Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 19,472
- 25,403
Ni ukweli usiopingika kwamba Marcos Rene Maidana au Chino kama anavyojulikana na mashabiki wake ndiye bondia pekee aliyempa misuko suko ya kutosha unbeaten man Floyd Mayweather kiasi kwamba ilibaki kidogo ampige Mayweather kwa knockout kwenye lile pambano lao la kwanza kwenye zile round nne za mwanzo sema tu alishindwa mwenyewe kumalizia round zilizo baki na kumfanya apoteze pambano.
Floyd mwenyewe akakiri kwa kinywa chake kwamba tangu aanze kucheza ngumi kuanzia zile za ridhaa mpaka za kulipwa hajawahi kuruhusu idadi kubwa ya ngumi kama alizopigwa na Maidana hivyo basi ingawaje alishinda pambano hilo lakini floyd akaomba tena rematch na huyo bwana mdogo lakini bado floyd aliendelea kupata ushindi kiduchu sana.
Ingawaje pambano la Floyd Maywether na Manny Pacquiao lilibatizwa kama pambano la karne lakini bado halikuweza kufua dafu ukilinganisha na lile la maidana.
Sifa kuu ya Marcos Maidana ni kwamba ni bondia asiye kata tamaa hata kidogo hata umpigaje ,na hilo lilidhihirika haswa kwenye pambano la Maidana na Amir Khan .
Katika lile pambano Maidana round za mwanzo alichezea kichapo na almanusura atolewe kwa K.O haswa pale aliposukumiwa konde la mbavu ambalo lilimuangusha chini na kuagulia kwa sekunde kadhaa kabla ya kuamka na kuendelea na pambano, na alipoamka ,aliamka kwa kasi ya ajabu kwani Amir Khan alikuwa anachezea makonde ya kutosha sema kilichomuokoa ni round za mchezo zilikuwa zimeshaisha ila bila hivyo Amir alikuwa anakiona cha mtema kuni.
Na sifa kuu inayomtambulisha Maidana ni uwezo wake wa kurusha makonde mengi yenye kasi na shabaha ya ajabu vile vile kutokata tamaa mapema hata umpigaje kwani huwa anabadilisha matokeo muda wowote ule .
Sifa hizi pia anazo Manny Pacquao , Manny Pacq anasifa ya kurusha makonde mengi ya haraka harakaa mpaka yakabatizwa jina la cherehani.
Hivyo basi kwa wale wapenzi wa masumbwi bila shaka watakuwa na hamu kubwa sana ya kuona wawili hawa wakipambanishwa ili kujua mkali zaidi nani kwa maana asilimia kubwa kama sio wote wakali wa masumbwi ambao wamepigana na floyd wamepigana pia na Manny Pacquaioa kasoro huyu bwana mdogo.
Natumai mapromota watafika muafaka na watakaa mezani ili kuwaandalia vijana hawa pambano ili wakate kiu ya muda mrefu ya mashabiki