Usishangae ya barabara tu. Kila jambo la serikali linashangaza. Neno dharura au emergency halimo kabisa katika kamusi ya serikali. Muda mrefu sasa nawaza ivo kweli hawa watu haya hawayaoni au ndo dharau tu. Almuradi maisha yanakwenda. Angalia umuhimu wa traffic lights, hasa baada ya magari kuzidi kama yalivyo sasa. Ni kitu gani kinachosababisha taa isiwake. Labda bulb imeunguwa au waya zimechomoka. Serikali ndio ishindwe kweli. Kabla ya uhuru barabara nyingi kama si zote za Gerezani, Kariako Upanga na kwengineko zilikuwa na lami kamili. Imepotea hivi hivi wananchi wakilalamika na serikali ikifedheheka. Labda kabla tu ya uchaguzi ujao mambo yatakuwa mazuri. Vuta subra , sema Insha- Allah.