Manyara: Mtendaji wa Kijiji ahukumiwa Miaka 41 jela kwa Ubadhirifu, Matumizi mabaya ya Madaraka na Wizi wa Mali ya Umma

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,614
Aprili 25, 2023, Mahakama ya Wilaya ya MBULU imemtia hatiani Mshtakiwa Bw. SAMWEL QAMBINA DUKHO, katika Shauri la Uhujumu Uchumi Na.06/2022.

Shauri hili lilikuwa mbele ya Mh. Victus KAPUGI na liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka MARTINI MAKANI

Katika shauri hilo mshtakiwa alikua anashtakiwa kwa makosa matatu.

I) Ubadhirifu, ambapo kahukumiwa miaka 20 jela.

II) Matumizi mabaya ya madaraka, ambapo kahukumiwa miaka 20 jela.

III) Wizi katika utumishi wa Umma, ambapo kahukumiwa mwaka mmoja jela.

Mshtakiwa ataitekeleza adhabu hiyo kwa pamoja (concurrently) na Mahakama imemtaka Mshtakiwa kurejesha fedha shs. 3,687,000/= ambazo alizifanyia ubadhirifu au mali yake iuzwe ili kufidia deni hilo.


Chanzo: TAKUKURU
 
Aiseee.....

Wizi wowote ni mbaya ila vidagaa kupewa adhabu kubwa na kuacha kambale wanaturingishia ndevu zao ndio Huwa sielewi Inatumika kanuni gani.

Milioni tatu na nusu imfunge mtu miaka 20!?
 
Hii Hukumu ukiifatikia sanaz utagundua Huyu Hakimu alitaka kitu kidogo ,kikakosekana.


Yaan mafisadi makubwa yapo mtaan, anagonga nyundonzote hizo Kwa mtu ambaye hata kula yake ni ya kuhesabu
 
Wanaoiba mabilioni,either wanamaliza kesi nje ya mahakama kwa kisingizio cha makubaliano na DPP au wanaombwa na Mama waache hiyo tabia mbaya au mama anawaomba warudishe hizo pesa za umma.
Pathetic
 
Hahahahah daaah

Wakati watu wanapiga bilions of shilings wanadunda tu kitaa.

Masikini mtendaji wa kijiji kala vilaki laki anaenda kunyea debe hadi kufa kwake.

Kweli duniani hakuna haki.
 
Mimi namsubiria yule aliyeitwa "$tupid" na mama naye agongwe mvua zake za kutosha. 🙄
 
Back
Top Bottom