Mangula na Paul Sozigwa Waraka wenu wa JK Hafai kuwa Rais Mmeuchoma?

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020
1,225
Ndg wanajamvi katika harakati za kuhakikisha kuwa ccm inatoa kiongozi bora kwenye safu ya Uraisi mwaka 2005 ,Ndg Mangula akiwa Katibu mkuu wa ccm kupitia kamati ya maadili na usalama iliandaa dossier ya Kikwete na kubainisha kuwa hakuwa na sifa ya kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa binafsi za kiuchunguzi na kitelijensia kutoka ccm makao makuu zilionyesha kuwa Kikwete hakuwa na sifa za kimaadili za kupendekezwa kuwa Rais na kwamba Katibu mkuu alitaka ccm ipendekeze jina la mwanachama mwingine.Ingawa Kikwete alijua dossier yake hiyo ya kumdisqualify alitumia WANAMTANDAO (ROSTAM NA LOWASA) kumtisha mwenyekiti wa ccm(Mkapa) na Mangula Mwenyewe na hatimaye Mwenyekiti wa ccm ,mzee Mkapa aliondoa dossier ya Kikwete kwenye kikao cha CC-Kamati kuu na kufunika mwanaharamukupita.Katika uchunguzi wa kina umebainisha kuwa mara tu baada Kikwete kuingia Ikulu na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ccm ilikuwa kumuondoa Mangula na Sekretariat yake yote na wasaidizi wao akiwemo Mapuri, Paul Sozigwa mzee wa Kisarawe na Mangula Mwenyewe kulipiza kisasi maana walitaka kumwaga ugali wa Kikwete.Na mangual vyeo vyote alivyogombea ndani ya ccm alisambaratishwa kwa msaada wa wana mtandao/

Maswali machache ya kumuuliza Mangula ni je
1.Yeye kukubali kuwa MAKAMU ccm bara kumsaidia Kikwete ambaye awali aliona hana maadili alitumiwa?.
2.Ni njaa imemzidi na kukubali kutmikia tumbo kuliko nafsi ya ukweli wake?.
3.Je yupo tayari kuwaeleza wan ccm na watanzania dossier ya Kikwete inaeleza nini hata kabla ya hajafa ?
4.Je anajutia chochote kuwa kiongozi tena ndaniya ccm?
 
POMPO

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
6,690
1,195
Mambo ya Magamba wengine hatuyajui, tuachie wanayoyaweze wacha sie tufanye yetu...
 
Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,230
2,000
kangaJK alijibu hili akiwasili KIA from Dom huku sikia alichosema? acha kuendekeza majungu
 
Last edited by a moderator:

Joseph

JF-Expert Member
Aug 3, 2007
3,521
1,225
Mangula sidhani hata kama yumo humu JF,ila Nape kwa kiherehere chake anaweza kumjibia maswali hayo.
 
kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020
1,225
JK alijibu hili akiwasili KIA from Dom huku sikia alichosema? acha kuendekeza majungu
Watu nawe unakurupuka tunataka viongozi wanaojisimamia kama Mangula aliamini Kikwete hafai kuwa Rais kwa nini leo amtumikie kama siyo kutumika kama kondomu?
 
Last edited by a moderator:

Watu

JF-Expert Member
May 12, 2008
3,230
2,000
Watu nawe unakurupuka tunataka viongozi wanaojisimamia kama Mangula aliamini Kikwete hafai kuwa Rais kwa nini leo amtumikie kama siyo kutumika kama kondomu?

No! JK alisha samehe, ww kama umtumwa na mangula ambaye bado anakinyongo(kitu ambacho sidhani kama anaweza kutuma umseme), lakini njaa inamsuta shauri yako ....
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,342
2,000
Mangula alikuwa na Mtandao wake 2005 ila ulikuwa weak sana na alifanya makosa kama aliyofanya Mashishanga na mtandao wake wa Sumaye,Afisa mifugo ambaye alipata bahati ya kuwa waziri mkuu from nowhere mara akataka awe rais. Watu wazima wakina Kikwete wakamtuliza hakufika popote.
 
