mnyawusi
Senior Member
- Apr 1, 2012
- 169
- 254
Tangu mwanzoni mwa mwezi Machi Manispaa ya Kinondoni iliwapa barua za uhamisho walimu wa shule za msingi ukiwa ni utaratibu wa kawaida unaolenga kuboresha utendaji wa walimu hao.Wengi wa walimu hao walihamishwa kutoka shule za mjini mfano Hananasif na kupelekwa nje ya mji mfano Bunju,Boko,Mbezi salasala na kwingine.Walimu hao walitakiwa kuripoti kwenye vituo vyao mapema na kuanza kazi na walifanya hivyo huku Manispaa ikiahidi kuwalipa stahiki zao ndani ya muda mfupi.Licha ya walimu hao kuripoti kwenye shule zao mpya hawajalipwa stahiki zao mpaka sasa pamoja na Rais Magufuli kuwaagiza waajiri kutowahamisha watumishi mpaka walipwe stahiki zao.Jambo hili limewasababishia usumbufu walimu na hata kuwavunja moyo na linaweza kuathiri juhudi za kuongeza ufaulu katika shule za umma.Manispaa ya Kinondoni walipeni walimu hao stahiki zao baada ya kuwahamisha kwani baadhi wamelazimika kuhama makazi wakiamini watalipwa stahiki zao kwa wakati hali inayowasababishia usumbufu mkubwa.