Manispaa ya Kibaha Yapandisha Gharama za Vibali vya Sherehe Kuanzia Agosti 6

Manispaa ya Kibaha Yapandisha Gharama za Vibali vya Sherehe Kuanzia Agosti 6

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Manispaa ya Kibaha imetangaza rasmi mabadiliko ya gharama za vibali kwa shughuli zote za sherehe na burudani zinazofanyika kwenye kumbi, ambapo kuanzia Agosti 6, 2025, wamiliki wa kumbi na waandaaji wa matukio watalazimika kulipia huduma mbalimbali kwa viwango vipya.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Afisa Michezo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha, gharama mpya ni pamoja na Tsh 50,000 kwa kibali cha sherehe na burudani, Tsh 30,000 kwa mshereheshaji (MC), Tsh 30,000 kwa mambouzi, Tsh 20,000 kwa muandaaji wa keki, Tsh 20,000 kwa mpiga picha (mnato na mjongeo), na Tsh 30,000 kwa mpishi wa chakula. Tangazo hilo limeeleza kuwa hatua hiyo ni kwa mujibu wa sheria za manispaa, na kwamba wateja wote watatakiwa kulipa gharama hizo mpya wanapokuja kuchukua vibali.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIBAHA

WAMILIKI WA KUMBI ZA BURUDANI,
MANISPAA YA KIBAHA.

YAH: TANGAZO LA MABADILIKO YA GHARAMA ZA
VIBALI VYA SHEREHE NA SHUGHULI ZIFANYIKAZO
UKUMBINI.

REJEENI MADA TAJWA.

  1. MKURUGENZI WA MANISPAA YA KIBAHA ANAWATANGAZIA KUWA, KUANZA AGOSTI 6, 2025 GHARAMA ZA SHUGHULI ZOTE ZIFANYIKAZO UKUMBINI ZITAKUWA KAMA IFUATAVYO:
a) KIBALI CHA SHEREHE NA BURUDANI TSHS. 50,000/=
b) MSHEREHESHAJI (MC) TSHS. 30,000/=
c) MAMBOUZI TSHS. 30,000/=
d) MUANDAAJI WA KEKI TSHS. 20,000/=
e) MPIGA PICHA (MNATO NA MJONGEO) TSHS. 20,000/=
f) MPISHI WA CHAKULA TSHS. 30,000/=

  1. HII NI KWA MUJIBU WA SHERIA ZA MANISPAA. HIVYO, TUWAJULISHE WATEJA WETU KUWA WANAPOKUJA KUCHUKUA KIBALI WATALAZIMIKA KULIPIA NA GHARAMA NYINGINE ZILIZOBAINISHWA HAPO JUU.
KNY: MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIBAHA

(Sahihi)
Burwan Thussub
AFISA MICHEZO
KNY. MKURUGENZI WA MANISPAA KIBAHA.

NAKALA: MKURUGENZI WA MANISPAA - (AIONE KWENYE JALADA)

P.o. box 30112, KIBAHA PWANI, phone +255 232402938, Fax +255 232402007
1 Halmashauri street 11 0812 Kibaha CBD, Email: tpd@kibahatc.go.tz, web:


vibali.jpg
 
Mnakaba hadi penati? Niandae keki ndogo ya birthday ya mwanangu halafu mnitoze hela kubwa hivyo? Basi siandai sherehe. Msivyo na haya mtataka kuchukua hela mpaka kwenye misiba maana huko nako kuna wapishi, mc, na wapiga picha. Angalieni msije mkakosa hata senti kidogo kama kwenye mabango ya mitaani
 
Back
Top Bottom