SHERRIF ARPAIO
JF-Expert Member
- Aug 25, 2010
- 9,539
- 5,904
Kwa muda mrefu ndondi esp. za heavy weight division zimekosa ule utamu wa boxers wa miaka ya akina enzi za watu kama akina Mike Tyson, Evander holyfield, Lennox Lewis, John Ruiz, Larry Holmes, Riddick Bowie etc.
Kwa muda mrefu watu tumekuwa tukitegemea hili pambano kati ya hawa dogo wawili, yule mfilipino Pacquiao na huyu mmarekani Floyd Maywether Jr.ambao wamekuwa wakitambiana kila kukicha kutokana na boxing records zinazovutia sana.
Maywether Jr. hajapigwa hata pambano moja. Pacman ameweka record ya kuwa bingwa wa pound for pound kwa uzito wa aina mbalimbali na speed ya punches zake sio ya kawaida inatisha.
I can't wait kwa hawa jamaa wakizipiga kwani imesemwa kuwa itakuwa is one of the mega fights of the century. Kuna wanaosema Mayweather anamwogopa mfilipino. I hope watamaliza ubishi sooner than later
``Record ya kuwa bingwa wa pound for pound`` !...Pacman ameweka record ya kuwa bingwa wa pound for pound kwa uzito wa aina mbalimbali
UFC ndio nachotizama sikuhizi mie kuna Mbrazil Silva jamaa anachapa kama Bruce Lee.
Kuna Dogo anaitwa Amir Khan ni mkali ila naye bado sijamuona kuzichapa na watu kama Floyd ndio tutajuwa ukali wake. Pacman na Floyd waache kutafutiana sababu wazipige.. .
Mkuu hapa naona tunafananisha dagaa na Sangara..., huyu dogo baada ya kushinda Gold Medal Olympic wamekuwa wakimpambanisha na vilaza ili kwanza atengeneze Jina..., kumuweka kwenye kundi la kina Floyd nadhani ni mapema sana.... tumpe muda...
Anderson Silva si binadamu yule.
Ila Silva bado hajashindwa kabisa. Kuna moja alishindwa kwa disqualification dhidi ya Yushin Okami lakini kalipiza Jumamosi kwa kumpa kisago cha ukweli.
Kile Kichapo kweli ni cha hatari nilijuwa atamuachia asimame tena alafu naona wameamuwa kuifanyia Brazil wa Brazil kwa UFC wanatisha sasa hivi kuliko football.
Angalia pacman/marquez....halafu angalia mayweater/marquez.Mpaka sasa mpambano wao haujawa confirmed na nakumbuka pacman alisema angetaraji kustaafu october 2011 si unajua kwa sasa pia ni mbunge nchini kwake!.
Kwa kifupi Folyd anamuogopa Manny mana kile kichapo alichopewa Cotto kilikuwa fundisho kwake..Pacman yupo juu