Manji kumkataa Wakili Kibatala 'kwa sababu za kisiasa', ametishwa na nani?

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
201
1,534
Nimestaajabu sana kusikia Manji amekataa Wakili Msomi Peter Kibatala kusimamia kesi yake na kumtetea mahakamani. Kwanza vyombo vingi vya habari vimepotosha habari hii. Vimeripoti kama vile Kibatala ndo alikua anaenda kuanza kumtetea Manji leo then Manji akakataa. Lakini ukweli ni kwamba Kibatala amekuwa Wakili wa Manji tangu alipokamatwa.

Tangu kesi ya Manji ilipoanza, mtetezi wake mahakamani ni Kibatala. Nyaraka zote za Manji kuhusu kesi yake zimekuwa zikitumwa kwa Kibatala. Mwenendo wa kesi ambaye amekua akiulizwa ni Kibatala. Hata DPP anawasiliana na Kibatala kuhusu kesi ya Manji.

Kwahiyo si kweli kwamba Manji amemkataa Kibatala kuwa Wakili wake, maana tayari alikua wakili wake. Huwezi kumkataa mama yako wakati tayari ameshakuzaa. Alichofanya Manji ni kuomba Kibatala asiendelee tena kuwa Wakili wake. Hii ni haki yake kisheria. Muda wowote mtuhumiwa anaruhusiwa kubadilisha Wakili kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo.

Lakini je Manji amefanya haya kwa ridhaa yake?Kwanini akatae kuwakilishwa na Kibatala leo? Maswali ya kujiuliza Manji kukataa kuwakilishwa na Kibatala;

1. Kiapo katika maombi yaliyowasilishwa Manji mwenyewe Mahakama Kuu na kupangiwa Judge Arufani kilisainiwa na Manji mwenyewe. Je; mpaka anaweka saini hakufahamu nani kaandika Kiapo hicho ambacho kina mahali panapoonesha kwamba Wakili aliyeshuhudia kiapo hicho alitambulishwa kwake na Wakili Kibatala?

2. Hati ya Dharula iliyoambatana na maombo ya dhamana ya Manji iliapwa na Wakili Kibatala; je Manji hakuona hati hiyo iliyo juu kabisa ya Hati ya Maombi?

3. Hati nzima ya Maombi ya Dhamana inaonesha wazi imeandaliwa na Wakili Kibatala. Ina maana Manji hakufahamu nani kaandaa Maombi yale?

4. Maombi ya Dhamana ya Manji yalipotajwa kwa mara ya kwanza hapo tarehe 28 July 2017 mbele ya Judge Arufani Wakili aliyezungumza kwa niaba ya Manji ni Kibatala. Je Manji hakufahamu mpaka muda ule iwapo Kibatala ndiye Wakili? Mpaka upande wa DPP wanaomba muda wa kuwasilisha kiapo kinzani, ni Wakili Kibatala aliyeomba muda uwe mfupi ikizingatiwa uharaka wa maombi husika. Je, Manji hakuwepo Mahakamani?

5. Nyaraka zote za majibu ya DPP zilielekezwa kwa Wakili Kibatala, je hii ilikuwa kwa bahati mbaya na Manji hakufahamu?

6. Ni lini na kwa namna gani Manji aliwasiliana na Wakili Kibatala na kumueleza yeye asingependa kuwakilishwa naye katika maombi ya dhamana aliyoyaanda Wakili Kibatala.

7. Manji anasema sababu za kisiasa ndo zimemfanya ashindwe kuendelea na kibatala. Lakini je, Manji amejua leo kuwa yeye na Kibatala wana itikadi tofauti za kisiasa? Wakati Manji anskubali (at first place) Kibatala awe Wakili wake hakujua Kibatala ni CHADEMA na yeye ni CCM? Au ndo amejua leo? And by the way utofauti wa kisiasa kati yake na Kibatala ungeathiri vipi mwenendo wa kesi?

Ni vizuri Manji akaeleza ukweli wa kilimchomfanya ghafla akatae kuwakilishwa na Wakili Kibatala badala ya kutoa sababu ambazo haziendani hata na records za Mahakamani, na hasa ikizingatiwa records hizo ni wazi kwa umma Public records).

Malisa GJ
 
Pengine ameshauriwa kua kumtumia Kibatala na kulingana na kesi yake inaleta picha ya kisiasa mno.
Na hapo hapo kuna mawakili walimsimamia mteja kesi haijafika mbali mteja akahama chama, itakua ameihofia hii picha.
 
Pengine ameshauriwa kua kumtumia Kibatala na kulingana na kesi yake inaleta picha ya kisiasa mno.
Na hapo hapo kuna mawakili walimsimamia mteja kesi haijafika mbali mteja akahama chama, itakua ameihofia hii picha.

This is a brilliant analysis...which could make some sense. Wengine sababu wanamuamini wakili wao msomi wanataka kila kesi aichukue yeye. Haiwezekani.
 
Ametishwa na Muhimili wa pili,ule uliojichimbia kuliko mihimili yote
Muhimili uliojipa mamlaka ya kusimamia "Check and Balance" na "Rule of Law"

Ule muhimili ulimuagiza mkuu wa muhimili mmoja,kuwashughulikia wengine ndani na wenyewe unawasubilia nje.Muhimili wenye mizizi mikuu,ulioagiza hakimu ahamishwe kituo cha kazi ndani ya mwezi mmoja.

Lazima uwe ni muhimili wenye nguvu,maana huko kwa Manji mwenye muhimili wake amekaimishwa tu,ili awe anafuata kama channel ya luninga inavyoitikia amri ya remote
 
Jamaniii.. mnataka kumwekea Manji maneno mdomoni?

Manji kasema wazi wazi kuwa Yeye ni CCM ( tena Diwani ) hajisikii vema kutetewa na Wakili ambae ni CHADEMA.. na katamka wazi wazi..
Sasa nyie mnaanza speculation za ajabu, kilicho wazi ni kuwa Manji kaamua hataki kutetewa na wakili wa Chadema, full stop..
Kwani si ni yeye alimwomba Kibatala amwakilishe huku akifahamu kuwa Kibatala ni Chadema? Wakati ule alijisikia vema?
 
Manji doesn't owe anyone any explanation on why he decided to get rid of his attorney.

It's his right to do what he did. Period, end of sentence.

Quit reading too much into it otherwise y'all will come across as salty and butthurt for getting dumped.

There's nothing unusual with what he did.
 
Back
Top Bottom