Mangula na Paul Sozigwa Waraka wenu wa JK Hafai kuwa Rais Mmeuchoma?

Ndg wanajamvi katika harakati za kuhakikisha kuwa ccm inatoa kiongozi bora kwenye safu ya Uraisi mwaka 2005 ,Ndg Mangula akiwa Katibu mkuu wa ccm kupitia kamati ya maadili na usalama iliandaa dossier ya Kikwete na kubainisha kuwa hakuwa na sifa ya kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa binafsi za kiuchunguzi na kitelijensia kutoka ccm makao makuu zilionyesha kuwa Kikwete hakuwa na sifa za kimaadili za kupendekezwa kuwa Rais na kwamba Katibu mkuu alitaka ccm ipendekeze jina la mwanachama mwingine.Ingawa Kikwete alijua dossier yake hiyo ya kumdisqualify alitumia WANAMTANDAO (ROSTAM NA LOWASA) kumtisha mwenyekiti wa ccm(Mkapa) na Mangula Mwenyewe na hatimaye Mwenyekiti wa ccm ,mzee Mkapa aliondoa dossier ya Kikwete kwenye kikao cha CC-Kamati kuu na kufunika mwanaharamukupita.Katika uchunguzi wa kina umebainisha kuwa mara tu baada Kikwete kuingia Ikulu na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ccm ilikuwa kumuondoa Mangula na Sekretariat yake yote na wasaidizi wao akiwemo Mapuri, Paul Sozigwa mzee wa Kisarawe na Mangula Mwenyewe kulipiza kisasi maana walitaka kumwaga ugali wa Kikwete.Na mangual vyeo vyote alivyogombea ndani ya ccm alisambaratishwa kwa msaada wa wana mtandao/

Maswali machache ya kumuuliza Mangula ni je
1.Yeye kukubali kuwa MAKAMU ccm bara kumsaidia Kikwete ambaye awali aliona hana maadili alitumiwa?.
2.Ni njaa imemzidi na kukubali kutmikia tumbo kuliko nafsi ya ukweli wake?.
3.Je yupo tayari kuwaeleza wan ccm na watanzania dossier ya Kikwete inaeleza nini hata kabla ya hajafa ?
4.Je anajutia chochote kuwa kiongozi tena ndaniya ccm?
ongezea
5.Anaweza kuelezea kilichomtokea wakati akigombea uenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa?
6.Aliwaeleza nini wana ccm walipomwita katika kikao kujieleza wakati alipokuwa akikibeza chama kuwa kimepoteza mwelekeo wakaacha kumkolimba.
 
hilary clinton alisemaga kua obama hafai kua rais wakati wa kampeni 2008 lakini obama alivyoshinda akampa clinton secretary of state..siasa ni siasa...leo mnaumbuana kesho mnakaa meza moja mnakula pamoja...
 
Nadhani mkipata kitabu kilichoandikwa na yule mzee anayerusha kipindi cha JE, TUTAFIKA? mtapata habari za namna BEN alivyopindisha mambo ili JK apite lakini kwa bora liende na ndo sababu BEN hakutaka kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM mora moja alimwachia JK kabla ya uchaguzi mkuu wa 2007.
 
Inawezekana ikawa kweli unayosema, lakini pamoja na wanamtandao kushinda na Jk kuchukua Nchi bado hakukuondoa ukweli wa Mangula, kuna wakati watu hurejerea yaliyopita na kufanya uchambuzi wa maamuzi yaliyopita katika lengo la kufanya tathimini. Mangula anabaki shujaa mwanasiasa ambaye hana kelele na kwa taarifa ya wana JF ili ushujaa wake udhihilike anatakiwa kufanya mambo ya ziada kumaanisha kile alichokua anaamini mwaka 2005 mie namuombea kheri.
Mangula jipya la kusema wala kufanya. Yeye Mangula alisema JK hana sifa na maadili ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mangula hawezi tena kuthibitisha aliyoyasema, anayeweza kuthibitisha au kukanusha mtazamao huo ni uongozi wa sasa wa JK. Ushujaa wake unathibitishwa na kurudi kwake kwenye safu ya uongozi. Uamuzi huu ndiyo unaweza ama kumpa ushujaa Mangula ama kufikiria kuwa huenda ushauri wake uliopingwa sasa umeanza kukubalika, lakini pengine inaweza kuwa kejeli kwake. Wachambuzi wa siasa za kibongo wanaweza wakasema ' yule uliyesema hana sifa za kuongoza, sasa anaongoza na kukuteua pia kwa nafasi ileile uliyosema haiwezi, je; bado unasema hana uwezo. Ni ubishi wa kitoto kwani kila kitu kiko wazi sasa. Kundi ambalo ni pro. JK halitakiri lakini pia Ant JK watasema Mangula alisema kweli. Tuiachie Historia itajibu.
 
