Mang'azi ya yatokanayo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
145,644
2,000
Tumezoea matukio ya mwisho wa mwaka kuwa ni hekaheka za kusafiri kurudi nyumbani au kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki kwa ajili ya kuungana nao kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka
Ni kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kumekuwa pia na matukio ya kupanda kwa nauli za mikoani, foleni kwenye majiji na miji na matukio ya ajali pia...kwa ufupi ni mchanganyiko wa matukio ya furaha taharuki huzuni na kufadhaika
Mwaka huu ni tofauti kidogo
-wasafiri sio wengi hivyo nauli hazijapanda na wala hakuna hekaheka na shamrashamra za maandalizi ya sikukuu
-Foleni ni za kawaida na wageni ni wachache
Matukio ya mwaka huu yamejaa mshangao taharuki huzuni na sintofahamu kwenye mambo ya kijamii na kisiasa
-watu wamepotea
-watu wako korokoroni
-wengine inasemekana wanaminywa kimyakimya
-baadhi ya mitandao ya kijamii iko 'under fire' na hatima yake haijulikani kwa kifupi ajali za mwaka huu ni tofauti kabisa
kuna uwezekano mkubwa kuanzia mwakani JF ya sasa haitakuwa kama ilivyo kutakuwa na mabadiliko makubwa mno...na pengine yasiyovutia
Nilipoona hii picha mahali nikakumbuka mang'azi yatokanayo na hali tuliyonayo sasa
kwa utani unaweza kusema huyu ni komando kipensi lakini uhalisia ni mkubwa na tofauti kuliko maudhui ya kawaida ya picha husika
Tumetiwa nira za uoga hofu na vitisho
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
50,954
2,000
Haha kuna mdAu wiki iliyopita kakoment kwneyw thread ya kukamatwa kwa Max kuwa eti wakitaka kukamata wana JF watampata Mshana tu .
Hahaha!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom