Mangula ndio amekwisha kabisa kisiasa?

Mangula ndio amekwisha kabisa kisiasa?

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
3,605
Reaction score
551
Baadhi ya wanaCCM tuliamini kuwa kurudi kwa Philips Mangula katika medani za juu za uongozi wa CCM kungeleta mwamko mpya, mabadiliko makubwa na hamasa kubwa kwa CCM, lakini hali imekuwa tofauti kabisa.

Mangula hana kazi yoyote ya maana ambayo amefanya ndani ya CCM mpaka sasa, lakini pia kifikra na kujieleza Mangulla amechoka sana kama tulivyomshuhudia jana kwenye runinga wakati wa mjadala wa kipindi cha Uzalendo.

CCM ndani kwa ndani tumechoka mno na kwa nje tunazidi kuchokwa zaidi. Binafsi sioni hatua zozote za maana zinazofanywa na viongozi wa juu wa CCM hususani Philips Mangula kunusuru hali hii.
Je, hali hii inaashiria kwisha kabisa kisiasa kwa Mangula?
 
Tabu yetu tuna haraka sana katika mambo makubwa, Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mang'ula na timu ya JK wao ni wana mtandao, Mang'ula hakuwa na hatakuwa mwana mtandao. Ni sawa na kuchanganya maji na mafuta wakati yana density tofauti wala havitachanganyika kabisa. Sisi tusubiri kunyolewa tu kimya kimya.

Mpaka tutakapo amua kurudisha Azimio la Arusha na Maadili ya viongozi. Vinginevyo tujiandae kwa anguko kubwa sana.
 
CCM wamechoka kifikra.....akili zimechoka wanaweza kufikiria na kutatua mabo mepesi mepesi.....tena kwa njia za shortcut.......angalia hata vijana wao humu ndani.....kazi ni kumzungumzia slaa na mbowe......hawezi kuongea mambo ya maana ya kitaifa.....they are tired...lakini pia wengi ni waswahili waswahili...wavivu wa kufikiri....?
 
Tabu yetu tuna haraka sana katika mambo makubwa, Kuna tofauti kubwa sana kati ya Mang'ula na timu ya JK wao ni wana mtandao, Mang'ula hakuwa na hatakuwa mwana mtandao. Ni sawa na kuchanganya maji na mafuta wakati yana density tofauti wala havitachanganyika kabisa. Sisi tusubiri kunyolewa tu kimya kimya.

Mpaka tutakapo amua kurudisha Azimio la Arusha na Maadili ya viongozi. Vinginevyo tujiandae kwa anguko kubwa sana.
Ni lini sasa wanaCCM tutaanza kuona matunda ya uongozi wa Philip Mangula, maana ni miezi nane sasa toka awe makamu Mwenyekiti wa CCM imepita na hakuna lolote na hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku.
Kumbuka mwakani 2014 kuna uchaguzi wa Serikali za mitaa na 2015 uchaguzi mkuu, sasa tutasubiri mpaka lini?

Lakini ni yeye mwenyewe Mangula aliyetuahidi wanaCCM matunda mazuri kwa kipindi kifupi, kwa mfano, Mangulla alijiapiza kuwafukuza mafisadi wote ndani ya Miezi sita!! Sasa ni zaidi ya miezi nane na hakuna fisadi yoyote aliyechukuliwa hatua.

Kama Mangulla hakubaliani na mfumo na mtandao mchafu wa kisiasa wa Kikwete ndani CCM kwanini basi alikubali nafasi hiyo na kwanini basi bado anang'ang'ania mpaka sasa?
 
Binafsi nilidhani Mangula kapatwa na ugonjwa mkubwa kama wa kiharusi

Duh!
 
Mangula ni Divai ya zamani ndani ya chupa ya zamani hakuna jipya hapo. Product ikikwa mbaya walau paking iwe nzuri kuvutia walaji. CCM inahitaji vijana mahiri wenye weledi na sio vijana waropokaji, kwa sasa Mangula anahitaji kupumzika ameshapitwa na wakati.
 
Mangula hajazoea na hakutarajia kuona siasa za kuchinjana, kubambikiana ugaidi na hata kurushiana mabomu zinazofanywa na akina savimbi na wabeba mikoba wake.
 
