Nijuavyo mimi, ukikopa na kushindwa kulipa, sio kosa la jinai la kumpeleka mtu jela!, ni kosa la madai ambapo ukiisha filisiwa kwa mali kupigwa mnada that is the end!.Sakata mali za John Komba kupigwa mnada kufuatia deni la Tsh bilion 1.2 analodaiwa na benki la CRDB limefikia tamati baada ya mfanyabiashara nguli na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Bw Yusuf Manji, kununua shule zake pamoja na baadhi ya mali zake ambazo zilikuwe zipigwe mnada.
Komba alikuwa anakabiliwa na uwezekano wa shule na mali zake kupigwa mnada (na kufungwa jela) ili kufidia deni hilo alilokopa CRDB miaka 5 iliyopita.
Source: Mwananchi.
MAONI YANGU
Komba amshukuru sana Manji kwa kumuokoa kwenda jela na mali zake kupigwa mnada. Sipati picha kama Komba angefungwa jela kile kitambi chake angekificha wapi. Lazima kingenywea kama puto lililotoboka. Hivi alidhani kuendesha shule ni lelemama au ni sawa na kuimba kwaya na kusimamia bendi? Chezea madeni wewe!
No sidhani kama zimeondoka!, kilichofanyika ni bail out tuu, kwa Manji kumlipia deni ili mali zisiuzwe na benki, out of that bail out, inawezekana Komba akaachia baadhi ya mali hizo preferably land kuifidia hiyo bail, out!.Daaaaaaaaa Vitega uchumi vya komba ndio vinaondoka hivyo.
Nijuavyo mimi, ukikopa na kushindwa kulipa, sio kosa la jinai la kumpeleka mtu jela!, ni kosa la madai ambapo ukiisha filisiwa kwa mali kupigwa mnada that is the end!.
Hakuna hukumu ya kifungo cha jela kwa kudaiwa!.
Pasco
No sidhani kama zimeondoka!, kilichofanyika ni bail out tuu, kwa Manji kumlipia deni ili mali zisiuzwe na benki, out of that bail out, inawezekana Komba akaachia baadhi ya mali hizo preferably land kuifidia hiyo bail, out!.
Pasco.
Sii kweli!.nijuavyo mimi ni kwamba ikiwa thamani ya mali zako ni ndogo kuliko deni, utasweka ndani sawia.