Manjonjo ya Dr Kimei wa CRDB!

Ndyoko, habari hii umeitoa wapi? Kwa namna ilivyokuwa, je ni sherehe ya kidini(shukrani) au ni sherehe ya kupongezana zaidi na hilo la misa (naamini ameomba kimei kama individual na sio crdb- i stand to be corrected!) labda ni by the way tu kwa sababu wahudhuriaji kwenye sherehe hiyo ya 'kupongezana' walikuwa dar?

Sioni katika hali ya kawaida ni vipi plc kama crdb inaweza kutumia fedha zake kwa ajili ya 'misa ya shukrani'. Hata auditors kwa auditors tu hili haliwrzi kupita kama lilivyo! Utafanya jambo jema kama utaweka/utatafuta maelezo zaidi katika habari hii.

SMU,

Hata mimi nafikiri kama wewe. Haiingii akilini CEO wa PLC atumie fedha za benki kwa shughuli ya kikanisa.

Hapa kuna possibilities mbili.

1. Kuna smear campaign na habari hizi hazina ukweli.
2. Bongo imeoza kiasi kwamba mambo ya kweli yakianikwa yanaonekana kama smear campaign.

I hope it is the first one, because if it is the second one, tupo pabaya kuliko nilivyofikiri.
 
Jamani naombeni msaada hapohapo hivi CRDB ni mali ya umma au?

Umeona post hii? Umeelewa maana yake?

https://www.jamiiforums.com/busines...njonjo-ya-dr-kimei-wa-crdb-2.html#post2999733 ?

Umetembelea CRDB Bank PLC ?

Unafahamu maana ya PLC katika "CRDB Bank PLC"? Kama hufahamu maana yake ni "Public Limited Company" maana yake kampuni iliyo offer shares zake kwa umma na inaendeshwa kwa mchango wa fedha za washikadau wake walio katika umma na kwa hiyo inawajibika kwa washikadau wake katika umma.
 
SMU,

Hata mimi nafikiri kama wewe. Haiingii akilini CEO wa PLC atumie fedha za benki kwa shughuli ya kikanisa.

Hapa kuna possibilities mbili.

1. Kuna smear campaign na habari hizi hazina ukweli.
2. Bongo imeoza kiasi kwamba mambo ya kweli yakianikwa yanaonekana kama smear campaign.

I hope it is the first one, because if it is the second one, tupo pabaya kuliko nilivyofikiri.
Hili la misa ya shukrani sijapata kulisikia hata kwa kampuni ndogo ambazo wamiliki ndio hao hao waendeshaji! Nina mashaka hata Mkombozi Bank (plc?) kama wameshawahi kufanya misa ya namna hii. Well, ngoja tusubiri..yawezekana ni 'maendeleo' katika corporate governance!
 
Sawa hajalazimishwa mtu kuhudhuria.

Lakini kwa nini anatumia fedha za benki, benki isiyo na dini, benki yenye wateja wa dini zote na wengine wasio na dini, benki ya umma katika nchi isiyofuata dini yoyote, kufanikisha misa ya dini moja?

Wafanyakazi wa dini nyingine wakisema wamebaguliwa kwa sababu hawajafanya yao atakubali kwamba kawabagua?

Tunaoamini kwamba kutumia fedha za shirika la umma katika shughuli za kidini tukisema amekosea atakataa?

Kufuatana na sheria za mabenki yote, CEO hawezi kujiamulia yeye mwenyewe kutumia fedha kwa njia yeyote ile bila kupata idhini ya bodi yake! Yote mnayosema kuwa Kimei wa CRDB ameyafanya kama ni kweli basi bodi yake imeidhinisha ama sivyo kama bodi ya CRDB haikiudhinisha matumizi hayo ,anaweza kuchukuliwa disciplinary action.
 
Hata kama bodi imeidhinisha, bodi pia inawajibika kwa washikadau na wajasirimali wa CRDB.

Huwezi kuniambia mie muislam au mtu nisiye na dini kwamba hela yangu niliyonunulia hisa za CRDB na hivyo ikatumika kufanikisha biashara zake, leo imetumika kufanyia misa ya kikristo.

Huwezi kuniambia mie ninayeamini mizimu hilo hilo.

Huwezi kuniambia mie atheist hilo hilo.

Hata kama Kimei kapata idhini ya bodi na rais.

Kimei na bodi wote wanawajibika kwa shareholders.

My thing is, habari hizi zina ukweli au ni kupakaziana tu?
 
fanyeni utafiti kabla ya kubwabwaja hapa....Acheni kudanganyana ile ilikuwa ni misa ya kimei kwenda kumshukuru Mungu kwa mafanikio ambayo bank imepata yeye kama CEO kwake ni kama furaha na jambo la kushukuru,then akaamua kualika wafanyakazi wa karibu atakaependa kumuunga mkono aende kujiunga nae...haukuwa lazima na hakuna alielipiwa chochote.
ni sawa na mtu anaeenda kushukuru Mungu kwa kitu chochote then akaomba rafikize wamsindikize
 
Wewe ndio mbumbumbu wa mwisho! changia hoja, nachojua sio kila mfanyakazi CRDB ni mkristio! ambacho angefanya nikumshukuru mungu kwa kuita viongozi wote wa dini na kuomba au kushukuru!!

Siku nyingine think!

Tatizo lako na wengine wote wenye mitazamo kama ya kwako ni tabia yenu ya ushindani wa kitoto, unajua watoto wana tabia ya kulilia kila anachopewa mtoto mwenzake.
Mkuu wa benki ni mkiristo ameamua kwenda kanisani kuhurudhisha mafanikio ya kazi yake kwa Mungu wake na kutoa shukrani, sasa wewe unataka eti amshirikishe na mungu mwingine nje na imani yake. Mkuu wa bank hakuwa mchoyo badala ya kwenda peke yake kutoa shukrani na kujizolea mibaraka lukuki peke yake yeye amewapa nafasi wafanyakazi wengine pia, wale waliojisikia huru kuandamana nae.
Unajua mwisho wa mwaka makampuni mengi hufanya sherehe za kumaliza mwaka, ukubwa wa sherehe unategemea na uwezo wa kampuni, hapa CRDB wameweza kukutanisha wafanyakazi wao wa kutoka maeneo mbalimbali jambo ambalo ni jema kwa kampuni. Kwenda kanisani ni suala binafsi la mkuu wa benki na wale wafanyakazi walioafiki kumuunga mkono, hili ni tukio moja tu kati ya matukio mengi na mbwembwe zao za kusherekea mwisho wa mwaka.
Mwandishi hapa ama kwa maslahi yake binafsi au kwa kutokuelewa anataka atuamishe kuwa sherehe nzima ilikuwa ni misa kanisani tu.

Hakuna ubaya kwa viongozi kwenda kuabudu hata rais wa nchi pia anahudhuria nyumba za ibada huku akiwa madarakani huku akijua kabisa kuwa yeye ni rais wa watu wa dini zote na wasio na dini pia. Tena apokwenda kuabudu anasindikizwa na kulindwa na vyombo vya dola, kwa nini hatulalamikii utumiaji wa raslimali za serkali na rais anapokwenda kuabudu mskitini au kanisani? kwa nini asiite viongozi wa dini zote na kuomba au kushukuru huko huko ikulu?
 
Jk alipopata urais 2006 alifanya maulid pale bagamoyo, wenye matumbo tukakamua pilau lililoandaliwa kwa hela ya ikulu.

La Kimei sio jipya
 
hiyo faida wanayopata wawakumbuke wateja,watupe mikopo ya riba nafuu.

hili nalo neno!!!! hivi Kimei ni Economist or just the same like all others??

maana sioni sababu za kufanya yote haya while wateja hatupati mikopo na riba bado ni juu mno!!!!! wake up KIMEI
 
Mzee kimei yupo smart sana, hapa kuna wapuuzi wachache wanataka kumchafua tu! Ni mchapakazi mzuri...personally I do admire him. Ni mzee ambaye anajua jinsi ya kuwa inspire wafanyakazi wake. Na ndio maana employee resignation rate ni ndogo sana CRDB compared na hizi benki nyingine kubwakubwa.
 
Zamani hapa JF, ulikuwa ukipost chochote kinachohitaji ushahidi ilikuwa ni lazima ulizwe uuweke hadharani kabla great thinker hawajachangia. Leo hii hapa pamejaa, kila kimoja kinapita tu.

Ni kweli kulikuwa na misa
Ni kweli aliyeomba misa ni Dk Kimei
Ni kweli watu walikaribishwa kumsindikiza.

Lakini SI KWELI
Misa ilikuwa ya Mkurugenzi wa CRDB kwa mamlaka yake.
Si kweli kuwa wafanyakazi walilipiwa chochote kwenda kwenye hiyo misa.
Haikutumika hata cent moja ya shareholders kwenye hiyo ibada.

