Nini kitatokea Marekani, Korea Kaskazini zikipigana vita?

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
WAKATI Korea Kaskazini ikidai kuwa inaweza kuzamisha meli inayoendeshwa na nguvu za kinyuklia yenye iwezo wa kubeba ndege za kivita, wataalamu wanatazama itakuwaje iwapo vita hii na Marekani itatokea.

"Hata kama ni shambulizi kali dhidi kuteketeza mifumo ya makombora na uwezo wa kinyuklia, Korea inaweza kuhisi kwamba ina wajibu wa kujibu mapigo. Huu ni utata ambao wanamikakati na waandaa sera wanakabiliana nao," linaripoti shirika la habari la AFP

“Sasa wakati tunamiliki nguvu kubwa ya kinyuklia kujilinda kutokana na tishio la nyuklia kutoka kwa Marekani, tutajibu bila kusita kwa vita kamili dhidi ya vita kamili na vita ya kinyuklia kwa njia yetu ya shambulizi la kinyuklia, na tutakuwa washindi wakati wa mapambano ya mwisho dhidi ya Marekani.”

Hilo ni moja kati ya matamshi mengi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Korea Kaskazini wakati nchi hiyo ikiendelea kuongeza majaribio ya makombora na mradi wake wa kinyuklia.

Jumapili iliyopita chama kinachotawala cha Wafanyakazi kilisema kwamba majeshi ya nchi hiyo “yako tayari kuizamisha meli inayobeba ndege za kivita na inayoendeshwa kwa nguvu za kinyuklia kwa shambulizi moja tu.”

Maoni ya mhariri wa gazeti la Korea Kaskazini aliifananisha meli hiyo ya USS Carl Vinson na “mnyama tu.”

Lakini, kKuanzia kwenye gwaride kubwa lililohusisha maonyesho ya makombora ya masafa marefu katikati ya Pyongyang huku ikitishia “shambulizi la maangamizi” dhidi ya maadui zake wa Marekani, kuna ishara kuwa serikali ya Kim Jong Un inaanza kusalimu shinikizo la kimataifa.

Donald Trump amejaribu kutumia lugha kali, na kutishia “kukabiliana sawasawa” na Korea Kaskazini iwapo China inashindwa kumdhibiti mshirika wake na kupeleka kile alichoeleza kuwa ni “msafara” wa meli za kivita kwenda katika peninsula ya Korea.

Amri yake ya kuharibu mfumo wa mahandaki unaotumiwa na wapiganaji wa ISIS huko Afghanistan kwa kutumia “mama wa mabomu yote” – bomu ambalo halijawahi kutumiwa kabla – na kushambulia uwanja wa ndege wa serikali nchini Syria ilionekana kama onyo kwa Pyongyang.

Lakini, mashambulizi hayo yameibua maswali iwapo Rais huyo wa Marekani yupo tayari kuchukua hatua kama hizo dhidi ya Korea Kaskazini na kuhatarisha kuzuka kwa vita kamili.

Kanali David S. Maxwel, komando mstaafu katika jeshi la Marekani ambaye amewahi kufanya kazi Korea Kaskazini na Japan, alisema bomu lenye nguvu linalofahamika kama Massive Ordnance Penetrator (Mop) limeundwa kwa ajili ya maabara za chini ya ardhi za Korea Kaskazini.

“Kuna maeneo mengi duniani ambayo yameundwa chini sana ya ardhi na Mop liliundwa kwa ajili hiyo,” aliliambia gazeti la The Independent la Uingereza.

“Lakini inabidi wajiulize swali: Je, shambulizi la kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini haliwezi kusababisha majibu mabaya kutoka kwa nchi hiyo?”

Maxwell, ambaye sasa ni mkurugenzi katika Kitivo cha Masomo ya Ulinzi katika Chuo Kikuu cha Georgetown, alionya kuwa iwapo Korea Kaskazini itaona kwamba uhai wa serikali yake unahatarishwa, inaweza kutumia bomu la kinyuklia.

“Haina uwezo wa kushinda vita dhidi ya Marekani, lakini wanaweza kuamini kwamba huo ndio uchaguzi pekee walio nao,” aliongeza.

“Hata kama ni shambulizi kali dhidi ya mifumo ya makombora na uwezo wa kinyuklia, Korea Kaskazini inaweza kuhisi inabidi ijibu. Na huu ndiyo utata ambao wana mikakati na watunga sera wanakabiliana nayo.”

Komando huyo mwenye sifa ambaye amewahi kuwa mkuu wa sera katika Komandi ya Operesheni ya Korea katika jeshi la Marekani ameonya kwamba hata shambulizi moja la anga linaweza kuzua “jibu lenye madhara makubwa,” ambalo litahitaji kuondolewa kwa watu katika sehemu kubwa ya nchi ya Korea Kusini na kupelekwa kwa majeshi ya Marekani kwa ajili ya maandalizi ya vita ya ardhini.

Dokta John Nilsson-Write, mtafiti mwandamizi wa masuala ya Asia wa Chatham House, anaamini kuwa uwezekano wa kuingia kijeshi wa Marekani ni “mdogo sana.”