hilary clinton alisemaga kua obama hafai kua rais wakati wa kampeni 2008 lakini obama alivyoshinda akampa clinton secretary of state..siasa ni siasa...leo mnaumbuana kesho mnakaa meza moja mnakula pamoja...
sikumbuki hata siku moja Clinton kusema Obama hana maadili ya kuwa kiongozi that is a very serious allegation. ni mtu anayeendekeza njaa tu ndiye anayeweza kukubali kufanya kazi na mtu asiye na maadili.
 
Mimi sijui tuseme nini ili sura ya halisi ya CCM ieleweke kwa watanzania. Mwaka 2005 Kikwete hakuwa chaguo la Mkapa. Timu ya Mkapa ilikuwa na watu wake. Mkapa alizidiwa kete katika kutupa karata ya mrithi aliyempenda. Kikwete akapita kwa nguvu ya waliompitisha. Kikwete alivyo mtu wa visasi aliwaondoa wote na kuweka mtandao wake. Hii ndiyo ilikuwa 'turning point' ya maisha ya Mtanzania. Toka hapo, Kikwete alikosa control ya kuongoza nchi. Mtandao ukashika hatamu hata leo! Kitendo cha Mangula na Kinana kukubali nafasi walizopewa ni ajabu na unafiki. Kwanza Kinana alisema anastaafu saisa. Halafu Mangula akasema JK hafai. Kumbe haya yanatupa picha moja. CCM TUMBO KWANZA! Period!
Good analysis keep up
 
Mangula jipya la kusema wala kufanya. Yeye Mangula alisema JK hana sifa na maadili ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mangula hawezi tena kuthibitisha aliyoyasema, anayeweza kuthibitisha au kukanusha mtazamao huo ni uongozi wa sasa wa JK. Ushujaa wake unathibitishwa na kurudi kwake kwenye safu ya uongozi. Uamuzi huu ndiyo unaweza ama kumpa ushujaa Mangula ama kufikiria kuwa huenda ushauri wake uliopingwa sasa umeanza kukubalika, lakini pengine inaweza kuwa kejeli kwake. Wachambuzi wa siasa za kibongo wanaweza wakasema ' yule uliyesema hana sifa za kuongoza, sasa anaongoza na kukuteua pia kwa nafasi ileile uliyosema haiwezi, je; bado unasema hana uwezo. Ni ubishi wa kitoto kwani kila kitu kiko wazi sasa. Kundi ambalo ni pro. JK halitakiri lakini pia Ant JK watasema Mangula alisema kweli. Tuiachie Historia itajibu.
hakuna shujaa ambaye anaweza kukubali kutumwa na mtu aliyemwita hana maadili. angekataa cheo cha mtu asiye na maadili labda hapo tungeweza kumuita mwenye msimamo kwa maana ameweza kuyasimamia maneno yake na siyo level ya kuitwa shujaa oneni aibu jamani shujaa mnajua maana yake ??
 
Mimi sijui tuseme nini ili sura ya halisi ya CCM ieleweke kwa watanzania. Mwaka 2005 Kikwete

hakuwa chaguo la Mkapa. Timu ya Mkapa ilikuwa na watu wake. Mkapa alizidiwa kete katika kutupa

karata ya mrithi aliyempenda. Kikwete akapita kwa nguvu ya waliompitisha. Kikwete alivyo mtu wa

visasi aliwaondoa wote na kuweka mtandao wake. Hii ndiyo ilikuwa 'turning point' ya maisha ya Mtanzania. Toka hapo, Kikwete alikosa control ya kuongoza nchi. Mtandao ukashika hatamu hata leo! Kitendo cha Mangula na Kinana kukubali nafasi walizopewa ni ajabu na unafiki. Kwanza Kinana alisema anastaafu saisa. Halafu Mangula akasema JK hafai. Kumbe haya yanatupa picha moja. CCM
TUMBO KWANZA! Period!

