Manispaa ya Kinondoni yabomoa nyumba zilizojengwa kiholela

Watz hawaeleweki kabisa, serikali ikisimamia sheria mnalalamika, ikifumba macho mnalalamika, hivi mnataka nini hasa?

Kama watu waliishi hapo kinyume cha sheria, hakuna namna zaidi ya kuwaondoa. So tusilete siasa kwenye mambo ya msingi kama haya, kumbe hadi mahakama ilishaamuru watoke.

Binafsi sina tatizo na hili ila ninachotaka wasiishie hapo bali pia waingie Mbezi beach, Msasani kina Mengi wamejenga wameziba mto na hata mama Lwakatare nyumba yake ipo ndani ya mto na amejazie vifusi mvua ikinyesha maji hayana pa kwenda hali inayosababisha mafuriko!

Hivyo ni zoezi zuri tena sana tu lkn liwe endelevu na lenye kutenda haki
kwa mfano Mbezi beach hoteli ya giraffe, belinda, White sands zote hizi ziko ndani ya ufukwe ambapo sheria za nchi haziruhusu kujenga ndani ya mita 60 ktk ufukweni kwa hiyo kwa kuwa wamesema zoezi lipo W.Kinondoni na litafika Mbezi Beach basi nasubiri kuona Giraffe, belinda, White sands zikipigwa nyundo!
 
Nasubiri jengo la Tanesco Ubungo nalo lishuke,maana wanataarifa muda mrefu.
 
kumbe wangechagua mamvi jiji lingekuwa uswazi hata ukitaka kujenga katikati ya barabara poa tu

Huo ni mtazamo wako kaka, na ukae ukijua sio kila kitu ni siasa,

kwa taarifa yako kaka, nchi hii haijawahi kuongozwa na chama cha upinzani tangu tupate uhuru mpaka leo, sasa jiulize hizo nyumba zinazovunjwa leo zilijengwa lini?, utakuta zingine tangu enzi ya Mwalimu zipo tu sasa Lowassa anaingiaje kwenye hili la kuvunja nyumba?
 
Ikulu kakaa mtu wa kazi alafu nyie mnataka kuishi kwa kubebwa? Hapa kazi tu... safi sana na kila mmoja aubebe msalaba wake sasa.
 
Tokea lini uliona mvuvi akimpa samaki aliyekwisha kumvua tayari chambo.Unapewa chambo ukiwa majini ukiishaingia chomboni unasubiri kukaangwa tu!!..#HapaKaziTu
 
muxar;
Msasani wapi?? Kule kwa wazee hafiki mtuuuu. Malofa na Wapumbavu ndo watakiona cha moto hadi wajue ccm ni ndumeee. Yaani we acha tu. Kilio hiki hata Mola hasikii tena, huku wanaendelea kuapishwa kulee mjengoni
Sioni unachofurahia, kwa hiyo machinga na bodaboda wa Mwenge wanamiliki majumba yanayobomolewa? lazima zitakuwa mbele dk 3.
 
Hizi nyumba zilizobomolewa mwenge zinazaidiy ya miaka arobaini na kama zilikuwa ni maeneo ya wazi je serekali ilikuwa wapi kwa muda huo wote au isije ikawa sababu ni hiyo hoteli inayojengwa hapo karibu ? Nadhani wakaazi wa hapo wanajua na shauri lao lilikuwepo mahakamani je limeshatolewa uamuzi ?
Vipi kituo cha mafuta cha BIG BON na jengo la ghorofa lililokaribu yake hapo sinza mori je si ni eneo la wazi hilo maana kwenye mchoro halimo je vitabomolewa ? na pia kituo cha mafuta cha TSN BAMAGA kipo ndani ya hifadhi ya barabara je kitabomolewa lini ?

Nawakilisha.............
 
Huyo mama kwenye you tube tuliishinaye hapo magorofa ya jeshi,mume wake alivostaafu akahamia hapo pembeni, hata hivyo mume wake alipalalaizi akafariki...mama ni bingwa wa kukaanga samaki huyo
 
Hayana uhusiano.
 
Huyo mama kwenye you tube tuliishinaye hapo magorofa ya jeshi,mume wake alivostaafu akahamia hapo pembeni, hata hivyo mume wake alipalalaizi akafariki...mama ni bingwa wa kukaanga samaki huyo
Sawasawa ni mkaanga samaki maarufu anaitwa mama Upendo au Mama Mwakasendile.
 
Back
Top Bottom