Manyanyaso uoenevu ni udhaifu wa katiba iliyopo, CCM/UKAWA sio jukumu lao

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,144
2,000
Ni wazi kabisa kua CCM ndio maadui wakubwa wa upatikanaji wa katiba mpya katika taifa letu ili waendelee kuyalinda maslahi yao binafsi, hawana huruma na hali ilivyo nchini. Wanapiga kelele kwamba taifa linaibiwa ilihali wao ndio walikua wasimamizi wa rasilimali za taifa letu, wanamlaumu nani kama wao ndio waliokua wakiingia mikataba na wezi?Wanalialia kutafuta huruma za wananchi ilihali ukweli uko wazi.

CCM hawawezi kuliundia taifa hili katiba mpya, hata UKAWA hawawezi kuliundia taifa katiba mpya. Katiba itatafutwa na wananchi wenyewe, kila mwananchi anajua kabisa kinacholiangamiza taifa hili ni katiba mbovu mbovu inayowapa watawala mamlaka kuendesha kila kitu. Kinacholiumiza taifa hili ni wenye mamlaka kuitumia katiba iliyopo kwa maslahi yao wenyewe kwa sababu inawapa mwanya huo.

Katiba gani isiyompa nafasi mgombea kupinga matokeo ya Urais mahakamani? Ni katiba gani hii mkuu wa nchi anateua wakuu wa wilaya,mikoa,wakurugenzi,Makatibu tawala na watendaji wote wa mamlaka nyeti za serikali? Yaani inampa kutengeneza chain yake kuendelea kufanya atakavyo kwa vile hakuna wa kumhoji.

Sio kazi ya Rais au wapinzani kuamua katiba ipatikane, hili ni suala la wananchi wenyewe, taifa wenye raia zaidi ya million 50 haliwezi kuendeshwa kwa mifumo ya kizamni ni lazima likwame tuu. Rais hana uwezo wa kuamua kupatikana kwa katiba bora, hilo haiwezekani. Duniani kote mabadiliko ya kikatiba huletwa na wananchi na sio watawala, hakuna mtawala anayeweza kukubali mwenyewe kujipunguzia mamlaka.

Vyeo vya wakuu wa mikoa na na wilaya viondolewe, tuchague Magavanor na Senators watokanne na sisi na sio kuteuliwa na wanasiasa,mfumo wa kiutawala waweza kubadilishwa na katiba mpya. Katika vyeo vya ajabu kwenye taifa hili ni pamoja na hivi. Wananchi ifike pahali tuseme imetosha kuteseka,tuamue sisi wenyewe kuidai katiba yenye maslahi kwa taifa na sio kupangiwa na watu wachache.

Leo hii watumishi wa umma wanalia na malimbikizo ya madai yao, hakuna nyongeza kwenye malipo yao,hawapandishwi madaraja kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa kisheria. Unaenda mwaka wa tatu mamlaka ziko kimya juu ya hili wala hakuna hatua zinazochukuliwa, yaani maisha gharama zinapanda kila siku na hawa watumishi wa umma wanaendelea kuteseka bila kuonewa huruma na majukumu yao yanaendelea.Maslahi ya mtumishi wa umma sio suala la mtu kuamua kupanga atakavyo bali ni suala la kisheria na ni lazima.

Ifike mahali tulikumboe taifa hili kwa kujitengenezea utaratibu wenye sauti za wengi na sio kuamuliwa na watu wachache, ifike mahali wakuu wa wilaya na mikoa wasahaulike kabisa kwa utaratibu wa katiba mpya,nafasi zao zielekezwe kwa governors na senators nakuna kitakachoongezeka zaidi ya kubadilisha vyeo na mifumo tuu wa kiutendaji na upatikanaji wao.

Majaji na mahakimu wetu wanakabiliwa na mashinikizo ya kisiasa kufanya maamuzi kwa vile wateuzi wao ni mamlaka za kisiasa, Watumishi hawa wanakosa utashi wa kufanya kazi zao kitaaluma kwa hofu ya kukosa kazi zao.Kama katiba itaamua nafasi zao zitokane na mamlaka zilizo huru nadhani watafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia taaluma zao na sio maagizo kutoka juu.Haiwezekani jaji anatoa Order ya kuzuia nyumba flani isibomolewe lakini kwa sababu kuna watu wana mamlaka wanapuuzia maagizo hayo. Tuondoke huko, tutafute katiba iliyo bora ituongoze katika mwanga bora.
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,619
2,000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,144
2,000
Pamoja na kuitwa malofa, lazima tukubaliane kwamba katiba yetu iliyopo hivi sasa bado haitoi nafasi kwa kiongozi teyoyote kulikomboa taifa hili.
 
morenja

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
4,361

Sio siri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom