Manyara: Watu wawili wauawa wakicheza na tembo

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia kundi la Tembo saba kuingia katika makazi ya Watu katika Kata ya Dumbeta Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara ACP George Katabazi amesema " waliofariki Wanaume wawili na majeruhi wawili huku mmoja akiwa ni Mwanamke ambapo kwa taarifa tulizopata ni kwamba mmoja alikuwa akimshika mkia Tembo na mwingine akipiga nae picha kwahiyo hao Tembo ndipo wakacharuka"

"Nitoke wito kwa wakazi mkoa wa Manyara kuacha kuchezea wanyama wakali kama Tembo,Simba na wanyama wengine wakali maana hao hawana tabia za kibinadamu bali wanatabia za wanyama ila kama kuna Mtu anataka kupiga picha na wanyama zipo Mamlaka husika na taratibu zipo, hivyo wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapoona matukio kama haya kwenye Maeneo yao ili Mamlaka zinazohusika ziweze kuwadhibuti" RPC Katabazi.

Chanzo: Millad Ayo
 
Swaga Swaga....Conservation initiative

Hao walikuwa wanaitafuta Hanang ...wigo wa Tembo umerudi kama zamani...hiyo ni connectivity kati ya Kusini na Kaskazini Ruaha Tarangire Itigi Swaga Swaga.....

Wa kulaumiwa ni Tawiri watafiti mnakaa sana Maofisini.....Movement za Tembo zifuatiliwe mahali popote walipo ...kunasiku watu wa Mrombo Arusha mta Tafutana

Tumeuwa Malihai Club Mashuleni hiki kizazi hakijuwi Tabia za wanyama hatari kama Tembo ....

R.I.P Alfred Kikoti _ Mtafiti wa Tembo Mahili Kusini mwa Jangwa la Shahara
 
Back
Top Bottom