Manispaa yampa muda Spika kubomoa uzio | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manispaa yampa muda Spika kubomoa uzio

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lilombe, Jun 2, 2011.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda


  SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ametakiwa kubomoa uzio aliouweka kuziba barabara inayounganisha eneo la Kijitonyama na Sinza, Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ujenzi wa nyumba yake katika Kiwanja namba 630, Kitalu 47 eneo la Kijitonyama.

  Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Gaudence Nyamwihula alisema jana kwamba Spika Makinda amepewa kibali cha muda kufunga barabara hiyo ili awe katika nafasi nzuri ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba yake hiyo na si vinginevyo.

  "Kibali alichopewa (Makinda) ni kama kile kinachoweza kutolewa kwa mtu mwingine yeyote iwe kuna shughuli ya msiba, ngoma au ujenzi kama inavyotokea katika maeneo mengine," alisema.

  Kaimu Mkurugenzi huyo alisema Spika Makinda hana ruhusa ya kujenga katika barabara aliyoweka uzio na kwamba kufanya hivyo ni kosa kisheria.

  Alisema tofauti na madai ya wakazi wa eneo hilo kuwa spika huyo amejenga katika barabara ili kujiongezea kiwanja, Ofisi ya Manispaa ya Kinondoni inamini kuwa jambo hilo haliwezi kutokea na kwamba Makinda ataheshimu taratibu zilizopo.

  "Hivi sasa barabara imefungwa kwa muda na ujenzi ukimalizika itafunguliwa na kutumika kama awali," alisema na kuongeza kuwa hakumbuki hasa kwamba spika amepewa kibali cha muda gani, lakini akasistiza kuwa kibali alichonacho ni cha muda ili kupisha ujenzi.

  Nyamwihula alisema hakuna mtu aliye na mamlaka ya kufunga barabara moja kwa moja kwa ajili ya matumizi yake, na kwamba ili hilo litokee ni lazima wakubaliane katika ngazi ya mtaa.

  Diwani wa Kata ya Kijitonyama, Ulole Juma Athuman alipoulizwa jana kuhusiana na kauli hiyo alisema anahitaji barua kutoka manispaa inayoeleza pamoja na mambo mengine, muda ambao barabara hiyo itakuwa imefungwa.

  Alisema ujenzi wa ghorofa hilo ulianza miaka mitatu iliyopita na kwamba hadi sasa haujakamilika. Alisema tangu ulipoanza, hapakuwa na uzio na kuelezea kushangazwa kwake kuona ukiwekwa sasa na kufunga barabara... “Jambo baya zaidi ni kwamba hata taratibu hazikufuatwa.”

  Ulole alisema kama manispaa isipoainisha muda wa kibali hicho, barabara hiyo inaweza kufungwa maisha kwa kisingizio cha kupisha ujenzi akisisitiza kuwa anahitaji kujua yote hayo ili aweze kuyawasilisha katika mkutano na wakazi wa eneo hilo utakaofanyika Jumapili katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kijitonyama.

  “Mosi taratibu zimekiukwa kwa Spika Makinda kuziruka mamlaka za mtaa na kata na kwenda kuomba kibali manispaa. Pili, nataka wanieleze itafungwa kwa muda gani kwani ujenzi wa ghorofa hilo una mwaka wa tatu sasa na haujakamilika,” alisema na kuongeza kuwa wananchi katika mkutano huo ndiyo watakaokuwa na uamuzi na siyo yeye.

  Alisema mkutano huo ambao umeahirishwa mara mbili kutoa nafasi kwa manispaa kutoa uamuzi, sasa utafanyika Jumapili na maandalizi yake yameanza ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo kwa wakazi wa kata hiyo.

  Sakata la Spika huyo kuifunga barabara hiyo liliibuka baada ya kubandika kibao kinachoonyesha kuwa imefungwa katika kona unapoanzia Mtaa wa Sahara, mwendo wa dakika takriban tano kwa mguu hadi kufika nyumbani kwake.