Ronn M

JF-Expert Member
May 2, 2012
1,279
0
Mimi sijui tuseme nini ili sura ya halisi ya CCM ieleweke kwa watanzania. Mwaka 2005 Kikwete

hakuwa chaguo la Mkapa. Timu ya Mkapa ilikuwa na watu wake. Mkapa alizidiwa kete katika kutupa

karata ya mrithi aliyempenda. Kikwete akapita kwa nguvu ya waliompitisha. Kikwete alivyo mtu wa

visasi aliwaondoa wote na kuweka mtandao wake. Hii ndiyo ilikuwa 'turning point' ya maisha ya Mtanzania. Toka hapo, Kikwete alikosa control ya kuongoza nchi. Mtandao ukashika hatamu hata leo! Kitendo cha Mangula na Kinana kukubali nafasi walizopewa ni ajabu na unafiki. Kwanza Kinana alisema anastaafu saisa. Halafu Mangula akasema JK hafai. Kumbe haya yanatupa picha moja. CCM
TUMBO KWANZA! Period!
 
kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020
1,225
Ronn M Hapo upo sawa, viongozi wa matumbo kama Mangula hawatufai na kujisifu kuwa yeye ni mwanafunzi mwaminifu wa Mwalimu Nyerere ni kumdhalilisha sana Baba wa Taifa.
 
Last edited by a moderator:

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Hakuna the seating president kutoka CCM aliyewahi kufanikiwa kumuweka mtu wake baada ya kuondoka madarakani.
  1. JK Nyerere Chaguo lake lilikuwa Dr. Salim Ahmed Salim, lakini akazidiwa kete na Wanzazibari (hard core ASP zelots) Mzee Mwinyi akaukwaa URAIS wa JMT
  2. Mzee Ali Hassan Mwinyi Chaguo lake lilikuwa Samuel (aka Jumanne) Malecela. Nyerere akamzidi kete Mwinyi, Mkapa akaukwaa URAIS wa JMT
  3. Benjamin W. Mkapa Chaguo lake lilikuwa Frederick T. Sumaye. Wanamtandao wakamzidi kete Mkapa, Kikwete akaukwaa URAIS wa JMT
  4. Tunaambiwa Chaguo la JK ni Benard Membe. Ngoja tuone kama Mfupa uliomushinda FISI JK atauweza 2015!

Kwa upande mwingine ninali miss sana GAZETI la MWANAHALISI, kwani ninaamini ndilo lingekuwa na uthubutu wa kuandika hiyo dossier ya Mangula na Sozigwa iliyokuwa inamkataa Kikwete kwamba hana SIFA ZA KUWA RAIS. BTW, the guys were damned RIGHT na sasa tuna-pay PRICE kwasababu CCM hawakutaka kuwasikiliza Mangula na Sozigwa.

Lakini kitendo cha Mangula kurudia kula MATAPISHI yake kimemshushia hadhi na heshima sio tu mbele ya CCM bali hata kwa watanzania wote makini kama mimi. Na kama MWANAHALISI ingetoa hiyo dossier nafikiri ndiyo ungekuwa mwisho wa Mangula kupayuka payuka majukwaani na kutoa ahadi HEWA ya kuwashughulikia watoa RUSHWA wote ndani ya miezi 6.
 
kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,020
1,225
Bobuk hapo nakubaliana nawewe mkuu,MwanaHalisi Gazeti kwa Great Thinkers mafisadi wamelichinjia baharini na kukizingatia harakati za uchaguzi zinakaribia kwa mwaka 2015 mafisadi na wachafu wote na kambi zao watahakikisha halipo mitaani. Na mshauri Kubenea aanzishe online ambalo litanunuliwa kwa electroni na mtu anaweza kuprint na kusoma na ndg zake home hii ni kwa ajili ya kukomboa wana wa Tanzania Halisi
 
MAKAH

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,589
0
siasa si hasa - yeye kutowaafiki kuchukua nchi na wao kumwangukia kabla hata hakujacha.
 
Wimbo

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
608
500
Hakuna the seating president kutoka CCM aliyewahi kufanikiwa kumuweka mtu wake baada ya kuondoka madarakani.
  1. JK Nyerere Chaguo lake lilikuwa Dr. Salim Ahmed Salim, lakini akazidiwa kete na Wanzazibari (hard core ASP zelots) Mzee Mwinyi akaukwaa URAIS wa JMT
  2. Mzee Ali Hassan Mwinyi Chaguo lake lilikuwa Samuel (aka Jumanne) Malecela. Nyerere akamzidi kete Mwinyi, Mkapa akaukwaa URAIS wa JMT
  3. Benjamin W. Mkapa Chaguo lake lilikuwa Frederick T. Sumaye. Wanamtandao wakamzidi kete Mkapa, Kikwete akaukwaa URAIS wa JMT
  4. Tunaambiwa Chaguo la JK ni Benard Membe. Ngoja tuone kama Mfupa uliomushinda FISI JK atauweza 2015!

