya maendeleo ambapo maeneo hayo yakifanyiwa kazi isiyoridhisha CAG anawajibu wa kutoa taarifa.

Alisema kama Mkaguzi Mkazi ameweza kuwasilisha taarifa yake kwa Bunge pamoja na kwa Rais. Awali, Mjumbe wa kamati hiyo, Kange Lugora alisema kamati hiyo iliishauri wizara husika kushirikiana nao pamoja tangu mwanzo wa ziara yao katika majumuisho ya kamati hiyo ili kubaini yanayotendeka katika miradi ya maendeleo.
"Kitendo cha wizara kutoshiriki katika majumuisho ya kamati hii ni kuendelea kuhalalisha ubadhirifu unaoendelea kwenye halmashauri, tunaonyeshwa miradi hewa na serikali ngazi ya wizara ilipaswa wajionee wenyewe," alisema.

Aliongeza kuwa, ili waweze kuwatendea haki Watanzania na wana Mwanza, kamati iliagiza kuwa hawawezi kuendelea na mahesabu ya halmashauri ya jiji la Mwanza hadi wizara itakapomrudisha Mkurugenzi wa zamani wa jiji hilo, Wilson Kabwe ambaye kwa sasa amehamishiwa Dar es Salaam.

Alisema kwamba wizara haijafanya jitihada za kumrejesha mkurugenzi huyo na kudai kuwa mazingira hayo yanawafanya washindwe kuwatendea haki Watanzania.
Alisema ili kamati ilinde heshima yake na kwa mazingira hayo hawataweza kufanya majumuisho kwani kwa kufanya hivyo ni kuwasaliti Watanzania.

CHANZO: Habari Leo
 
hivi yule mkurugenzi so alihamishwa?arudishwe awajibishwe ..kiboko take wenje.
 
Hakuna atakayekamatwa kwa ubadhirifu huo, Hapo wanamwanza inabidi wajifunze kupambana kama wenzao wa Arusha. Mbinu za uchakachuaji zilianza mapema tangu. ziara ya Kikwete siku ya maadhimisho ya ccm kule Mwanza alipotoa maagizo ya kwamba halmashauri ya Jiji na ile ya Ilemela sharti zirudi kwa ccm kwa Gharama yoyote.

Ikafuatia mizengwe ya umeya wa Ilemela na hatimaye Jiji la Mwanza vyote vikaangukia ccm kwa mshangao wa wengi ktk siasa za Tanzania. Kwa mara ya kwanza Chama kinachoongoza kwa kuwa na wajumbe wengi ndani ya Vikao vya Halmashauri kikashindwa uchaguzi kwa chama chenye wajumbe wachache karibu nusu ya wajumbe wa chama B

Hapa wanamwanza walipaswa kuingia Barabarani kukemea na kupinga Uchakachuaji mkuu uliotokea kwenye Uchaguzi ule, Badala yake Wananchi wa Mwanza wakawaachia Chadema atu watamaliza wenyewe... Haya sasa jioneni wenyewe ufisafi huu ndani ya Halamashauri yenu..!!!!

Mnamkabidhi Fisi Bucha......!!!!!!!!!!
Filipo Mungi Crashwise etc

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Kwa hii serikali hapo akua kuwajibishana, kwani kuanzia ngazi za juu mkowani hadi jiji wamepeana kindugunaization kwaiyo hata wakipiga pesa wao wanapeta tu!
Ebu tizama zile pesa walizopewa na BOT baada ya kubomowa Clinic ya makongoro mission ya watoto na wanawake Billion 3, wakaenda kujenga banda la kuku la thamani ya million 70 , zingine zikapigwa na kugawana wanafamiliya.
Siku hizi ikienda pale Jiji hata sehemu ya kupaki gari lako akuna maana kila mfanyakazi wa Jiji ana gari zaidi ya moja na magari yamejaa sana ukijiukiza hawa wafanya kazi wametowa wapi pesa za kununulia MAGARI yote hayo, utaambiwa chezea Jiji.
 