  Mwenyekiti wa Mtaa wa Kijitonyama, Philip Komanya alidai kwamba hakuwa na taarifa za kufungwa kwa barabara hiyo akisema huenda wahusika walimzunguka na kwenda manispaa badala ya kupitia kwake.
  Alisema kwamba awali, kulikuwa na maombi ya kutaka kuifunga kwa sababu zilizoelezwa na waombaji kuwa ni za kiusalama jambo ambalo hata hivyo, lilikataliwa katika ngazi ya kata.

  Kauli hiyo ya Komanya ilithibitishwa na Msemaji wa Spika, Herman Berege ambaye alikaririwa akisema kwamba bosi wake alikuwa na vibali vyote vya kumruhusu kuifunga barabara hiyo isitumiwe tena na wapita njia na watu wengine na kwa sababu za kiusalama na kwamba hayo yamefanyika kwa baraka zote za Manispaa ya Kinondoni.

  Hata hivyo, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ilifuatilia sababu hizo za kiusalama na kubaini kwamba hazikuwapo. Mkuu wa wilaya hiyo, Jordan Rugimbana alisema kuwa ofisi yake iliangalia kama pengine kulikuwa na agizo lolote kutoka ngazi za juu lakini akabaini kuwa hakuna kitu kama hicho hivyo suala hilo akaliacha manispaa.

  Awali, Komanya aliwataka walioifunga barabara hiyo kuachana na fikra hizo na badala yake kuwashauri kuweka lango la kuingilia na kutokea na mlinzi kwa ajili ya kuhakiki wanaopita na pia muda wa kuitumia, pendekezo ambalo hata hivyo, hawakuliafiki.

  Taarifa ya kufungwa kwa muda kwa barabara hiyo imekuja baada ya awali, Mhandisi wa Manispaa hiyo, Urio Athanas kusema kwamba manispaa haishughuliki na barabara za vichochoroni kama hiyo akisema ufungaji wa aina hiyo una taratibu zake za kufuata kuanzia ngazi ya mtaa hadi kata.

  Source: Gazeti la Mwananchi, Juni 2, 2011
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,330
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kamanda diwani ulole mkikutana j'pili ushauri wangu ni kuanzisha task force maalum ya kumfumgulia kesi spika kwa kuvunja utaratibu wa kufunga barabara kwani haiwezekani kila mtu akifanya ujenzi wa nyumbayake basi afunge barabara it does not make sense at all. Viongozi wa manispaa majibu yanaonyesha wazi kuwa wanamwogopa spika na wako tayari kuvunja utaratibu ili wamlinde spika this is wrong. Viongozi wote wa mtaa akiwemo m-kiti wa mtaa na mbunge wa kinondoni huu ndio wakati wa ku test leadership zao lazima wachague moja kupigania wapiga kura au kupigania maslahi ya spika na inaelekea viongozi wa manispaa tayari wameshachagua kuwatosa wapiga kura wao na kumtetea spika kwahiyo tunataka kila kiongozi atoe msimamo wake wazi ili ieleweke wazi.
   
 3. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wewee Mama, chonde chonde, kama ubabe wako uliotumwa na mafisadi ni kwa wabunge, sasa nadhani unachomoza kidole mpaka kwa wananchi. Unapotea njia, huku watu wamechoka ujue hilo, watu hawaogopi chochote siku hizi kwani hawana cha kupoteza. Soma alama za nyakati, angalia wenzako kinachowakuta, utakuja kudhalilika bure. Kwanza nikueleze ukweli tu, yani huku uraiani hakuna anaekupenda, kifupi unachukiwa vibaya mno. Nadhani hao wachache wanaokuonyesha tabasamu na kukuunga mkono wanatetea vibarua vyao kutokana na mfumo wenyewe wa ajira hapa tz, wanajua wakisimamia ukweli unaweza kuwaharibia msivyokuwa na hiruma nyinyi. Hivo jiulize, na huyo wa mbele yako kabla ya kufika kwako akianza kujenga na yeye akifunga barabara wewe utafika vipi kwako? Unasema sababu za kiusalama wakati hujahamia, usalama huo wa kivipi? Tatizo lako we mama ni mbabe, sasa hapa bongo watu umewakuta, usijitie unajua sana utafundishwa mji uje kulalamika
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  SPIKA MAKINDA KUISHI KWENYE NYUMBA YAKE HUKO SINZA

