Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,108
*Maneno ya Magufuli hayatoshi: Makonda ashughulikiwe.*
*Taarifa Kwa Umma*
Maneno ya Mhe Rais, John Pombe Magufuli, aliyoyatoa jana dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kuhusiana na sakata la Makontena, yamethibitisha angalau mambo manne muhimu:
1. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, amepoteza sifa muhimu ya uongozi kwa kukwepa kodi, wakati kwa nafasi yake ya kuwa Kiongozi wa kiserikali alipaswa kuwa mstari wa mbele kulipa kodi. Rais alisema, namnukuu: *"Unaleta Makontena...unaambiwa ulipe kodi; kwanini usilipe kodi?"*
2. Mkuu wa Mkoa wa Dar ametumia madaraka yake vibaya kwa kuingiza Makontena nchini kwa maelezo kuwa ni samani za kusaidia walimu, wakati ni kwa maslahi binafsi zaidi. Rais alisema, namnukuu:
*"Shule zenyewe hata hazitajwi"* " *Walimu walikwambia wanataka makochi?* *Usiwatumie watumishi kwa maslahi yako binafsi*
3. Mkuu wa Mkoa wa Dar, amefanya udanganyifu wa makusudi (utapeli) wa kukwepa kodi na kuhujumu mapato ya serikali kwa kutaka Makontena yake yaingizwe nchini bila kulipiwa kodi yoyote huku akipuuza sheria za nchi na maadili ya uongozi na huku akijua fika kuwa samani zilizomo kwenye makontena hayo si kwaajili ya kusaidia walimu, bali ni kwa maslahi yake binafsi.
4. Hata baada ya serikali kuamua kuyapiga mnada, bado Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa dhamira ovu sana na bila kujali wajibu na maadili ya kiongozi wa serikali, aliyatumia vibaya tena madaraka yake ya Ukuu wa Mkoa kutisha wananchi wengine wasiyanunue, vinginevyo watapata laana ya kizazi kwa kizazi. Hapa pia Mkuu wa Mkoa alifanya jitihada ovu ya kuhakikisha kwa sauti ya mamlaka yake serikali ikose wanunuzi na mapato yanayolengwa kupatikana kwa kuuza makontena hayo.
Kwa mapungufu yote hayo makubwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili na misingi ya kiuongozi, nachukua fursa hii kutoa ushauri na msimamo ufuatao:
1. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kama kweli anamuheshimu Rais Magufuli na alimsikia jana wakati akieleza makosa yake makubwa ya kiuongozi na kimaadili;
Na kama kweli amekomaa kiuongozi na anataka kujirejeshea angalau heshima yake ndogo katika Taifa kutoka katika uozo wake mwingi unaofahamika nchini;
Basi mara moja achukue hatua ya kujiuzulu Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa Mhe Rais na uwajibikaji wa kiuongozi.
Vinginevyo, hatua ya Mhe Rais Magufuli kuyasema waziwazi makosa ya Makonda kama alivyoyasema jana, huku Makonda mwenyewe akiendelea kubaki madarakani bila kujali kuwa amemkosea Rais na ameikosea nchi;
Itakuwa ni sawa kabisa na Makonda kuonyesha dharau ya waziwazi kwa Mhe Rais, na itakuwa sawa na kumwambia Mhe Rais kwamba *wewe Mzee huwezi kunifanya kitu*
2. Mhe. Rais Magufuli anastahili pongezi angalau kwa kuweza kwa mara ya kwanza kuyasema hadharani makosa ya Makonda.
Hata hivyo, namuomba Mhe Rais ajue kuwa maneno yake dhidi ya Makonda hayatoshi. Taifa lilichoshwa na vitendo vingi vibaya vya Mkuu huyu wa Mkoa siku nyingi sana. Kwa hiyo, namshauri Mhe Rais kutengua mara moja uteuzi wa Makonda.
Vinginevyo, hatua ya Mhe Rais kuyasema waziwazi makosa makubwa ya Makonda huku akiendelea kumwacha madarakani, wakati wapo viongozi wengine ambao aliwaondoa madarakani huku makosa yao yakiwa hata hayajulikani; itatupa tafsiri moja mbaya sana kwamba *Mhe Rais wetu wa Nchi John Magufuli anamuogopa sana Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda*
3. Naitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi na TAKUKURU wamkamate mara moja Mkuu wa Dar, Paul Makonda, wamhoji, wafanye uchunguzi wa kina na kuhakikisha anaulfunguliwa kesi mahakamani, kwa kosa la kufanya udanganyifu wa kukwepa kulipa kodi (utapeli) kwa madai kuwa ameleta makontena yenye samani za walimu huku akijua fika ni kwa maslahi yake binafsi kama alivyosema Mhe Rais.
Vinginevyo hatua ya vyombo hivi, Jeshi la Polisi na TAKUKURU, kutochukua hatua dhidi ya Makonda inatua tafsiri kuwa ama wanamuogopa Makonda au wanathibitisha kuwa aliyoyasema Mhe Rais jana kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar ni maneno ya "uongo".
4. Kwa mara nyingine tena naitaka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma itimize wajibu wake wa kumchukulia hatua Makonda kwa makosa makubwa ya kimaadili aliyoyafanya kama ilivyofafanuliwa na Mhe. Rais.
Kinyume chake, Tume itakuwa ama imeamua kupuuza maelezo ya Rais kuhusu Makonda au itakuwa imemuogopa Makonda.
Mwisho, nasisitiza ...maneno ya Mhe Rais Magufuli hayatoshi. Makonda achukuliwe hatua.
Imetolewa Leo:
31/08/2018
Na. Henry Kilewo
Katibu wa Dar es Salaam Kuu (CHADEMA)
Sent using Jamii Forums mobile app