Lazima ulipata A ya DS pale UDSM.
 
Hakuna habari ya njaa hapa ... Mangula yuko sahihi ... achape kazi!! Akate kazi kwa nini?
 
JK ANAJUA MANGULA NDIYE MTU PEKEE ATAKAYEWANYAMAZISHA WAPINZANI kwani mpaka sasa si vijiweni sio Magazeti hata kwenye Mitandao ni Mangula MANGULA MANGULA hawajadili chochote kuhusu mustakabali wa nchi ila ni Uchaguzi ujao wa 2015
Mangula hahusiki na kumkatalia JK yeye aliletewa Faili na Sozigwa na vivyo hivyo na wengine wote km Salim A. Salim Mwandosya na wengineo hivyo Mkapa hakuwa na ubavu baada ya kugundua hata 1995 JK alipita Chimwaga lakini JK Nyerere akaingilia
Kwa sasa JK ndiye atakayemaliza ungwe yake, na Mangula hawezi zuia mabadiliko sioni haja ya kuwa na muhumkwe
 
sikumbuki hata siku moja Clinton kusema Obama hana maadili ya kuwa kiongozi that is a very serious allegation. ni mtu anayeendekeza njaa tu ndiye anayeweza kukubali kufanya kazi na mtu asiye na maadili.
Politiki, nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja. Haiwezekani mtu asiye na maadili na kutofaa kuwoa kiongozi wa nchi, leo hii ukae nae na uwe chini yake akuagize na wakati mwingine hata akukaripie unapoenda kinyume na matakwa yake. Ni njaa tu ndiyo inayotufikisha hapo.
 
Hakuna the seating president kutoka CCM aliyewahi kufanikiwa kumuweka mtu wake baada ya kuondoka madarakani.
  1. JK Nyerere Chaguo lake lilikuwa Dr. Salim Ahmed Salim, lakini akazidiwa kete na Wanzazibari (hard core ASP zelots) Mzee Mwinyi akaukwaa URAIS wa JMT
  2. Mzee Ali Hassan Mwinyi Chaguo lake lilikuwa Samuel (aka Jumanne) Malecela. Nyerere akamzidi kete Mwinyi, Mkapa akaukwaa URAIS wa JMT
  3. Benjamin W. Mkapa Chaguo lake lilikuwa Frederick T. Sumaye. Wanamtandao wakamzidi kete Mkapa, Kikwete akaukwaa URAIS wa JMT
  4. Tunaambiwa Chaguo la JK ni Benard Membe. Ngoja tuone kama Mfupa uliomushinda FISI JK atauweza 2015!

Kwa upande mwingine ninali miss sana GAZETI la MWANAHALISI, kwani ninaamini ndilo lingekuwa na uthubutu wa kuandika hiyo dossier ya Mangula na Sozigwa iliyokuwa inamkataa Kikwete kwamba hana SIFA ZA KUWA RAIS. BTW, the guys were damned RIGHT na sasa tuna-pay PRICE kwasababu CCM hawakutaka kuwasikiliza Mangula na Sozigwa.

Lakini kitendo cha Mangula kurudia kula MATAPISHI yake kimemshushia hadhi na heshima sio tu mbele ya CCM bali hata kwa watanzania wote makini kama mimi. Na kama MWANAHALISI ingetoa hiyo dossier nafikiri ndiyo ungekuwa mwisho wa Mangula kupayuka payuka majukwaani na kutoa ahadi HEWA ya kuwashughulikia watoa RUSHWA wote ndani ya miezi 6.

Bobuk hii ya Tanzania bila Mwanahalisi binafsi inaninyima raha kabisa. Nalikuwa na utaratibu wa kusoma gazeti hili jumapili, siku hizi jumapili yangu imepwaya sana...sijui Mwanahalisi na halali atarudi lini
 
Kelele za wazee wastaafu ambao wameondolewa ktk vikao rasmi vya chama + njaa ndizo sababu kuu zimemrudisha Mangula. Wamerudi kuunda timu ya kusaka fedha za kununua kura na wizi wa kura uchaguzi wa 2015!
 