“Hatari ya kuzua vita ya kawaida au baya zaidi yenye upotevu mkubwa wa maisha huko Korea Kusini inapinga matumizi ya njia hiyo,” aliliambia gazeti la The Independent.

“Washington haiwezi kuhatarisha kuziudhi Korea Kusini na Japan, na Trump mwenyewe anaonekana kuwa anapenda zaidi kutumia vitisho ambavyo havieleweki zaidi ya kutumia vita halisi.”

Trump alipunguza ukali wiki iliyopita, kwa kuiitaka China “mkombozi wa kiuchumi wa Korea Kaskazini” baada ya kuzungumzia suala hilo na Rais Xi Jinping.

Maandiko yake kwa njia ya Twitter yamekuja baada ya vyanzo ndani ya wizara ya ulinzi nchini humo kuwaeleza waandishi wa habari kwamba Marekani haikuwa ikifikiria kufanya shambulizi la kijeshi, huku Mike Pence akisisitiza kwamba suluhisho la amani bado linawezekana.

“Bado tunaamini kwamba, kama washirika wetu katika ukanda huo na China wanaweza kuweka shinikizo la kutosha, kuna nafasi kwamba tunaweza kufikia malengo yetu ya muda mrefu wa peninsula ya Korea isiyokuwa na silaha za kinyuklia kwa njia za amani,” Makamu wa Rais alisema wiki iliyopita.

Tunatiwa moyo na hatua ambazo zimechukuliwa na China hadi sasa.”

Meli za kivita za Marekani zikiongozwa na USS Carl Pence anasisitiza kwamba meli ambazo zinaongozwa na USS Carl Vinson, ambazo zilikuwa zinashiriki katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi na jeshi la wanamaji la Australia, zitawasili katika bahari karibu na peninsula ya Korea ndani ya siku chache zijazo.”

Kama yale mashambulizi ya Syria na Afghanistan, hatua hiyo inaweza “kuimarisha msimamo wa Korea Kaskazini” kuongeza uwezo wake wa kijeshi, Maxwell alionya.

Alisema mtu asiyeeleweka ni Kim mwenyewe, ambaye ametumia ukatili kwa kuondoa wapinzani miongoni mwa wandani wa utawala wake katika miaka sita aliyokuwa madarakani, na kuongeza kwamba “Hakuna taasisi yoyote ya kijasusi ulimwenguni ambayo inaweza kusema kwa hakika hatua gani atachukua.”

Korea Kusini imekuwa katika hali ya tahadhari kutokana na uwezekano wa kufanyika kwa majaribio mengine ya silaha wakati maadhimisho ya miaka 85 ya Jeshi la Watu wa Korea yakikaribia wiki hii, huku idadi kubwa ya silaha zikiwa katika pande zote za mpaka.

Joseph Yun, mwakilishi maalumu wa sera ya Korea Kaskazini wa Marekani atakuwa Tokyo kwa ajili ya mkutano na wawakilishi wa Japan na Korea Kusini.

Siku za nyuma Korea Kaskazini imewahi kurusha makombora au kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia kwenye maadhimisho fulani ya kitaifa.

Dokta Nilsson-Wright alisema kwamba wakati kumekuwa na wito kwa Marekani kuharibu silaha za maangamizi za Korea Kaskazini, ni vigumu kufahamu kwa uhakika zilipo silaha hizo na pia zimewekwa katika maeneo ambayo ni magumu kuharibiwa.

Aliongeza kwamba njia pekee ambayo Marekani inaweza kutumia ili kumaliza mgogoro huo ni kuongeza shinikizo kwa kushirikiana na washirika wake na utayari wa kufanya mazungumzo.

Mashinikizo yanaweza kuhusisha vikwazo vya kiuchumi kutoka kwa China, ili nchi hiyo ikubali kuacha majaribio ya silaha na kufanya mazungumzo ambayo atahusisha mataifa yaliyo katika eneo hilo.

Maxwell anakubali, kwa kusema kwamba japokuwa Serikali ya Kim imekuwa inaweza kupata upenyo katika mfumo wa kimataifa wa mabenki, lakini vikwazo vya kifedha bado vina nguvu.

Aliitaka Marekani kupunguza sintofahamu na hali ya wasiwasi wa kukataa kujibu kila majaribio ya makombora na mienendo ya kijeshi kwa maneno makali.

“Kim anafanya kazi kama gaidi na kitu kimoja ambacho magaidi wanataka ni utundu,” aliongeza Maxwell.

Badala yake dunia inapaswa kuelekeza nguvu zake dhidi ya rekodi mbaya ya haki za binadamu ya Korea Kaskazini.

“Tunapozungumzia haki za binadamu, inaondoa uhalali wa utawala,” Maxwell alisema. “Kuna thamani ya kimaadili na kimkakati kuwaambia watu wa Korea Kaskazini kwamba tunafahamu kwamba wanateseka.”

Raia mwema
 
Kwanza MOAB waliyoishushia afhghanistan impact yake wala haitishi miti bado imesimama hata mapango hayaja athirika,kwa ujumla ule mkwara wa mother of all bombs ni aibu tupu,hata hiyo(Mop) ni bure tu tu hizo maabara za korea kaskazini zimejengwa deep chini ya milima labda watumie thermal nuclear.
 
Back
Top Bottom