  Baada ya kuishi hotel kwa muda mrefu spika wa bunge la jamuhuri, Ndugu Anne Makinda
  sasa anaishi kwenye nyumba yake binafsi huko sinza kuepusha matumizi mabaya ya serikali,
  hili kwamba pesa hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo
  Spika alikuwa miongoni mwa viongozi wa serikali ya Kikwete waliojazana kwenye mahotel ya jiji la Dar-es-salaamu baada ya kukosa nyumba za serikali kutoka na zile walizopaswa kutumia kushikiliwa na viongozi waliopita kwa kuuzwa kwao na serikali iliyopita.
  Hii ni moja ya matumizi makubwa ya serikali ya Kikwete na kuipa kisogo miradi ya maendeleo, hawa viongozi wangeweza kuishi kwenye nyumba zao binafsi na kuwekewa ulinzi wa polisi na hapo tungeokoa pesa nyingi sana,
  kwa kuishi hapo hotelini ilikuwa pia inalighalimu taifa chakula cha hao viongozi wakiwa hapo hotelini, kutona na mazingira ya hoteli nyingi vyakula vinauvya kwa bei kubwa na ulinzi wa vyumba vya hao viongozi hapo hotelini.
   
 5. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jamani kama kuna mtu mwenye panga na rungu hapo aniazime please!! nimechka na kurembaremba ishu zinazoweza kumalizwa in a minute, mi naenda mwenyewe kuifungua hiyo barabara, nimechoka na ngonjera za mafisadi!
   
 6. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  siamini kama makinda hana nyumba hadi leo, siamini kama kujenga nyumba ni lazma ufunge mtaa, kwani magorofa ya k.koo yanajengwa vipi na mitaa hafungwi? Na ni nyumba gani ya makazi ijengwe zaidi ya miaka mitatu? Labda ya mlala hoi, huyo alikuwa na mpango wango wa kuiba eneo la barabara hilo amewahiwa ndio anatoa sababu za kipuuzi
   
 7. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,106
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mama hodari wakuvunja kuta yuko wapi????Au hapo maji mazito.
   
 8. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 23,130
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  wenzio wana magobole shauriloooo
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 23,130
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  wenzio wana magobole shauriloooo!
   
 10. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Mwanzoni sana hakuna hata kiongozi mmoja alithibitisha Makinda kupewa kibali. Ghafla leo inaonekana kuna kibali lakini mwisho wake haujulikani. Hapa kuna uchakachuaji. Ningekuwa kinaonekana, bila shaka tarehe zingekuwa za nyuma sana na hakioneshi ukomo, hivo inawezekana miaka 5 ijayo bado ujenzi utakuwa unaendelea!!

  Ukuta kwa ajili ya usalama kikomo chake ni kipimo cha uwanja, sio mita kadhaa kuelekea kwenye kiwanja. Viongozi wetu, katika hili Makinda, hawana fikra kwa atu wengine. Umimi ni mwingi sana!!! Mkutano uendelee na ukuta ubomolewe. Ni matendo ya raia tu ndio yatawafundisha hawa viongozi. Wakawaulize Ben Ali, Mubarak na wengineo!!
   
 11. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ningekuepo jirani yake ningesubiri akihamia nami nikaombe kibali niifunge bara bara....tuone akija na hiyo gari yake atapita wapi?
  Nawapongeza sana wananchi wa hayo maeneo...na huyo kiongozi wa mtaa wao...atasingiziwa kua si raia!....
   
 12. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu diwani bila shaka atakua si wakujivua magamba!.
   
 13. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 23,130
  Likes Received: 10,456
  Trophy Points: 280
  hahahaaa nyumba yaweza kupigwa x akaambiwa haipo kwenye mipangomiji
   
Loading...