Hakuna the seating president kutoka CCM aliyewahi kufanikiwa kumuweka mtu wake baada ya kuondoka madarakani.
  1. JK Nyerere Chaguo lake lilikuwa Dr. Salim Ahmed Salim, lakini akazidiwa kete na Wanzazibari (hard core ASP zelots) Mzee Mwinyi akaukwaa URAIS wa JMT
  2. Mzee Ali Hassan Mwinyi Chaguo lake lilikuwa Samuel (aka Jumanne) Malecela. Nyerere akamzidi kete Mwinyi, Mkapa akaukwaa URAIS wa JMT
  3. Benjamin W. Mkapa Chaguo lake lilikuwa Frederick T. Sumaye. Wanamtandao wakamzidi kete Mkapa, Kikwete akaukwaa URAIS wa JMT
  4. Tunaambiwa Chaguo la JK ni Benard Membe. Ngoja tuone kama Mfupa uliomushinda FISI JK atauweza 2015!

Kwa upande mwingine ninali miss sana GAZETI la MWANAHALISI, kwani ninaamini ndilo lingekuwa na uthubutu wa kuandika hiyo dossier ya Mangula na Sozigwa iliyokuwa inamkataa Kikwete kwamba hana SIFA ZA KUWA RAIS. BTW, the guys were damned RIGHT na sasa tuna-pay PRICE kwasababu CCM hawakutaka kuwasikiliza Mangula na Sozigwa.

Lakini kitendo cha Mangula kurudia kula MATAPISHI yake kimemshushia hadhi na heshima sio tu mbele ya CCM bali hata kwa watanzania wote makini kama mimi. Na kama MWANAHALISI ingetoa hiyo dossier nafikiri ndiyo ungekuwa mwisho wa Mangula kupayuka payuka majukwaani na kutoa ahadi HEWA ya kuwashughulikia watoa RUSHWA wote ndani ya miezi 6.

Bobuk leo umenena, nimependa mpangilio wako No 1-4. Kwa upande mwingine nilifikiri kuwa wewe ni mmoja wa waandishi wa Mwanahalisi, maana kwa mtindo huo ndio hilo gazeti lilikuwa linapayuka.

Kifupi, kushindana kete au kutoshindana, lakini la msingi la kuelewa ni moja ; CCM NI YA AKINA NANI? Wengi walifikiri kuwa Nyerere alipokufa basi CCM ilikuwa haina mwenyewe, waliofikiri hivyo walikosea. CCM ina wenyewe na mkoba walikabidhiwa na Baba wa Taifa.

CCM haikuwa ya Mwinyi wala Mkapa, hawa wote walikuwa wapita njia tu. Lakini sasa imefika na wala haitaondoka, na baada ya 2015 ndio mtajua kama chama kimeshikwa na nani? Mimi jibu nalijua, lakini sipendi kulisema leo na tusubiri mpaka 2015.
 
Walichokiseama amngula na Sozigwa kuimeonekana dhahiri, tyaani udhaifu wa Raisi umejionyesha waziwazi hat kutamkwa na wapinzani. Ndio maana Mangula karejeshwa ili kuondoa udhaifu ndani ya chama hadi wserikalini.
 
Porojo za Jumapili hizo

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Yaliyopita si yamepita.......sidhani kama hilo lina nafasi kwa sasa, ila walichokuwa wanataka kuwaambia wana CCM wamekiona sasa.... sidhani kama ni busara kukataa ombi la Mwenyekiti wake wa chama.... kwa mwelevu yeyote, nadhani unapofuatwa kuombwa, maana yake wanakubaliana na msimamo wako wa awali, s lazima aseme, ila mwelevu utajua tu kuwa saa wanatambua mchango wako
 
CCM inapofikia kuhujumu nchi wanakuwa pamoja hata Kama wanatofautiana kimtizamo.

CCM lao moja, tumbo kwanza ufisadi mbele. Maslahi ya taifa yalikwisha zikwa.

Back
Top Bottom