Manjonjo ya Dr Kimei wa CRDB!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Ameendesha misa ya shukrani kwa Mungu baada ya CRDB kupata faida kubwa. Amealika wafanyakazi wa benki ya crdb toka nchi nzima kuja dar es salaaam kuhudhuria sherehe na misa ya leo, nauli na gharama za kukaa dar ni juu ya benki. Zaidi ya yote, kuanzia mwezi januari mwakani kila mfanyakazi atakuwa akipata 'bonus' ya sh 120,000/= kila mwezi.

Haka kanchi ni katamu sana ukikapatia!
 
Crdb! Waliuza hisa nyingine this year to raise their operating capital....haya bwana ponda mali kufa kwaja
 
hiyo faida wanayopata wawakumbuke wateja,watupe mikopo ya riba nafuu.

Hahahaaaaa! Kalagabaho mkuu. jaribu kukumbuka ile kanuni ilotamkwa na Yesu kwa biblia kwamba........kila aliyenacho ataongezewa na asiye na kitu hata kile kidogo alicho nacho at..........................! malizia
 
Ameendesha misa ya shukrani kwa Mungu baada ya CRDB kupata faida kubwa. Amealika wafanyakazi wa benki ya crdb toka nchi nzima kuja dar es salaaam kuhudhuria sherehe na misa ya leo, nauli na gharama za kukaa dar ni juu ya benki. Zaidi ya yote, kuanzia mwezi januari mwakani kila mfanyakazi atakuwa akipata 'bonus' ya sh 120,000/= kila mwezi.

Haka kanchi ni katamu sana ukikapatia!
lazima wale faida;
nakumbuka siku zile hawa CRDB ukiweka pesa kwa account ya mtu nawe huna account nao lazima wakulipishe. we do not have a robust and active regulatory auhtority for Tanzanian banking industry.BOT are observers and not regulators as one would think/expect!!!!!!!!
 
Na haka kajamaa lazima huko mbeleni tuje tukahoji kuhusu issue ya EPA, asidhani tumesahau jinsi CRDB ilivyoshiriki katika kufanikisha dili la EPA. Watanganyika bado hatujamalizana nae huyu.
 
Hii nchi inahitaji lawsuit mindset. Mtu awapige benki na Kimei lawsuit kwa discrimination na kuingiza dini kazini.

Mtu akisema Kimei anapendelea wafanyakazi wa dini yake atakataa?

Kama huyu ndiye CEO wa benki mimi siwezi kuwekeza katika benki yake.

hajalazimishwa mtu kuhudhuria misa au ulitaka achangie mahakama ya kadhi ndo uone hana udini? Mbowe mdini juzi kachangisha pesa za mskiti au vipi? Tatizo lako unapima kila kitu kwa kioo cha dini yako, utajilipua bure
 
Sawa hajalazimishwa mtu kuhudhuria.

Lakini kwa nini anatumia fedha za benki, benki isiyo na dini, benki yenye wateja wa dini zote na wengine wasio na dini, benki ya umma katika nchi isiyofuata dini yoyote, kufanikisha misa ya dini moja?

Wafanyakazi wa dini nyingine wakisema wamebaguliwa kwa sababu hawajafanya yao atakubali kwamba kawabagua?

Tunaoamini kwamba kutumia fedha za shirika la umma katika shughuli za kidini tukisema amekosea atakataa?
 
Wewe achana na fikra za kijinga hizo,nani kakwambia crdb ni mali ( benki ) ya umma? Kama wewe ni mfanyakazi na unaona ujatendewa haki basi mwaga wino. Upo hapo?
:hat:
 
Acha mawazo ya kidini ndugu yangu, ukifikiria hivo basi unataka hata Rais, waziri, na wengineo wanapoenda ktk mikusanyiko ya dini wasitumie magari ya serikali bali watumie magari binafsi, achana na huo mtazamo sio mzuri. mbona makamu wa rais hutumia magari ya serikali kwa ajili ya kwenda msikitini jioni na ijumaa?
mbona hufikirii gharama anayoitoa huyu ndg Kimei kwa ajili ya kusafirisha hao wafanyakazi bali wewe umeng'anania misa tu? nafikiri toka hapo ulipo and start thinking positively. huoni gharama zinazotumiwa na CRDB kwenye family day kulipia vinywaji vyenye kilivi wewe umeona misa tu? acha hivo ndugu yangu........................
 
hajalazimishwa mtu kuhudhuria misa au ulitaka achangie mahakama ya kadhi ndo uone hana udini? Mbowe mdini juzi kachangisha pesa za mskiti au vipi? Tatizo lako unapima kila kitu kwa kioo cha dini yako, utajilipua bure

Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho! changia hoja, nachojua sio kila mfanyakazi CRDB ni mkristio! ambacho angefanya nikumshukuru mungu kwa kuita viongozi wote wa dini na kuomba au kushukuru!!

Siku nyingine think!
 
Kama anafanya hivyo ni safi,pili afanye pia ibada na msikitini awaalike waislamu wafanyakazi nao wapate neema,wadau haujalazimishwa kwenda crdb kwahyo kulalamika sio vizuri kuna bank ya makabwela unaweza enda huko
 
Wewe achana na fikra za kijinga hizo,nani kakwambia crdb ni mali ( benki ) ya umma? Kama wewe ni mfanyakazi na unaona ujatendewa haki basi mwaga wino. Upo hapo?
:hat:
CRDB ni benki ya umma kabisa, Kiranga yuko sahihi.!
Au unataka kusema UMMA ni SERIKALI KUU?...
Hah ha h hah
 
Hakika kabisa ishu ya kusoma misa kanisani kwaajili ya taasisi ya watu mchanganyiko (kama benki) ni kituko cha aina yake, unless kama mleta mada amekosea au kuchanganya jambo hili, labda pia aliitwa shehe ili asome dwaa kukidhi upande wa pili wa dini!
 
Back
Top Bottom