Manyara: Watu wawili wauawa wakicheza na tembo

Kuna ndugu yangu yupo hapo Katesh aliniambia mpaka jioni idadi ya waliouwawa ilifika watu tisa.

Anasema mamlaka hasa police walijitahidi kuzui watu kuwasogelea lakini ndio hivyo watu walikua wengi na wabishi sana
 
Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kufuatia kundi la Tembo saba kuingia katika makazi ya Watu katika Kata ya Dumbeta Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara ACP George Katabazi amesema " waliofariki Wanaume wawili na majeruhi wawili huku mmoja akiwa ni Mwanamke ambapo kwa taarifa tulizopata ni kwamba mmoja alikuwa akimshika mkia Tembo na mwingine akipiga nae picha kwahiyo hao Tembo ndipo wakacharuka"

"Nitoke wito kwa wakazi mkoa wa Manyara kuacha kuchezea wanyama wakali kama Tembo,Simba na wanyama wengine wakali maana hao hawana tabia za kibinadamu bali wanatabia za wanyama ila kama kuna Mtu anataka kupiga picha na wanyama zipo Mamlaka husika na taratibu zipo, hivyo wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapoona matukio kama haya kwenye Maeneo yao ili Mamlaka zinazohusika ziweze kuwadhibuti" RPC Katabazi.

Chanzo: Millad Ayo
Tafiti ianzie hapa

Inasemekana Tembo walianza ku ditekti mitetemo ya Mlima Hanang...na kuanza kuondoka kwenye hilo eneo la mzingo unao zuunguka Mlima
 
Back
Top Bottom