Jiji kwa ujumla limeoza sana na mie naunga mkono kweli alistahili kuitwa Jiji, kwani ujinga mwingi sana kila idara, kwa mfano km huna pesa (kitu kidogo) failing lako linafichwa mpaka uwatoe pesa yaani kwa ujumla kila mtu pale ni Boss,
 
Jamani huu ugonjwa aupo tu Jiji la mwanza ni nchi nzima, anapaswa ashike nchi mtu mwenye mahamuzi magumu ni kuwapiga chini wafanya kazi wote.
Afu kuweka mifumo mipya ya utendaji kazi na kuajiri upya vijana wasomi walio mtahani.
 
Huyo Mkurugenzi Wilson Kabwe aliyehusika na ubadhirifu huo hawezi kufanywa kitu na mamlaka yeyote, kwasababu analindwa na Pinda. Ndio maana hata baada ya wizi huo akamuhamishia Dar Es Salaam, Mimi huwa ninashangaa Watanzania wanaomuita Pinda mtoto wa Mkulima.
 
Jana niliwasikia wananchi wa Mtwara kama sikosei walikataa kupokea mradi wa maji baada ya kuona maji hayatoki.
Wananchi walisema wangechakachua watakavyo lakini maji yatoke lakini wao walipitiliza mpaka hata maji hayatoki...siasa mbaya ya kulea uovu itatufikisha pabaya.
 
mwanza_300_182.jpg

​
SAKATA la ubadhirifu wa bilioni 40 katika halmashauri ya jiji la Mwanza limechukua sura mpya baada ya maofisa wa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) walioibua sakata hilo kudai kutishiwa maisha.

Hayo yalibainishwa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Rajab Mohammed Mbarouk wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yao mkoani hapa ambacho hakikuendelea kufanyika kutokana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia au mwakilishi wake kutofika katika majumuisho hayo.

“Tumepokea taarifa ya kutishiwa amani kwa baadhi ya wakaguzi, tunasema ofisi ya CAG ipo kisheria na kikatiba na wanafanya kazi kwa kufuata sheria na Katiba,” alisema Mbarouk na kuongeza kuwa, kama wabunge watahakikisha wanatunga sheria na kuzisimamia na kwamba wakaguzi waendelee na kazi yao bila ya hofu.

Mbarouk alimpongeza Mkaguzi Mkazi pamoja na timu yake kwa kuwa na uzalendo wa kitanzania wa kutaka kuokoa uchumi wa Mwanza ambao kwa asilimia 90 unahujumiwa.
Alisema uchumi wa Mwanza unatokana na mapato na miradi ya maendeleo ambapo maeneo hayo yakifanyiwa kazi isiyoridhisha CAG anawajibu wa kutoa taarifa.

Alisema kama Mkaguzi Mkazi ameweza kuwasilisha taarifa yake kwa Bunge pamoja na kwa Rais. Awali, Mjumbe wa kamati hiyo, Kange Lugora alisema kamati hiyo iliishauri wizara husika kushirikiana nao pamoja tangu mwanzo wa ziara yao katika majumuisho ya kamati hiyo ili kubaini yanayotendeka katika miradi ya maendeleo.
“Kitendo cha wizara kutoshiriki katika majumuisho ya kamati hii ni kuendelea kuhalalisha ubadhirifu unaoendelea kwenye halmashauri, tunaonyeshwa miradi hewa na serikali ngazi ya wizara ilipaswa wajionee wenyewe,” alisema.

Aliongeza kuwa, ili waweze kuwatendea haki Watanzania na wana Mwanza, kamati iliagiza kuwa hawawezi kuendelea na mahesabu ya halmashauri ya jiji la Mwanza hadi wizara itakapomrudisha Mkurugenzi wa zamani wa jiji hilo, Wilson Kabwe ambaye kwa sasa amehamishiwa Dar es Salaam.

