Mangwea ft Mwana FA & Lady Jaydee - Sikiliza (Lyrics)

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
kiitikio [ jide ]
Kama ni dem sikiliza (nisikilize mimi)
kama una swali uliza (niulize mimi)
hata kama sija malizaaa uliza x2

ubeti [Ngwear]
Madem ninyi nisikilizeni kwa makini mimi
hivi kwanini nyie mnakua hamjiamini
Mnajua nyie yaani mnanguvu zaidi ya sisi
Mwanaume kwa dem ni kama mfupa kwa fisi
sina nia ya kubadili maadili (siyo)
ninacho pinga nyie kushikwa masikio
sema tu hamjui umuhimu wenu, ila leo nita waambia tu ila iwe siri yenu
mi mwenyewe naenda club kila wiki
haina maana huwa nafuata tu muziki
Nikiwa Church huwa napaona hapalipi
hata niwe na hela vipi na rundo la marafiki
Vijijini ni asilimia 90 masikini starehe yao ni pombe na nyinyi
sasa mpaka lini mtakua mna nyanysika, na kudhalaulika
au wenyewe meridhika
kuolewa mna haki wala msiite bahati/ hivi we unadhani wanangu mi nitalea na nani
sema tu wengi wenu ni vicheche
Japo siyo moto ukuu na siogopi cheza

RUDIA KIITIKIO x2

ubeti 2 [ Mwana FA]
kwanza mi siamini kabisa mitungi
ukiacha mabinti siyo minelli siyo mirungi
ila nakosa imani nikiwaona mnajigonga
yaani hadhi yenu inashuka kimsimamo mnapo yumba
mnakosa nini kinachofanya msijiamini
au mwalimu wenu kipofu msemo na nyi mmeamini
msichimbe madini sawa, ila sio wote muwe wafanyakazi wa ndani
Hesabu hazipandi, so ningumu kuwa rubani/
ila hata kalani nina imani haishindikani
Big up kwa my mamy
Na wote ambao computer imelala kichwani
sisemi mlee wanaume kama mabinti
ila mnapo jitosheleza machaguo yanaongezeka
hamuoni basi someni
kama uliishi vibaya, kwa mwanao ilekebishe
wenye upeo mdogo ndo daima wanakua vicheche
kuolewa siyo lazima
japo inaongeza heshima
ina haja yake, hawatajali mke wa kigogo au mkulima
na ole wenu msio penda kutafuta vyenu
mnatamani tu vya wenzenu
ndiyo maana huwa mnamegwa na wazee wa umri wa babu zenu
nieleweni jikazeni
msipo komaa waume zenu watawaletea vicheche ndani
niamini Binamu B

RUDIA KIITIKIO x2

ubeti 3 [Ngwear]

wengine mnapenda sana vya kupewa
Ndiyo maana wengi wenu mnaishia kuchezewa
mna megwa mnaachwa
na hata mkiolewa
Ndoa inajaa visa na kuonewa
mfano ngwear narudi muda ninaotaka
na ukiniletea kibesi tu asubuhi talaka kwenu
sinajua hauna kitu zaidi ya begi lako
ila nisinge thubutu endapo nyumba ni yako
najua hamuwezi kwenda haja ndogo mmesimama
ila mnaouwezo wakufanya kila sisi tunacho fanya
hata kuwa Rais mwanamke pia ana haki
mladi tu awe na vigezo wanaume tunapata wapi
kama kusoma wote ruksa kusoma
Bado biashara hata ufundi wa kushona
wenzenu wachache bungeni simnawaona
hata kuimba imbeni tu wala msione noma
ka sister P, Zay B, Stara, Ray C
Je unataka kuendesha Prado kama Lady Jay Dee komando
Amini wote tumezaliwa watupu
Na kuvaa kutokana na juhudi tu za mtu
Haaaaalllaah

Rudia kiitikio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom