GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
Jana tarehe 03.02.2016 uongozi wa soko la feri ulizuia kulaza magari katika parking za magari za soko hilo. Kwa kawaida muda wa jioni kuanzia saa 12 ambapo watu wa Tanzania Parking Sytsem wanapo maliza muda wao wa kutoza ushuru wa parking za magari za eneo palikuwa panatumika kufanya huduma ya parking ya kulaza magari ambapo kwa kila gari lilikuwa likitozwa Tshs. 2,000/=. Eneo hili kwa wastani linauwezo wa kutoa huduma hiyo kwa magari zaidi ya 50, hivyo kwa siku moja lilikuwa likiingiza Tshs 100,000/=. Hivyo watu wengi walikuwa wanalaza magari yao kwa siku 6 ukiondoa siku ya Jumapili. Hivyo basi kwa mwezi huduma hutolewa kwa siku 26 (ukiondoa Jumapili 4). Mapato ya mwezi kwa hesabu za haraka haraka ni Tshs 2,600,000/= (i.e. Tshs 100,000/= x 26), na kwa mwaka ni Tshs 31,200,000/= (i.e Tshs 2,600,000/= x 12 ).
Kwa mapato ya Halmashauri haya makusanyo si madogo na ndio vyanzo vingine vya mapato. Hivyo kuacha kulitumia eneo hili kwa huduma hii ya kuegesha magari ni hasara kwa Halmashauri kwani kwa muda huu wa saa 12 jioni eneo hili huwa wazi na huwa halina kazi nyingine yoyote zaidi ya kulala waathirika wa dawa za kulevya (mateja) na paka. Ningeomba viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala waruhusu kuendelea huduma hii ya parking ya magari ikiwa ni chanzo kingine cha mapato. Tumeona sehemu nyingi ikifanyika hivyo mfano ofisi za CCM etc wamekuwa wakitoa huduma hii.