Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 5
Kwa wakazi wa Dar es Salaam na hususani wale wanaoitumia barabara ya Uhuru watakubaliana nami kuwa hiyo ni moja kati ya barabara mbaya sana Tanzania.Awali eneo lililokuwa baya lilikuwa kati ya amana hospitali na bungoni.Angalau kwa sasa mahadhaki yamepunguzwa japo kwa vifusi na kuchimbwa kwa greda.
Tatizo jingine kwenye barabara hii lipo kati ya buguruni malapa na sheli (Kobil Petrol station).Kwa muda mrefu eneo hilo limekuwa na mashimo madogomadogo njiani.Wiki tatu zilizopita manispaa husika ilituma watenda kazi wakiwa na mashine ndogongogo wakaanza kukata lami kwenye maeneo yaliyokuwa na mashimo.Hivi sasa ni wiki tatu zimepita tangu wakate lami kwa ajili ya kuziba mashimo lakini hakuna kilichofanyika.
Hivi sasa kama unaendesha ni afadhali usipite njia hiyo na kama upo kwenye daladala utaionea huruma gari la mwenzio.Ni mashimo makubwa yameachwa tena ni mabaya kwa usalama wa magari kwa kuwa walipokata yamekuwa makubwa na yana kingo zinazoharibu gari mara tairi linapoingia.
Madereva wanaotumia njia hiyo wanakwenda mwendo wa zig zag kukwepa mashimo yanayokwepeka japo ni kazi ngumu.
Najiuliza inakuwaje manispaa wakate lami kabla ya kujiandaa kuziba mashimo?HIvi kweli tunaowatendaji walio makini kwenye manispaa zetu? Ni utovu mkubwa wa nidhamu na udhaifu wa watendaji wetu pale wanapofanya jambo kwa kukurupuka pasipo kujipanga.
Sijui kama ni kila mtu analiona hili kuwa kero? au tushajichokea mwaego?