Manowari za Marekani hazikuwa zinaelekea Korea Kaskazini

dtj

JF-Expert Member
Nov 29, 2014
1,332
1,375
Wakuu.

Kwakuwa, siwezi kucomment kwenye Uzi wa Siasa za USA naomba wazee wangu

Cc Mag3 na Nguruvi

Mnisaidie hapa, Mara ya kwanza Potus alidanganya kuhusu Sweden kuna maafa, tena juzi kadanganya kuwa meli ya kivita inaelekea NK lakini LEO CNN inasema ile meli ilikua inaenda kufanya mazoezi Australia.

Inakuaje taasisi Kama ya Rais marekani inakua haiko systematic?

Inakuaje Rais anakoseakosea Sana tena kwenye hadhara?

Kuna hatari gani kama rais ataendelea kukosea hivi?

[HASHTAG]#Tusemezane[/HASHTAG]

0a55a07e9b7614f13d6b0e26ea60209a.jpg
 
Marekani ni mwoga sana kwenye vita, yaani ni kama mwanamke anayeogopa giza hulazimika kumchukua hata mtoto mdogo wa kiume ndio huwa na ujasiri. Marekani bila kupata uungwaji mkono haigusi Korea katu!!. Ni mwoga sana, alishawahi kuingia peke yake kupambana na Vietnam muulize alichokipata, bila washirika haingii vitani, saiz anampango wa kupmba kampani kwa mataifa sita(Japan,S.Korea,China, France, Britain na Germany) akikubaliwa ndio atalianzisha. But France wanamasuala ya uchaguzi kwasasa na China hawapo tayari kwasababu China ni mshirika mkubwa wa N.Korea, na Russia ambao wapo against U.S.A

Bila washirika tutaendelea kuzisikia bit tu za Trump ila Kumgusa Mapank hana jeuri hiyo
 
Huyu jamaa na US ni vigeuvigeu vitisho Vinci kumbe sasa hivi wameamua kudanganya kwamba hawa kutuma "armada" kuelekea north Korea ni upuuzi kufanya watu hawana akili. Hapo hakuna vita wala nn.
 
Mkuu mi nilidhani kukosea kosea ni huku tu, kumbe mpaka Washington DC. Naona kuna dalili ya US kuanza kupoteana.
 
Timeline of recent tensions

8 April: The US military orders a navy strike group to move towards the Korean peninsula

11 April: North Korea says it will defend itself "by powerful force of arms"

15 April: North Korea puts on a huge military parade - complete with missiles - to mark 105th birthday of the nation's founding president, Kim Il-sung. Meanwhile US Vice-President Mike Pence arrives in South Kore

a
16 April: North Korea conducts a rocket test, but it fails

17 April: Senior North Korean official tells the BBC the country will continue to test missiles "weekly" and Mr Pence warns North Korea not to "test" Donald Trump

18 April: It emerges the US Navy strike group was not heading towards North Korea when US officials said it was
 
_95696150_b9a8a15a-d6ac-420b-b1fc-c679b09723a6.jpg
Kundi la meli za kivita za Marekani, ikiwemo meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita, hazikuwa zinaelekea upande wa Korea Kaskazini kama ilivyoripotiwa awali, bali zilikuwa zinaelekea eneo tofauti.

Jeshi la wanamaji la Marekani lilikuwa limetangaza 8 Aprili kwamba kundi hilo la meli likiongozwa na meli kubwa ya Carl Vinson lilikuwa likielekea rasi ya Korea, kama hatua ya kuionya Korea Kaskazini.

Wiki iliyopita, Rais Trump pia alitangaza kwamba kundi kubwa la meli za kivita lilikuwa likitumwa eneo hilo.

Lakini imebainika kwamba ukweli ni kuwa meli hizo zilikuwa zinaelekea eneo tofauti.

Kufikia mwishoni mwa wiki, zilikuwa zimesafiri mbali sana na rasi ya Korea na zilikuwa zinapitia mlango wa bahari wa Sunda kuingia katika Bahari ya Hindi.

Wakuu wa jeshi la wanamaji la Marekani katika Bahari ya Pasifiki walisema Jumanne kwamba walikuwa wamefutilia mbali safari ya meli hizo katika bandari ya Perth.

Hata hivyo, wanajeshi wake walikuwa wamekamilisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyokuwa yamepangwa awali kati ya majeshi ya Marekani na Australia katika pwani ya kaskazini magharibi mwa Australia.

Baada ya mazoezi hayo, meli hizo zilielekea Singapore tarehe 8 Aprili.

Kundi hilo la meli sasa "linaelekea Magharibi mwa Pasiki kama lilivyoamrishwa".

Mwandishi wa BBC anayeangazia habari za Korea Stephen Evans anasema bado haijabainika iwapo kulitokea suitafahamu katika mawasiliano au labla Marekani ilipotosha watu makusudi kujaribu kumtia wasiwasi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Awali, Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alionekana kutoyumba alipohutubia wanahabari akiwa kwenye meli ya kivita ya USS Ronald Reagan ambayo imetia nanga Japan.

Aliapa kwamba Marekani iko tayari "kushinda shambulio lolote na kukabiliana na matumizi yoyote ya silaha za kawaida au za nyuklia kwa nguvu zake zote."

Korea Kaskazini na Marekani zimekuwa zikijibizana vikali viki za hivi karibuni na safari ya meli hizo ilikuwa imeibua uwezekano wa Marekani kutekeleza shambulio la mapema kujaribu kulemaza mfumo wa kijeshi wa Korea Kaskazini.

Jumatano, Bw Pence alitaja taifa hilo kuwa "tishio kubwa zaidi na la dharura kwa amani na usalama" katika maeneo ya Asia na Pasifiki.

Chanzo: BBC Swahili
 
"All options are on the table" by POTUS. Kombora la kwanza likitua Pyongyang hamkawii kurudi hapa mbiombio "anaonewa" ila sasa hivi, aaah; "athubutu aone". Ndugu yangu, hata simba anapowinda porini huko mojwapo ya tekniki anazotumia ni "kupotezea"; anajifanya hana habari na kiumbe alichokiweka kwenye target yake; ila akianza kufanya kweli, hamkani si shwari, pori zima kila mmoja atafuta kunusuru uhai wake wakati mzee mzima akijipatia mlo wa siku. Subiria uone kazi; sio propaganda uchwara za ziwa ni letu; sio letu zile; ni game la kiutu uzima.
 
Last week, President Trump said that he hadn’t realized how difficult it would be to disarm North Korea until he received a short history lesson from Chinese President Xi Jinping. "After listening for 10 minutes, I realized it’s not so easy!"
Trump confessed to the Wall Street Journal.

WE ALL KNEW THAT MR. SMART GUY - GO TAKE A NAP!
 
Last week, President Trump said that he hadn’t realized how difficult it would be to disarm North Korea until he received a short history lesson from Chinese President Xi Jinping. "After listening for 10 minutes, I realized it’s not so easy!"
Trump confessed to the Wall Street Journal.

WE ALL KNEW THAT MR. SMART GUY - GO TAKE A NAP!
 
Mapanki wasimuchukilie kama hizibollah na wanamgambo wakikurd, hilo ni taifa huru lenye teknolojia ya hali ya juu sana, propaganda za marekani hulenga kuligawa taifa kwa kuwaunga mkono waasi dhidi ya serikali, N.Korea its a patriotic and fidelity nation, hawana nafasi ya kuweka mashirika yao ya kichochezi, it will still united forever!!!
USA the nation of lucifer
 
Back
Top Bottom