Hakuna the seating president kutoka CCM aliyewahi kufanikiwa kumuweka mtu wake baada ya kuondoka madarakani.
- JK Nyerere Chaguo lake lilikuwa Dr. Salim Ahmed Salim, lakini akazidiwa kete na Wanzazibari (hard core ASP zelots) Mzee Mwinyi akaukwaa URAIS wa JMT
- Mzee Ali Hassan Mwinyi Chaguo lake lilikuwa Samuel (aka Jumanne) Malecela. Nyerere akamzidi kete Mwinyi, Mkapa akaukwaa URAIS wa JMT
- Benjamin W. Mkapa Chaguo lake lilikuwa Frederick T. Sumaye. Wanamtandao wakamzidi kete Mkapa, Kikwete akaukwaa URAIS wa JMT
- Tunaambiwa Chaguo la JK ni Benard Membe. Ngoja tuone kama Mfupa uliomushinda FISI JK atauweza 2015!
Kwa upande mwingine ninali miss sana GAZETI la MWANAHALISI, kwani ninaamini ndilo lingekuwa na uthubutu wa kuandika hiyo dossier ya Mangula na Sozigwa iliyokuwa inamkataa Kikwete kwamba hana SIFA ZA KUWA RAIS. BTW, the guys were damned RIGHT na sasa tuna-pay PRICE kwasababu CCM hawakutaka kuwasikiliza Mangula na Sozigwa.
Lakini kitendo cha Mangula kurudia kula MATAPISHI yake kimemshushia hadhi na heshima sio tu mbele ya CCM bali hata kwa watanzania wote makini kama mimi. Na kama MWANAHALISI ingetoa hiyo dossier nafikiri ndiyo ungekuwa mwisho wa Mangula kupayuka payuka majukwaani na kutoa ahadi HEWA ya kuwashughulikia watoa RUSHWA wote ndani ya miezi 6.