Manispaa yaingilia sakata la kifo cha mzazi Ukonga

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeunda timu maalum kuchunguza chanzo cha kifo cha Sabela Mganga(31) aliyefariki katika zahanati ya CHO ya Ukonga Mazizini baada ya kujifungua watoto mapacha na kuzuiliwakwenda hospitali ya wilaya kutokana na deni li
Marehemu Sabela alizuiliwa kutoka katika zahanati hiyo kwenda kupata matibabu katika hospitali ya Amana kutokana na kudaiwa kiasi cha shilingi 155,800 kama gharama za kujifungua.

Marehemu alipelekwa katika zahanati hiyo tangu Februari 5 hadi 7 na kujifungua watoto mapacha na mara baada ya kujifungua watoto hapo aligundulika kuwa aliishiwa damu na daktari kutaka mama huyo apelekwe amana kwa matibabu zaidi.

Hivyo timu hiyo maalum imeundwa chini ya Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala na baadae ripoti hiyo kupelekwa kwa mkurugenzi na kutolewa rasmi.

Taarifa kutoka dnani ya familia hiyo inasema watoto hao mapacha wanaendela vizuri na mazishi ya mwanamke huyo yanatarajiwa kuwa kesho mkoani Dodoma.
 
Back
Top Bottom