Alisema kwamba wizara haijafanya jitihada za kumrejesha mkurugenzi huyo na kudai kuwa mazingira hayo yanawafanya washindwe kuwatendea haki Watanzania.
Alisema ili kamati ilinde heshima yake na kwa mazingira hayo hawataweza kufanya majumuisho kwani kwa kufanya hivyo ni kuwasaliti Watanzania.

CHANZO: Habari Leo

Kiukweli jiji la mwanza limeoza linanuka rushwa, tena meya huyu aliyepo ndio tatozo kubwa, hana elimu ya kukabiliana na changamoto za jiji. Anapewa visafari vya nje ya nchi na kununuliwa visuti na wakuu wa idara, wenzie wanaiba mabilioni ya fedha za wananchi. Ameshiriki sana na ndg yake kabwe kuihujumu halmashauri ya jiji, lazima awajibishwe
 
watiwe ndani tu mwizi siyo wa kucheka naye kabisa.
 
hivi yule mkurugenzi so alihamishwa?arudishwe awajibishwe ..kiboko take wenje.

Hapo ndio tunapomkumbuka meya manyerere, alikuwa makini sana kulinda mali za umma. Leo meya huyu bishoo anaongeza malaya mjini tu, hana lolote. Ameshiriki sana kwenye wizi huu, madiwani wenzie wanamwambia achukue hatua hataki kwasababu ameshalambishwa. Na alivyo na upeo mdogo meya huyu anapewa vijisenti tu vya kutesea kwa malaya, huku mkurugenzi na wakuu wa idara wakichota mabilioni ya wananchi bila huruma. Tujifunze kuchagua mameya wenye elimu japo ya diploma itatusaidia. Haiwezekani jiji kubwa kama la mwanza meya awe hana elimu ya kutosha
 
watiwe ndani tu mwizi siyo wa kucheka naye kabisa.

Ni kweli mkuu! Na kinara wa mtandao huu ni huyo mnayemuita mtoto wa mkulima, kavuruga sana halmashauri kwa maslahi yake ya kutaka urais, sasa wakurugenzi wengi na mameya wamegeuka kuwa madalali wake wakuziibia halmashauri zetu kwa maslahi yake
 
Hapo ndio tunapomkumbuka meya manyerere, alikuwa makini sana kulinda mali za umma. Leo meya huyu bishoo anaongeza malaya mjini tu, hana lolote. Ameshiriki sana kwenye wizi huu, madiwani wenzie wanamwambia achukue hatua hataki kwasababu ameshalambishwa. Na alivyo na upeo mdogo meya huyu anapewa vijisenti tu vya kutesea kwa malaya, huku mkurugenzi na wakuu wa idara wakichota mabilioni ya wananchi bila huruma. Tujifunze kuchagua mameya wenye elimu japo ya diploma itatusaidia. Haiwezekani jiji kubwa kama la mwanza meya awe hana elimu ya kutosha

Jiji la mwanza limevurugwa sana na siasa. Sijui kama tutatoka hapa tulipokwama
 
Ukiona mahali CCM na serikali wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanaweka Meya wao ujue kuna wizi wa hali ya juu wanataka kuulinda. Ni wazi kuwa yeyote anayemlinda mwizi naye ni mwizi hivyo bila kumung'unya maneno CCM ni genge la wezi. Tena wezi na wauaji wakubwa sana.
Kwa mabilioni yote hayo yanayopotea kila mahali ni Watanzania wangapi wamepoteza maisha kwa huduma mbovu zinazopatikana kwa ukosefu wa fedha? La ajabu ni kuwa bado Watanzania haohao masikini wanaokosa huduma za afya, elimu bora na mikopo ya Elimu ya juu wanaendelea kuiunga mkono CCM kwa hadaa wanazopewa. Ifike mahali wote tuseme sasa basi.
 
