Manin'g nice yafungiwa leseni ya usafirishaji

Manin'g nice yafungiwa leseni ya usafirishaji

y-n

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
2,391
Reaction score
2,514
Sumatra imeifungia leseni ya usafirishaji kampuni ya mabasi ya Manin'g nice inayofanya kazi za usafirishaji kwa mikoa ya Mtwara na Lindi kuelekea Dsm.
Inasemekana chanzo ni ajali ya moja kati ya mabasi yao lililopata ajali Tarehe 19 mwezi huu mkoani Lindi.
Mwenye maelezo au ufafanuzi zaidi juu ya hili unaweza ukalifafanua zaidi.
Mnakaribishwa.
 
Attachments

  • 1395947001847.jpg
    1395947001847.jpg
    61.5 KB · Views: 560
As usual we are dealing with the simptoms. Wanamkomoa nani kama si abiria.
kama vilekuwakamata dada poa na kuwaacha majambazi.
kuwapiga mabomu CHADEMA waqt inchi imevaa kyupi.
Kuelekeza nguvu zote kwenye kampain chalinze waqt wanajua wataiba kura.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Sumatra na jeshi la polisi ni wapuuzi, waje mbeya waone ujinga wa madereva , makonda ,na wamiliki wa daladala , wanaenda petrol station na vidumu kununua Mafuta then yanakaa kwenye gari hadi yaliyopo kwenye tank yaishe ndio konda anachukua kidumu na kuweka kwenye tank, ipo siku watawachoma abiria wao kama mishkaki
 
Hiyo ni hatari sana #chalantai
Ifike hatua sasa Sumatra wachunguze kiundani na sio kukurupuka na kuzuia leseni kwa kampuni husika.
 
Duu kumbe maning walipata ajali? Mi naona kuwafunngia ni uonevu au ni njama za kibiashara maana jamaa alishaishika hii njia na mabus yake yapo order sana pia madreva wake wana lugha mzuri sana kwa abiria kuliko mabus ya kusini.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Duu kumbe maning walipata ajali?

Ajali yao ilihusisha na bodaboda ambayo nadhani mwendesha bodaboda na abiria wake walipoteza maisha.
Sijajua hasa nani au nini ni chanzo cha ajali yenyewe.
 
Yaani we acha tu. HOOD BUS tangu mwaka hhuu uanze limechinja mara ngapi ? Inaoneka wenye Hood wanajua kula na Kipofu sutra. Maning Ice mnakula peke yenu basi na msiba huu wa kufungiwa ni wenu peke yenu.
 
Sumatra iko kwa ajili ya kukusanya hela tu( dhulma) .hawan kaz wanayoifanya zaid ya faini na kufunga lesen
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Inasemekana chanzo ni ajali ya moja kati ya mabasi yao lililopata ajali Tarehe 19 mwezi huu mkoani Lindi.

Kwani hiyo ajali ilisababishwa na nini?? Na hapa ndipo ugomvi wangu na SUMATRA ulipo. Unakuta chanzo cha ajali ni Mwendo kasi wa Gari. Sasa unajiuliza wa kufungiwa ni Dereva na leseni yake au Kampuni ya Basi? Unless wadhibitishe kwamb Dereva alitumwa na Kampuni akimbize basi kwa kasi. Hata hivyo, naunga mkono ufunguaji leseni Kampuni za mabasi ambazo chanzo cha ajali zinatokana na Kampuni zenyewe, mfano kuweka gari bovu barabarani na kuajiri Madereva wasio na leseni.

Yangu ni hayo tu..
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Naona wanamwekea mazingira ya biashara mbunge wa Mtwara mjini kwani ndio mmiliki wa mabasi ya Machinga na mshindani wake ni Manning Nice na Hamanju.

Machinga ndio basi lenye watumishi wasio na elimu na wapuuzi kuliko wapiga debe wa kwa Azizi Ally. Na jeuri hii ni sbb mabasi yao hayakamatwi
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Daaah hapo kuna kaujanja kamefanyika....huyu anashkwa mkono asiendelee kukimbia ili yule wamtakaye aendelee na mbio. Jaman rushwa italimalza hili taifa.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Sumatra iko kwa ajili ya kukusanya hela tu( dhulma) .hawan kaz wanayoifanya zaid ya faini na kufunga lesen

Wangeifungia na hii hapa.
Ally's.
 
Attachments

  • 1395984557547.jpg
    1395984557547.jpg
    58.3 KB · Views: 194
Sumatra imeifungia leseni ya usafirishaji kampuni ya mabasi ya Manin'g nice inayofanya kazi za usafirishaji kwa mikoa ya Mtwara na Lindi kuelekea Dsm.
Inasemekana chanzo ni ajali ya moja kati ya mabasi yao lililopata ajali Tarehe 19 mwezi huu mkoani Lindi.
Mwenye maelezo au ufafanuzi zaidi juu ya hili unaweza ukalifafanua zaidi.
Mnakaribishwa.

nchi hii kama sumatra watafata sheria basi kampun ya mabasi itakayobak barabarani labda iwe inamilikiwa na Mungu,maana SUMATRA wamekazania mabas yenye kusababisha ajali,lakin jaman mabas tunayotumia watanzania ni machafu(yapo mengi) kiujumla yamechoka sana,ila SUMATRA kama imeunda kufatilia ajali na NAULI TU,,,,,
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Naona wanamwekea mazingira ya biashara mbunge wa Mtwara mjini kwani ndio mmiliki wa mabasi ya Machinga na mshindani wake ni Manning Nice na Hamanju.

Machinga ndio basi lenye watumishi wasio na elimu na wapuuzi kuliko wapiga debe wa kwa Azizi Ally. Na jeuri hii ni sbb mabasi yao hayakamatwi

vitu kama hivi unavipata JF tu,hata kwenye bunge la katiba havipo
 
Huu ni uwonevu sana au kwasababu ni msambaa? Alafu isitoshe jamaa alijipanga hadi boda ya msumbiji dah!! Kwa hili bosi wa sumatra rudisha moyo wako tunajua ni shinikizo na kama unataka kufanya kazi fanya kazi siyo kwa njia ya mtwara tu, kunanjia ya mwanza,arusha ,mombasa,dodoma, iringa,mbeya na bukoba mabasi kila kukicha yanapata ajali tena kuna makampuni ya mabasi yana ongoza kwa ajali au mbona boti azifungiwi. Achani usisiem wenu.
 
Hapa kuna njama za kiaina za kuididimiza hii kampuni. Kuna basi miezi kama miwili iliuwa watu zaidi ya kumi njia hiyo hiyo ya Dar - Lindi lakini haikufungiwa.
 
kama kweli imefungiwa, basi ni hujuma za kibiashara. maning nice amemwaga gari mtwara, masasi na nachingwea na kwa sasa wapinzani wake wanajikongoja kwa mbali sana
 
Huyo atakuwa Murji tu si bure yote hii ili mabasi yake ya Machinga yauze. Hivi kuna mabasi yanayoenda kazi Tanzania hii kushinda Ally's kuna Mabasi yanayoongoza kwa ajali kushinda Mohamed Trans, abood mbona lilichinja sana lakini halikufungiwa
 
Back
Top Bottom