Manufaa ya uongozi na muundo wa Utawala unaozingatia watu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,030
59B40482-A069-484D-8855-C460A473F791.jpeg



Wengi wamehoji kwamba serikali nzuri inajulikana kutokana na uwezo wake wa kutimiza mahitaji ya raia wake pamoja na kuzingatia matakwa ya watu. Lakini yamkini imethibitishwa kuwa utawala bora ni wazo ambayo wakati mwingi ni vigumu kuafikia kwa jumla.

Walakini, kama inavyoonekana katika sehemu zingine za ulimwengu, kupitia hatua kabambe, kuna uwezekano wa kutimiza ndoto hii.

Katika juhudi za kujenga jamii yenye uchumi mzuri, kwa mfano, China imekuwa ikipambana kubadili hali ya kiuchumi ya raia wake. Kasi ya maendeleo iliyoshuhudia hivi karibuni nchini humo inaonyesha mabadiliko ya kihistoria yaliyofanyika katika China ya leo.

Ni ukweli unaojulikana kuwa wakati Chama cha Kikomunisti kilipata udhibiti wa nchi mnamo 1949, China ilikuwa jamii ambayo watu wengi walikuwa masikini na wenye kutegemea kilimo pakubwa.

Na ili kubadili hatma yake, na kufikia kilele cha ustawi pamoja na kubadili mstakabali wa raia wake, China ilianza kwa kushughulikia mambo kadhaa makuu ya maendeleo ya taifa, kama uchumi, afya, na elimu. Ilifanya hivyo kwa kanuni ya msingi ya kuwekeza katika watu wake na kuwahudumia raia.

Hii ndio sababu mwishoni mwa miaka ya 1970, uongozi wa CPC ulianzisha mageuzi kadhaa katika maeneo ya kilimo, tasnia, sayansi na teknolojia, na vile vile katika idara ya majeshi ili kuifanya China kuwa taifa muhimu la viwanda na ambao mafanikio yake yangemnufaisha kila mtu nchini siku za baadaye.

Kwanza, ili kumaliza kiwango cha juu cha kutojua kusoma na kuandika na kuwa na nguvu kazi endelevu na ya kutosha, China ilifanya masomo kuwa ya lazima. Kila mtoto sasa lazima aende shule angalau miaka 12, huku ada ikitolewa na serikali. Idadi kubwa ya watoto huhudhuria shule za serikali.

Kabla ya mageuzi haya katika tasnia ya elimu, kulikuwa na tofauti kubwa katika ubora wa shule, kati ya shule za mjini na vijijini. Serikali za mikoa zilitarajiwa kutoa ufadhili kwa shule na mara nyingi mikoa masikini sana yalikuwa na uchumi mdogo na hayakuweza kuwekeza katika vituo vipya vya masomo au kuwaajiri walimu. Maelfu ya watoto wa wahamiaji pia hawakuwa na haki ya kupewa nafasi katika shule ya mtaa.

Pili, ili kuunga mkono kilimo, serikali imeifanya iwe rahisi kwa wakulima kupata mkopo ili waweze kuwekeza na kuongeza mapato yao ya kilimo. Serikali pia imekata kodi kwa wakulima na kuongeza msaada wa kilimo na wa kiufundi unaotolewa kwa wakulima ili kufanya shughuli hii ya ukulima iwe na faida zaidi.

Mbali na hilo, pamoja na uhuru wa kukuza mashamba yao na kuuza mazao yao sokoni, mapato ya wakulima yameongezeka.

Ukuaji wa sekta zisizo za kilimo pia huwapatia watu vijijini fursa za kazi. Biashara ya jiji na biashara ya vijijimaarufu kama TVEs ilikua kwa kasi zaidi kuliko viwanda vya mjini. Biashara hizi zinazomilikiwa kwa pamoja na wakulima ndio asili ya viwanda vijijini ambavyo vilifanyika uti wa mgongo wa maendeleo ya China.

Mara tu baada ya kuanzishwa kwa taifa la Jamhuri ya watu wa China, ukulima uliendeshwa kwapamoja. Hakukuwa na motisha ya kifedha ya kufanya kazi kwa bidii na kwa hivyo uzalishaji wa kilimo ulikuwa duni mno.

Katika mageuzi makubwa yaliyofanywa na CPC mwaka 1978, ulianzishwa mfumo wa uwajibikaji ambao unaruhusu wakulima kufanya ukulima kama wamiliki na kupata faida. Pato la ukulima kwa haraka lilianza kuongezeka. Leo uhaba wa chakula nchini China si tishio ikilinganishwa na ilivyokuwa zamani.

Sehemu nyingine ambayo imeshuhudia mageuzi makubwa nchini China ni sekta ya afya. Kwa miaka, mfumo wa utunzaji wa afya ulikuwa wa hali mbaya. Muundo wake ulikuwa hafifu na gharama ya matibabu ilikuwa ghali mno kwa maskini wa vijijini. Hiiilichochea serikali kuanzisha mfumo mpya wa ushirikiano wa matibabu vijijini ili kufanya huduma ya afya iwe nafuu zaidi.

Chini ya mpango huu, asilimia 40 ya gharama ya huduma ya afya ya raia hulipiwa na serikali kuu, asilimia nyingine 40 hulipwa na serikali ya mkoa huku asilimia 20 iliyobaki ikigharamiwa na raia. Katika mpango huu, serikali inagharamia jumla ya asilimia 80 ya bili ya hospitali.

Serikali ya Rais Xi na chama cha CPC pia inatekeleza mpango wa Afya China 2020, ambao unanuia kutoa huduma za afya na matibabu kwa wote nchini China ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Jambo lingine ambalo lilivutia umakini wa serikali na chama ilikuwa ukosefu wa usawa wa kimaendeleo. Ikilinganishwa na miongo miwili iliyopita, na ili kufanikisha maendeleo ya uchumi wa haraka na endelevu, serikali imeongeza uwekezaji katika miundombinu kama vile barabara, na usambazaji wa umeme na ule wa maji hadi vijijini. Kupitia miradi hizi serikali imeweza kufungua sehemu za mbali na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maendeleo.

Inafahamika kuwa mamilioni ya watu wa China waliondoka mashambani kutafuta kazi katika miji. Idadi ya wahamiaji hawa ilizidi kuongezeka kwa sababu kazi katika miji ilikuwa ya kulipwa vizuri pamoja na upatikanaji wa fursa za kujiendeleza ikilinganishwa na sehemu za vijijini.

Lakini zamani, ilikuwa hatia kwa watu kutoka vijijini kwenda kuishi katika miji bila kibali maarufu kama "hukou". Mfumo huu uliunganisha kila raia na wilaya yake na anapoondoka alikuwa anakosa baadhi ya haki, licha ya kukosa kufaidika kutokana na vitu kama matibabu au masomo.

Hata hivyo, serikali ilianza kuondoa mfumo huo wa kuwa na kibali na kukomesha kibali cha makazi ya muda baada ya kugundua kuwa uchumi wa China ungefaidika kutokana na kupunguza vikwazo kwa wafanyakazi.

Mipango hii inatekelezwa kwa ushirikiano wa chama na serikali kama jibu la moja kwa moja kwa mahitaji ya wananchi huku kukiwa na juhudi za kukuza uchumi wa nchi pamoja na kukuza mazingira dhabiti ya kijamii na kisiasa.

Falsafa inayozingatia matakwa ya watu sasa inaonekana kukita mizizi katika mfumo wa utawala wa China ambayo katika kila nyanja inaonekana kuwahudumia raia wake vizuri. Hii, kwa upande mwingine, imepunguza tofauti iliyoko kati ya raia na serikali na badala yake kuchochea raia kuunga mkono serikali na sera zake.
 
Back
Top Bottom