Kwa upande mwingine ninali miss sana GAZETI la MWANAHALISI, kwani ninaamini ndilo lingekuwa na uthubutu wa kuandika hiyo dossier ya Mangula na Sozigwa iliyokuwa inamkataa Kikwete kwamba hana SIFA ZA KUWA RAIS. BTW, the guys were damned RIGHT na sasa tuna-pay PRICE kwasababu CCM hawakutaka kuwasikiliza Mangula na Sozigwa.

Lakini kitendo cha Mangula kurudia kula MATAPISHI yake kimemshushia hadhi na heshima sio tu mbele ya CCM bali hata kwa watanzania wote makini kama mimi. Na kama MWANAHALISI ingetoa hiyo dossier nafikiri ndiyo ungekuwa mwisho wa Mangula kupayuka payuka majukwaani na kutoa ahadi HEWA ya kuwashughulikia watoa RUSHWA wote ndani ya miezi 6.

Inawezekana ikawa kweli unayosema, lakini pamoja na wanamtandao kushinda na Jk kuchukua Nchi bado hakukuondoa ukweli wa Mangula, kuna wakati watu hurejerea yaliyopita na kufanya uchambuzi wa maamuzi yaliyopita katika lengo la kufanya tathimini. Mangula anabaki shujaa mwanasiasa ambaye hana kelele na kwa taarifa ya wana JF ili ushujaa wake udhihilike anatakiwa kufanya mambo ya ziada kumaanisha kile alichokua anaamini mwaka 2005 mie namuombea kheri.
 
bantulile

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,572
1,250
Watu nawe unakurupuka tunataka viongozi wanaojisimamia kama Mangula aliamini Kikwete hafai kuwa Rais kwa nini leo amtumikie kama siyo kutumika kama kondomu?
Kanga, Mangula ( kwa maelezo ya mtoa uzi) alisema Kikwete hana sifa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa uelewa wangu, jambo hili alilisema kwa siri ndani ya CCM. Sisi wengine hatukulisikia. Mpaka sasa hatujamsikia akisema Kikwete anazo sifa za kuwa Rais. Tulicho na habari nacho ni kuwa Mangula amekubali uteuzi wa Mwenyekiti wa CCM kumteua kuwa Makamu Mwenye kiti wa CCM. Kukubali uteuzi sio kukiri kuwa anazo sifa za kuwa Rais. Sidhani kama sharti la kukubali uteuzi lilikuwa aikane kauli yake ya awali ya kusema Kikwete hana sifa za kuwa Rais.
Jambo la busara la kuangalia kama tathmini ya kauli ya Mangula ni kuwa je; JK anayo maadili ya kiuongozi? Maadamu JK sasa ni Rais, licha kukataliwa na viongozi wa CCM wa wakati huo, hali halisi ikoje? Je Mangula alisema uongo au ukweli?
JK alimkataa Mangula pamoja na sekretariti yake na sasa amemrudisha kwenye uongozi wa chama tena kwenye ngazi ya juu karibu na Mwenyekiti, tafsiri yake ni nini? Kwangu mimi naona JK, LICHA KUPATA UONGOZI KWA NJIA YA MTANDAO ANAKIRI KUWA UONGOZI ULIOPITA ULIKUWA NDIYO UONGOZI BORA. Sio jambo lakumuuliza tena Mangula, ukweli unajilipiza( soma 'Tujisahihishe' Julius Kambarage Nyerere)
 
Jalem

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
217
0
Zipo hela za zamani zinaitwa Rupia, wengi huzitafuta sn japo inawezekana ni za kizushi tu, lkn zinatafutwa zinaonekana zinathamani kubwa, hapa inaonyesha kabisa, kumuacha Mangula sbb tu alisema ukweli JMK ameona kuwa jahazi linachota maji, ss ili isitokee kuzama kwa chombo baharini au kufiwa na chichiem mikononi mwake basi bora akubari yaishe mangula aendelee na falsafa zake ili chama kiendelee, hope atamsikiliza atakapo mwambia kuwa fulani anafaa na fulani hafai,
ngoja tuone, lkn tunamtaka Kagame wa TZ atakae weza wachapa viboko wazembe ktk uongozi, nakuweka maslahi ya nchi mbele.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom