Manji awapa moyo Yanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manji awapa moyo Yanga

Discussion in 'Sports' started by Gudboy, Sep 15, 2009.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  mdhamini mkuu wa Young Sports Club ya jijini dsm amekutana na wachezaji wa timu hiyo ili kuelezwa ni kwanini wameanza vibaya kwenye mashindano yanayoendelea hivi karibuni.

  Manji alikutana na wachezaji hao alipowaalika kula nao chakula katika hotel ya Kilimanjaro jiji dsm. Je yanga mtafanikiwa kufanya vyema katika mechi zinazoendelea ili kuwapa moyo mashabiki wenu.

  habari hii ni kutokana na magazeti ya leo
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,018
  Likes Received: 23,936
  Trophy Points: 280
  Mpira hauchezwi hotelini mkuu. Akutane nao asikutane nao, mwaka huu ni Simba 4 Yanga 1.
   
 3. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  ni kweli lakini mipango si unajua tena vijana lazima wapewe moyo, sasa utaona mambo yake lazima wautete tu ubingwa bwanaa
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ameahidi kutoa pesa ya kununulia mechi pamoja na kamati za 'UFUNDI'? au anategemea ushindi ujilete hivihiv tu?
   
 5. Chimo

  Chimo JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 31, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 60
  mbona mnapenda kuingilia Mambo ya Daaaaaar es Salaam Young Africa Wao Kimyaaaaaaaaa Kama hawaaoni mnavyokurupuka hovyooooooooooo
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Yanga kama hawatanunua mechi kweli msimu huu ianaweza kushuka daraja, mimi nahudhuria mechi zote za ligi kuu, pale Taifa, kwa ile soka a yanga hakika inatia kinyaa....
  manji anapenda sana kulabwa miguu, ameona wamekwama ndo0 sasa anatoa msaada
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  wamekata rufaa wanataka tunyanganywe pointi 6.....daah soka la bongo kazi kweli kweli watu hawachezi mpira uwanjani wanataka za mezani, kashaona mziki wa simba ni mnene, wanataka tupokwe pointi sita ili watuvurugi akili lakini mwaka huu hatukubali kunyangwa pointi kirahisi...
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  anataka simba anyanganywe pointi sita halafu anunue mechi ya mtibwa..teh teh
   
 9. O

  Omumura JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mchezo walioucheza mwaka jana tumeshaushtukia safari hii, wamezoea kuhonga marefa na wachezaji wa timu pinzani, mwaka huu wasahau.wamejidai kusajili wachezaji wa nje 11 halafu wote wanapigwa benchi, to hell with them!
   
 10. s

  smp143 Member

  #10
  Sep 16, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Yanga mwaka huu hakuna kitu..wamezoea kutumia pesa kushinda kila mechi..Manji kashakubali mwaka Simba kali na hata JKT,Mtibwa na Azam zitawachapa tuu, ndio maana kaamua kuokoa jahazi..Tumeshawastukia pamoja na hizo hela za kuhonga hawatpata njia rahisi..Wameshapeleka hela pale TFF et Simab wanyanganywe pointi 6 na wanataka Patric Phiri afungiwe mechi tatu kwa sababu aliingia uwanjani kule mbeya kumlaumu refa wakati kila moja alishaona rafu mbaya aliyochezewa Mrwanda and refa kamezea...
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  Date::10/13/2009
  Mrithi wa Kondic atua Yanga asema anaijua Simba tangu Serbia


  Kocha mpya wa Yanga, Kostadin 'Kosta' Papic, baada ya kutua Dar amedai kuwa anaifahamu Simba toka akiwa kwao Serbia.


  Na Frank Sanga
  KOCHA mpya wa Yanga, Kostadin 'Kosta' Papic ametua nchini na juzi usiku alitarajia kuingia mkataba akisema kwamba anajua vema kuwa kuna mechi baina ya timu yake dhidi ya Simba, Oktoba 31.
  Papic, mzoefu wa soka ya Afrika ambaye alitembelea makao makuu ya klabu jana alisema hakuna mechi rahisi duaniani kwani kila mchezo katika ligi ni ngumu hivyo anaamini katika ligi kuu bara kila mechi kwake itakuwa ngumu.
  "Ninajua Jumamosi tunakutana na Azam na Oktoba 31 tutacheza na Simba, mechi zote hizo kwangu ni ngumu, ukweli hakuna mechi rahisi , mimi nitaanza maandalizi ya uhakika katika mechi zote na si Simba tu."
  "Kama kocha kabla hujaenda sehemu unayotaka kwenda kufundisha, lazima ujue mazingira ya huko, na kabla sijafikaTanzania ninajua kuwa kuna timu pinzani nitakutana nazo, naijua Simba tangu nikiwa Serbia na najua mfumo wa ligi ya hapa, hivyo hainipi shida," alisema.
  Jana usiku, kocha huyo alitarajia kukutana na mfadhili wa klabu hiyo, Yusuph Manji na kusaini mkataba na ilitarajiwa kuwa kocha anayemaliza muda wake, Dusan Kondic angemkabidhi kila kitu.
  "Kesho (leo) nitaangalia mazoezi ya timu hii asubuhi na jioni ili niweze kumjua kila mchezaji yukoje na nijue nitaanzia wapi.
  "Lakini, nitaanza kibarua katika mechi na Azam na sitarajii kurejea Serbia hivi sasa hadi pale msimu wa Ligi Kuu utakapomalizika, kwani wakati nakuja huku nilikuwa najua lazima nisaini mkataba," alisema.
  Papic, ambaye amewahi kufundisha Enyimba ya Nigeria na Hearts of Oak ya Ghana, zote za Afrika Magharibi kwa muda tofauti anasifika kwa kuinoa timu kucheza kwa pasi fupi, lakini ni kocha asiyependa majina makubwa katika kikosi chake.
  Kocha huyo, maarufu 'Bill Clinton' kutokana na kufanana wajihi na rais wa zamani wa Marekani, wiki iliyopita alikuwa Afrika Kusini kufanya mazungumzo na timu za Moroka Swallows na Mamelodi Sundowns, lakini hawakufikia muafaka na sasa imebaki kumalizana na Yanga.
  Kimaisha, alizaliwa Juni 17, 1960 mjini Novi Sad, Serbia na hutumia mfumo wa 4:4:2. Alitimuliwa na Hearts of Oak ya Ghana Juni 20, mwaka huu.
  Timu nyingine ambazo amewahi kufundisha akiwa Afrika Kusini ni Maritzburg United aliyoifundisha kwa miezi sita na Kaizer Chiefs.
  Alipohamia Nigeria, kocha huyo alifundisha timu nne zikiwamo Lobi Stars, Enyimba, Enugu Rangers na Kwara United kabla ya kuhamia Hearts of Oak ya Ghana alikotimuliwa Juni 20.
  Iwapo atasaini mkataba na Yanga, Kosta atakuwa akilipwa mshahara wa dola 5,000 (shilingi milioni sita) kwa mwezi na kuishi makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam.
  Mtangulizi wake, Kondic alikuwa analipwa dola 10,000 (sh milioni 12) kwa mwezi na muda mwingi aliishi katika hoteli ya New Africa ambako kila siku alikuwa akitumia zaidi ya Sh. 250, 000.
  Kondic na msaidizi wake, Spaso Solokovisk wanamaliza mkataba wao mwezi ujao, lakini Manji hana mpango wa kuendelea nao na kuna habari kuwa hii itakuwa ni wiki ya mwisho kwa makocha hao.


  Source: Gazeti la Mwananchi
   
Loading...