MACCM ni washahili tu yaani Mangula kawekwa na KIkwete huku akiendeshwa kwa remote wewe huoni hata KInana kachoka ,Nape anarudisha majeshi nyuma kaachwa Mwigulu akikamata nafasi zote kwa sababu watafanya nini kila wanachofanya wananchi hawataki utachoka tuu mtu
 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa , jina la bwana lihimidiwe , uwekwe mahali unapostahili ccm , wote tuseme amina .
 
Mangula peke yake atafanya nini wakati amezungukwa na many'ang'au!!! Kikwete kuwa pale na Mangula ni convenience tu kwani Kikwete alimdhalilisha sana huyu mzee baada ya kuukwaa Urais; kwanini alishawishika kurudi baada ya dhahama waliomfanyia atajua mwenyewe moyoni mwake!!
 
Binafsi nilidhani Mangula kapatwa na ugonjwa mkubwa kama wa kiharusi

Duh!

Hata mimi nilijua labda Mangula kahojiwa akiwa mgonjwa na pale imemlazimu tu. Hakuwa na uchangamfu wowote na hakuwa akijibu maswali kwa weledi kabisa!!

Yaani ukweli nadhani CCM kipindi hicho watakilaani sana na wanaweza wakagomea kabisa maana kinawadhalilisha kabisa.
 
Hakuna mangula,nape wala kinana! Wote wamefunikwa na mropokaji mwigulu!
Mwigulu ndio makamu mwenyekiti,katibu mkuu,katibu itikad na uenezi!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hivi ni kipindi gani Mangula amewahi kuwa juu kisiasa? ninachoweza kusema hapa ni kwamba huko nyuma alikuwa anasaidiwa na unyonge wa vyama vyetu vya upinzani pamoja na elimu ndogo ya uraia kwa watanzania, hali ambayo kwa sasa imebadilika.
 
Hata mimi nilijua labda Mangula kahojiwa akiwa mgonjwa na pale imemlazimu tu. Hakuwa na uchangamfu wowote na hakuwa akijibu maswali kwa weledi kabisa!!

Yaani ukweli nadhani CCM kipindi hicho watakilaani sana na wanaweza wakagomea kabisa maana kinawadhalilisha kabisa.

Ni mgonjwa wa mawazo. Alidhani CCM ni ile ya Mkapa. Hamadi! Kumbe ni kitu tofauti kabisa. Akazidi kushtuka na hoja ya baby Nape kuwa wazee wanasubiri kufa. Akazidi kuchanganyikiwa. Anavyomwogopa Savimbi hakuthubutu kuzungumzia tabia yake isiyokublika bungeni. Sijui angeongea nini kuhusu ujangili. Ushauri wa bure. Mangula arudi kijijini kulima nyanya na kufurahia ndoa yake kama anataka kufurahia maisha ya uzeeni. Poor man.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sijui kilichompata Mangula but whatever it is isn't good at all for CCM. Contrary to everybody's expectation Mangula so far has taken only single notable action: marrying. I am so disappointed with him. A man who got appointed to restore hope, clean the party and reinforce patriotism and discipline as reduced himself to nothing, leaving his fans (I included) with some unanswered questions.

He needs to wake up before we judge him failure. The party got some outstanding issues and he can't keep us on hold anymore. Enough time he got to organize his team and get back to work on people's expectation. Mangula, of all the new party leaders owes us some serious party cleanups. Yes, top-down type of cleanups. We praised his appointment because we trusted he was the much needed therapy to the ills of the party but now he gives us reason to think his therapy, if any, is as less effective as placebo or that of babu wa Loliondo.

Strangely people still believe in Mangula's ability to bring good change and direction to the party. As that isn't enough they believe he is going to do today if not tomorrow. They less they forget is that Mangula is dead asleep. Wake up Mangula, Chadema is stealing the party.
 
nimeona itv kikao cha ndani cha ccm kinachofanywa mbeya na kina lemutumboz inatumika nguvu kubwa sana kumjadili sugu.
yani ccm wamepagawa hawajielewi.
 
Back
Top Bottom