Manji akumbwa na balaa

watu wanauziana nchi wenyewe kwa wenyewe.zabuni zote wanapewa matapeli ambao ndio wadhamini wa chama chao kazi hipo.

kwahio jinsi hela inavyozunguka nina haki kusema kwamba serikali ya ccm inatumia hela ya walipa kodi kudhamini chama chao.

hii sio maisha bora kwa kila mtanzania tena imekuwa "maisha bora kwa kila rafiki wa ccm".
 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, inatarajia kumfikisha mahakamani mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa(CCM), Yusuph Manji,
kwa kukabidhidhi matela ya kubebea takataka yaliyo chini ya kiwango.
Nia hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Manispaa hiyo na Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo,
Alisema Manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (Septemba – Desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi Novemba mwaka huu.
Aidha, alisema halmashauri katika mkataba wake na Manji, ilitaka matela yenye matairi manane, lakini mfanyabiashara huyo aliwapelekea matela yenye matairi manne.
alieleza.
Alisisitiza kuwa, kamati yake na halmashauri haikuwa tayari kupokea matela hayo na kumshauri Manji kutimiza kile walichokubaliana katika mkataba husika.
Alisema hivi sasa kuna mbinu chafu na ushawishi unaofanywa na mfanyabiashara huyo kwa baadhi ya madiwani ili wakubali kuyapokea matela hayo.
Alibainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilitoa siku saba kwa Manji kuyaondoa katika eneo yalipowekwa matela hayo na kuleta yale yanayokidhi viwango.Chanzo Tanzania Daima.[/QUOTE]



Kwa nnavyowajua wasiasa wa kibongo sidhani kama kweli watampeleka mheshimiwa huyu! Pia kwa jinsi
manji alivyo mzito duh sidhan..... hata hayo yaliyochini ya kiwango yatapokelewa ama sivyo hakuna kitakachoendelea Manji sijui analindwa na nani..... mmmh?
haka ka-manispaa katalimydu jitu hili??? hawa ndiyo walioishika nchi wanafanya watakavyo Jamaaniiiiiiiii!
Ngoja tuone kitakachotokea
 
hivi sasa kuna mbinu chafu na ushawishi unaofanywa na mfanyabiashara huyo kwa baadhi ya madiwani ili wakubali kuyapokea matela hayo.

ndugu yangu, basi kaa utambue kwamba hizo mbinu chafu hazitaishia kwa hao madiwa tu!! kuna ma-advocate maarufu kwa hayo madudu, mahakimu, waendesha mashtaka na wanasheria wa serikali!!! Tena uchaguzi mwakani ndio kabisaaaa

hebu tusubiri
 
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, inatarajia kumfikisha mahakamani mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Manji, kwa kukabidhidhi matela ya kubebea takataka yaliyo chini ya kiwango.
Nia hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Manispaa hiyo na Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo, ambaye alibainisha kuwa, halmashauri hiyo ilimpatia zabuni ya kuagiza matela mfanyabiashara huyo, lakini ameshindwa kulinda makubaliano ya mkataba.
Alisema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Manji hana nia ya kupeleka matela yenye viwango vinavyohitajika au kurejesha kiasi cha shilingi milioni 324 alichopewa kwa ajili ya kazi hiyo.
Bujugo alisema matela 27 yalikusudiwa kusambazwa katika kata zote za wilaya hiyo ili kuiweka manispaa hiyo katika hali ya usafi.
Alisema Manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (Septemba – Desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi Novemba mwaka huu.
“Zabuni hiyo ilikuwa ni ya kipindi cha miezi mitatu, lakini Manji alikiuka utaratibu huo ambapo imepita zaidi ya mwaka ndiyo anatuletea matela hayo yasiyo na ubora,” alifafanua Bujugo.
Aidha, alisema halmashauri katika mkataba wake na Manji, ilitaka matela yenye matairi manane, lakini mfanyabiashara huyo aliwapelekea matela yenye matairi manne.
“Sisi tuna ushahidi wa kile tulichokiagiza katika makubaliano yetu. Tulihitaji kuletewa matela yenye matairi manane, amechukua muda mrefu anatuletea matela ya matairi manne, hatuyataki,” alieleza.
Alisisitiza kuwa, kamati yake na halmashauri haikuwa tayari kupokea matela hayo na kumshauri Manji kutimiza kile walichokubaliana katika mkataba husika.
Alisema hivi sasa kuna mbinu chafu na ushawishi unaofanywa na mfanyabiashara huyo kwa baadhi ya madiwani ili wakubali kuyapokea matela hayo.
Alibainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilitoa siku saba kwa Manji kuyaondoa katika eneo yalipowekwa matela hayo na kuleta yale yanayokidhi viwango.
Alidai kwamba pamoja na agizo hilo, mfanyabiashara huyo alishindwa kutimiza masharti aliyopewa, jambo lilioifanya manispaa kufikiria kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha jambo hilo linamalizika.
Tanzania Daima Jumatano lilijaribu kumtafuta Manji ili kuzungumzia sakata hilo, lakini simu yake ya mkononi ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake.
Msaidizi huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Manji hakuwepo ofisini huku akilitaka gazeti limuachie maagizo ili akirudi ampe.
“Ninaomba uniachie ujumbe nitamfikishia na kama atakuwa tayari najua lazima atakupigia,” alieleza msaidizi huyo.
Hata hivyo, msaidizi huyo alishindwa kutimiza ahadi hiyo ambapo hadi Tanzania Daima Jumatano linakwenda mtamboni, hakuna simu yoyote iliyopigwa na Manji.



Chanzo Tanzania Daima.

Tungeazima sheria za China za kunyonga wahujumu uchumi kwa miezi sita uchumi wa Tanzania ungepaa.Tatizo la nchi yetu tunawabembeleza kina J Patel,Manjis,Rostam,Chenge,Lowassa na mafisadi wote wanaendelea kutamba uraiani badala ya kukaa keko.

Tanzania inahitaji kiongozi aliyetayari kuchukuwa maamuzi makubwa,kiongozi tuliyenaye sasa bado anafikiri rushwa si tatizo kubwa.
 
Kwenye hili usiseme mkuu. Mashabiki wa Yanga hawaoni wala kusikia lolote kuhusu Manji. Ziwe ni pesa za wizi au dhuluma mradi ni pesa. It is a pity! Vichwa vyetu wadanganyika inabidi vifanyiwe uchunguzi.

Nchi za wenzetu waliotutangulia Club kubwa kama Yanga wangesha waomba watanzania msamaha lakini siunajua tena vile vizee visivyokuwa na kazi wanavyomshabikia Manjis.Mwaka huu mwanzoni walitaka kumtoa macho Mzee Mengi kwa kumsakama mfadhili wao mkuu.
 
tatizo hapa ni CCM bila kuondoa mdudu anayeitwa CCM bado mambo hayata enda.
 
Back
Top Bottom