Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,782
Ni kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kumekuwa pia na matukio ya kupanda kwa nauli za mikoani, foleni kwenye majiji na miji na matukio ya ajali pia...kwa ufupi ni mchanganyiko wa matukio ya furaha taharuki huzuni na kufadhaika
Mwaka huu ni tofauti kidogo
-wasafiri sio wengi hivyo nauli hazijapanda na wala hakuna hekaheka na shamrashamra za maandalizi ya sikukuu
-Foleni ni za kawaida na wageni ni wachache
Matukio ya mwaka huu yamejaa mshangao taharuki huzuni na sintofahamu kwenye mambo ya kijamii na kisiasa
-watu wamepotea
-watu wako korokoroni
-wengine inasemekana wanaminywa kimyakimya
-baadhi ya mitandao ya kijamii iko 'under fire' na hatima yake haijulikani kwa kifupi ajali za mwaka huu ni tofauti kabisa
kuna uwezekano mkubwa kuanzia mwakani JF ya sasa haitakuwa kama ilivyo kutakuwa na mabadiliko makubwa mno...na pengine yasiyovutia
Nilipoona hii picha mahali nikakumbuka mang'azi yatokanayo na hali tuliyonayo sasa
Tumetiwa nira za uoga hofu na vitisho