Ukiona mahali CCM na serikali wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanaweka Meya wao ujue kuna wizi wa hali ya juu wanataka kuulinda. Ni wazi kuwa yeyote anayemlinda mwizi nayoe ni mwizi hivyo bila kumung'unya maneno CCM ni genge la wezi. Tena wezi na wauaji wakubwa sana.
Kwa mabilioni yote hayo yanayopotea kila mahali ni Watanzania wangapi wamepoteza maisha kwa huduma mbovu zinazopatikana kwa ukosefu wa fedha? La ajabu ni kuwa bado Watanzania haohao masikini wanaokosa huduma za afya, elimu bora na mikopo ya Elimu ya juu wanaendelea kuiunga mkono CCM kwa hadaa wanazopewa. Ifike mahali wote tuseme sasa basi.

Ndugu yangu hapa tulipifikia bila kufanya yale waliyofanya Burkins Fasso jana, tutapanga mistari ya kupiga kura sana wakati watawala wataamua wakitakacho
 
Tusameheane kidogo ila nimefatilia sana toka mwanzo mchakato mzima nimegundua hawa wabunge ni waongo sana wanadanganya wananchi na kwa kuwa hatuna uwezo wa kuhoji na sisi tunaendeleza mijadala kama vipofu.mimi nina maswali machache kama mwenyekiti aliweza kuwataja hadharani mtandao wa wakurugenzi mafisadi kwa majina Mbona Leo hatuambiwi ni nani amewatishia maisha CAG? ni mwongo huyo MZee anawapoteza huyo.atutajie na atuthibitishie Huyo aliyetishiwa maisha ni nani na katishiwa na nani.mwenyekiti mwongo sana na hata hizi taarifa anazotembea nazo nashindwa kuziamini ukweli wake.
 
Kwa hii serikali hapo akua kuwajibishana, kwani kuanzia ngazi za juu mkowani hadi jiji wamepeana kindugunaization kwaiyo hata wakipiga pesa wao wanapeta tu!
Ebu tizama zile pesa walizopewa na BOT baada ya kubomowa Clinic ya makongoro mission ya watoto na wanawake Billion 3, wakaenda kujenga banda la kuku la thamani ya million 70 , zingine zikapigwa na kugawana wanafamiliya.
Siku hizi ikienda pale Jiji hata sehemu ya kupaki gari lako akuna maana kila mfanyakazi wa Jiji ana gari zaidi ya moja na magari yamejaa sana ukijiukiza hawa wafanya kazi wametowa wapi pesa za kununulia MAGARI yote hayo, utaambiwa chezea Jiji.
ni shida......kweli kweli.hatari sana.
 
Nchi hii imekosa uwajibikaji. Kila mtu anakula awezavyo, mamlaka zinaangalia tu!
 
Tusameheane kidogo ila nimefatilia sana toka mwanzo mchakato mzima nimegundua hawa wabunge ni waongo sana wanadanganya wananchi na kwa kuwa hatuna uwezo wa kuhoji na sisi tunaendeleza mijadala kama vipofu.
mkuu nakuunga mkono,wanasiasa wanatuchonganisha na clients,kwa utafiti niliofanya,hakuna mkaguzi wa Mwanza aliyeripoti kwa kamati kwamba katishiwa maisha,bunge limeibuka tu,na hii inatuchonganisha na wateja wetu,kama kuna mtu katishwa kwa nini asitajwe na kuchukuliwa hatua,mda mwingine hizi ni mbinu za wabunge kutaka wakatiwe chao,au jiji limegoma kutenga fungu la kamati
 
Wewe kama hujui chochote ni vyema ukasoma comments za watu wanaolijua jambo hilo. Unajua kuna mkaguzi wa ndani hapo jiji amejengewa zengwe mpaka la kushushwa cheo kwa sababu ya kusimamia maadili ya kazi yake? Kutoka mkaguzi wa ndani na kuandikiwa barua ya kupelekwa kuwa mhasibu wa shule ya sekondari, kama wameweza hivyo watashindwaje kutishia maisha watu? Sitaki kuamini kuwa na wewe ni miongoni mwa wanufaika wa ufisadi huo
 
Back
Top Bottom