Mangwea - Ghetto Langu (Lyrics)

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Hii ni nyingine tena,
Ni Bongo Records tena,
P Funk

KIITIKIO
Ni gheto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linaloniweka kwenye chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo,

Ni gheto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linaloniweka kwenye chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo

VERSE 1:

Ngoja nianze na hili la East Zoo,
Ukilicheki kwa nje liko simple tuu,
Ila ndani jirani kuna vitu flani,
Yaaani, mi mwenyewe sometimes nalitamani..
Kapeti manyoya stuli meza kioo,
Kitanda nane kwa kumi,
Marumaru mpaka kwenye choo,
Kimashine cha uzushi cha drycleaner,
Chumba cha Kati kuna studio ya kiaina,
Bafuni sink hakuna bali kuna jacuzzi,
Screen kila kona tunacheki tu movie,
Ungo decoder mwendo ni Dstv,
Zinga la Tv na deck ya DVD,
Bonge la mziki linatwanga tu CD,
Na hakuna feni full time ni AC,
Na hili ni la Dom tuu acha la Dar,
Home K-nyama wanachemba tunapokaa..

KIITIKIO
Ni gheto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linaloniweka kwenye chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo

Ni gheto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linaloniweka kwenye chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo.

VERSE 2:

Masela wanapenda kuja na mademu zao,
Nia yao waje kuwachapa nao,
Wakifika ndani wanaishia kuduwaa,
Mwishowe muda ukifika wanaishia wanatambaa,
Mara kesho yake demu anakuja peke yake,
Eti anazuga anamtafuta mchizi wake,
Nikimuelekezea kwake amfate,
Anadai eti amechoka anataka kidogo apumzike,
Akifka ndani haishi kukusifia,
Hata mchizi wake anaanza kumkandia,
Haipiti muda ameshanikumbatia,
Ooh ndiyo maana mimi nawapigaga tu mikasi,
Ndiyo kisa cha kugombana na Evance,
Aliponikuta ghetto na mdogo wake Nancy,

KIITIKIO
Ni ghetto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linalonipa chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo.

Ni ghetto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linalonipa chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo.

Ghetto langu,
Utadhani majuu,
Ndilo linalonipa hadhi ya juu,
Nimesota mpaka kulipata,

VERSE 3:
Ghetto tu ndio linanipa heshima,
Sijui itakuwaje kama nitalikatia bima,
Linanukia mapafyumu ya Kinyamwezi,
Na ma airfresh utadhani ghetto la Mase,
Nakupa laivu wala sijisifii,
Kama hauamini kamuulize hata P,
Au kama unataka njoo mwenyewe mpaka home,
Ukinikosa K-Nyama basi utanikuta Dom.

KIITIKIO
gheto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linaloniweka kwenye chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo

Ni gheto langu tu,
Linalowachengua maduu,
Linaloniweka kwenye chati za juu,
Kijitonyama mpaka East Zoo.
 
Back
Top Bottom