Mangwea ft Lady Jay Dee - Mapenzi gani? (Lyrics)

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,463
VERSE 1: Mangwea

Mami nakuona umekula pozi,
Mbona unaonesha kama umejawa na majonzi,
Nieleze kipi hasa kinachokuumiza kichwa, Mtoto mwenye uzuri kama hazina iliyofichwa,
Mwenye raha zote fedha ipo nyumba nzuri, Pia nakupongeza kwa tabia yako nzuri,
Lakini mumeo anakufanya kama msukule, Na mapenzi yako ya dhati ndio yampa kiburi,
Mapenzi gani kila siku kugombana, Mnashindwa kukaa chini kuongea na kuelewana?
Na bila mateke na ngumi kutupiana,
Basi mwafaka ndani ya nyumba bado haujapatikana,
Mapenzi gani kwa mtu asiyeona yako thamani
Kukudhalilisha kwa ndugu na majirani,
Ndoa yenu matope anaipaka,
Na hata baadhi ya rafiki zako tayari ameshawataka,
Anakudhalilisha na tabia yake ya kishenzi, Japo amekukabidhi utembelee lake benzi,
Ila nani atakata kiu yako ya mapenzi,
Na hadi U feel kuwa crazy.CHORUS
VERSE 2: Mangwea

Na najua unampenda sana huyu mtu, Najua anakupatia kila kitu,
Ila sidhani kama kweli vinatoka moyoni, Naona sawa tu na porojo zake za mdomoni,
Unapo ongea nae kwenye simu,
Na kukupa maneno yake matamu yakuachayo ukitabasamu,
Bila kufahamu huko alipo pembeni yupo na demu,
Sehemu sehemu wanakula good time,
Na kurudi kwake usiku amechelewa,
Tena amelewa na hakuna anachokuelewa.
Kula hataki eti hana appetite,
Na kubwaga mziki unyumba hajisikii.
Kwani vyote alishavipata huko alikotoka,
Na akilala amekufa jinsi alivyochoka.
Wewe kote utachakarika hata maiki utashika,
Na hata kuna kucha na jogoo kuwika.
Huu msala dadaangu nasala,
Hivi kipi hasa kinachokufanya umgande huyu fala?
Nakiri kweli ana hela ila huoni maisha yako,
Hayana tofauti na mateka ndani ya jela!?
CHORUS: Lady Jay Dee
Sina maana sijui uwe na mimi anha anha.
Lakini umpate mmoja tu atakae kuthamini coz wewe ni bonge la queen.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom