Mantiki ya kaulimbiu MATAGA katika serikali ya awamu ya tano

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Kwa muda kidogo nimeona watu wakishindwa kuelewa kwa nini Serikali ya Awamu ya Tano imekua "branded" na kauli ya Make Tanzania Great Again au MATAGA

Tujielekeze kwenye kuimulika miradi inayotekelezwa na Serikali hii.

Kuna aina mbili za miradi inayofanywa SERIKALI ya Awamu ya 5 katika utekelezaji wa kihistoria ya Ilani ya uchaguzi.

1. Miradi iliyokuwepo na kuifanya Tanzania kuwa kubwa ikafa au kutetereka hii inafaa kuitwa MATAGA (Make Tanzania Great Again)

a ) Hapa mfano ni kama vile kufufuliwa kwa ATCL ndege zaidi ya 10 ,

b )TRC reli ya zamani kuboreshwa na baadhi ya njia kufufuliwa ikiwemo reli ya Moshi na Arusha

c) Nchi hii ilikuwa na VIWANDA vingi, Kutilia mkatazo Uchumi wa Viwanda ufufuaji wa Viwanda vilivyokuwa vimeterekezwa.

d ) Elimu bure kwa elimu ya msingi na sekondari.

e ) Kurudisha uwajibikaji, Utendaji na hadhi ya Utendaji wa SERIKALI kwa mujibu wa MAADILI na misingi ya UTUMISHI wa umma..

Hii ni mifano michache sana jinsi SERIKALI ya Awamu inavyofanya kazi kubwa ua kuirudisha Tanzania kwenye ukubwa wake wa zamani na kuzidi mwanzo.

2. Kuna miradi inayofaa kuitwa (MATAG) Make Tanzania Greatest

Hii ni miradi ambayo HAIJAWAHI kufanyika wala kuwepo tangu UHURU wa Nchi hii yaani Orodha yake ni kubwa kweli kweli

Hapa ndio penye Miujiza mingi sana

a ) Ujenzi wa SGR

b ) Ujenzi wa Nyerere Hydroelectric Power House kule Rufiji

b ) Ujenzi wa Barabara mpya kila kona ya nchi ikiwemo huko Pembezoni kama Mpanda ,Ruvuma Kigoma nk

c ) Ujenzi wa hospital na vituo vipya vya Afya kila kona ya nchi.

d ) Ujenzi wa flyovers Tazara , Ubungo, 8 lines highways kwenye Barabara ya Morogoro.

e ) Ununuzi wa Meli mpya katika maziwa yote ya Nyasa Tanganyika Victoria..

d ) SERIKALI KUHAMIA RASMI DODOMA NA DODOMA KUWA MJI MKUU RASMI WA NCHI KISHERIA..

Orodha ni orodha ya Miujiza ya Awamu ya 5 ndani miaka minne ni kubwa sana mpaka mimi uwa najiuliza imewezekanaje hapa Tanzania

Kwa kweli kwangu mimi Mhe. Rais Magufuli na SERIKALI yetu ya Awamu hii ya Tano hawajafanya kazi WAMEFANYA MIUJIZA YA KUSHANGAZA.
 
Kama si mdudu Corona tungesonga mbele sana.Lakini yote ni mitihani katika maisha.

Lakini yatubidi tutafute vianzo vingine vya mapato japo sio rasmi.

Tuna majeshi yetu DRC,tunalinda amani kule lakini hatuchumi kitu kama Rwanda, Uganda na Kenya wasio na majeshi.No free lunch, tuanze kuchuma kwa speed ya 5G.
 
Unasubiri nani akuwekee namba ya simu sasa?

Imekuwaje leo hujaweka, si unawekaga wewe kila siku namba?
 
Back
Top Bottom