Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,280
Jeshi la Polisi mkoani Manyara linamshikilia mwanamke Janeth Doto Vicent mkazi wa mji wa Babati kwa tuhuma za kumchoma Mtoto wake wa kike sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Marrison Mwakyoma amesema ilikuwa septemba 12/ 2021 majira ya saa tatu asubuhi katika mtaa wa Mrara Juu mjini hapo, ambapo mtoto huyo wa miaka mitatu alichomwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali baada ya kuchukizwa na kitendo cha mtoto wake kuomba fedha kwa mpita njia.
Mwakyoma amesema kuwa kitendo hicho kilimfanya mama huyo kumchoma usoni shingoni na kumsababishi majeraha ndipo wasamaria wema walivyoona kitendo hicho waliamua kutoa taarifa katika kituo cha polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwakyoma mtoto huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati, Mrara.