Kwa wakristo ni jambo la kawaida kumshukuru mungu kila unapopiga hatua moja kwenda nyingine na kwenye kushukuru unaweza kabisa kuwashirikisha waliokaribu nawe. Kwa mafanikio ya benk ambayo anaiongoza yeye anaweza pia kufanya misa ya shukrani kama mtu binafsi na watu wa karibu kwake kuwashirikisha ni wafanyakazi wenzake. nasisitiza "wafanyakazi wenzake" na marafiki zake.

Hoja hii ilikuwa na dhamira isiyo thabiti na ilikuwa inahitaji ushahidi kwenye mambo yafuatayo:
Kwamba benk iliwalipia wafanyakazi kutoka mikoani kuhudhuri?
Kwamba Kuna fedha za shareholders zilitumika?
Kwamba katika hiyo ib ada hakuna Waisilamu, wapagani, wakatoliki, waanglican na wengineo waliohudhuria?

Respect.
 
Sifurahishwi na aina ya watu wanaopost ndani ya JF. Siyo kwamba siwapendi hapana , sifurahishwi na post zao.
 
Tatizo lako na wengine wote wenye mitazamo kama ya kwako ni tabia yenu ya ushindani wa kitoto, unajua watoto wana tabia ya kulilia kila anachopewa mtoto mwenzake.
Mkuu wa benki ni mkiristo ameamua kwenda kanisani kuhurudhisha mafanikio ya kazi yake kwa Mungu wake na kutoa shukrani, sasa wewe unataka eti amshirikishe na mungu mwingine nje na imani yake. Mkuu wa bank hakuwa mchoyo badala ya kwenda peke yake kutoa shukrani na kujizolea mibaraka lukuki peke yake yeye amewapa nafasi wafanyakazi wengine pia, wale waliojisikia huru kuandamana nae.
Unajua mwisho wa mwaka makampuni mengi hufanya sherehe za kumaliza mwaka, ukubwa wa sherehe unategemea na uwezo wa kampuni, hapa CRDB wameweza kukutanisha wafanyakazi wao wa kutoka maeneo mbalimbali jambo ambalo ni jema kwa kampuni. Kwenda kanisani ni suala binafsi la mkuu wa benki na wale wafanyakazi walioafiki kumuunga mkono, hili ni tukio moja tu kati ya matukio mengi na mbwembwe zao za kusherekea mwisho wa mwaka.
Mwandishi hapa ama kwa maslahi yake binafsi au kwa kutokuelewa anataka atuamishe kuwa sherehe nzima ilikuwa ni misa kanisani tu.

Hakuna ubaya kwa viongozi kwenda kuabudu hata rais wa nchi pia anahudhuria nyumba za ibada huku akiwa madarakani huku akijua kabisa kuwa yeye ni rais wa watu wa dini zote na wasio na dini pia. Tena apokwenda kuabudu anasindikizwa na kulindwa na vyombo vya dola, kwa nini hatulalamikii utumiaji wa raslimali za serkali na rais anapokwenda kuabudu mskitini au kanisani? kwa nini asiite viongozi wa dini zote na kuomba au kushukuru huko huko ikulu?

Kijana wengine atukurupuki soma ulichochangia chini hapa:

hajalazimishwa mtu kuhudhuria misa au ulitaka achangie mahakama ya kadhi ndo uone hana udini? Mbowe mdini juzi kachangisha pesa za mskiti au vipi? Tatizo lako unapima kila kitu kwa kioo cha dini yako, utajilipua bure

Kama ungekua na fact ambayo umeisema hapo juu usi ngetegemea kupata mchango wangu hapo juu!

Kukuweka tu sawa mtoa mada hakuhusisha mahakama ya kadhi wala uislam, nchii ina watu wa imani nyingi, na wengine kama sisi tunaimani za ki mira na kukumbusha tu twaweza kua wadau au ni wadau wakubwa wa hiyo CRDB au shareholder na atutambuliki based on our believes.

Siku nyingine narudia tena think and think sio kuandika tu ilimladi!
 
Mod tafadhali funga hii mada, wachangiaji wengi ni waropokaji. Hakuna facts ku support hii posts....imejaa umbea na kuchafuana tu!
Tafadhali PAW au Invisible tumieni mamlaka tuliwapa ili kulinda status ya JF. Si watu wanakurupuka kutoka ulevini kutaka kuchafua watu wenye heshima zao kama mzee Kimei.
 
Back
Top Bottom