Maneno ya Magufuli hayatoshi, Makonda ashughulikiwe

*Maneno ya Magufuli hayatoshi: Makonda ashughulikiwe.*

*Taarifa Kwa Umma*

Maneno ya Mhe Rais, John Pombe Magufuli, aliyoyatoa jana dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kuhusiana na sakata la Makontena, yamethibitisha angalau mambo manne muhimu:

1. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, amepoteza sifa muhimu ya uongozi kwa kukwepa kodi, wakati kwa nafasi yake ya kuwa Kiongozi wa kiserikali alipaswa kuwa mstari wa mbele kulipa kodi. Rais alisema, namnukuu: *"Unaleta Makontena...unaambiwa ulipe kodi; kwanini usilipe kodi?"*

2. Mkuu wa Mkoa wa Dar ametumia madaraka yake vibaya kwa kuingiza Makontena nchini kwa maelezo kuwa ni samani za kusaidia walimu, wakati ni kwa maslahi binafsi zaidi. Rais alisema, namnukuu:
*"Shule zenyewe hata hazitajwi"* " *Walimu walikwambia wanataka makochi?* *Usiwatumie watumishi kwa maslahi yako binafsi*

3. Mkuu wa Mkoa wa Dar, amefanya udanganyifu wa makusudi (utapeli) wa kukwepa kodi na kuhujumu mapato ya serikali kwa kutaka Makontena yake yaingizwe nchini bila kulipiwa kodi yoyote huku akipuuza sheria za nchi na maadili ya uongozi na huku akijua fika kuwa samani zilizomo kwenye makontena hayo si kwaajili ya kusaidia walimu, bali ni kwa maslahi yake binafsi.

4. Hata baada ya serikali kuamua kuyapiga mnada, bado Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa dhamira ovu sana na bila kujali wajibu na maadili ya kiongozi wa serikali, aliyatumia vibaya tena madaraka yake ya Ukuu wa Mkoa kutisha wananchi wengine wasiyanunue, vinginevyo watapata laana ya kizazi kwa kizazi. Hapa pia Mkuu wa Mkoa alifanya jitihada ovu ya kuhakikisha kwa sauti ya mamlaka yake serikali ikose wanunuzi na mapato yanayolengwa kupatikana kwa kuuza makontena hayo.

Kwa mapungufu yote hayo makubwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili na misingi ya kiuongozi, nachukua fursa hii kutoa ushauri na msimamo ufuatao:

1. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kama kweli anamuheshimu Rais Magufuli na alimsikia jana wakati akieleza makosa yake makubwa ya kiuongozi na kimaadili;

Na kama kweli amekomaa kiuongozi na anataka kujirejeshea angalau heshima yake ndogo katika Taifa kutoka katika uozo wake mwingi unaofahamika nchini;

Basi mara moja achukue hatua ya kujiuzulu Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa Mhe Rais na uwajibikaji wa kiuongozi.

Vinginevyo, hatua ya Mhe Rais Magufuli kuyasema waziwazi makosa ya Makonda kama alivyoyasema jana, huku Makonda mwenyewe akiendelea kubaki madarakani bila kujali kuwa amemkosea Rais na ameikosea nchi;
Itakuwa ni sawa kabisa na Makonda kuonyesha dharau ya waziwazi kwa Mhe Rais, na itakuwa sawa na kumwambia Mhe Rais kwamba *wewe Mzee huwezi kunifanya kitu*

2. Mhe. Rais Magufuli anastahili pongezi angalau kwa kuweza kwa mara ya kwanza kuyasema hadharani makosa ya Makonda.

Hata hivyo, namuomba Mhe Rais ajue kuwa maneno yake dhidi ya Makonda hayatoshi. Taifa lilichoshwa na vitendo vingi vibaya vya Mkuu huyu wa Mkoa siku nyingi sana. Kwa hiyo, namshauri Mhe Rais kutengua mara moja uteuzi wa Makonda.

Vinginevyo, hatua ya Mhe Rais kuyasema waziwazi makosa makubwa ya Makonda huku akiendelea kumwacha madarakani, wakati wapo viongozi wengine ambao aliwaondoa madarakani huku makosa yao yakiwa hata hayajulikani; itatupa tafsiri moja mbaya sana kwamba *Mhe Rais wetu wa Nchi John Magufuli anamuogopa sana Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda*

3. Naitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi na TAKUKURU wamkamate mara moja Mkuu wa Dar, Paul Makonda, wamhoji, wafanye uchunguzi wa kina na kuhakikisha anaulfunguliwa kesi mahakamani, kwa kosa la kufanya udanganyifu wa kukwepa kulipa kodi (utapeli) kwa madai kuwa ameleta makontena yenye samani za walimu huku akijua fika ni kwa maslahi yake binafsi kama alivyosema Mhe Rais.

Vinginevyo hatua ya vyombo hivi, Jeshi la Polisi na TAKUKURU, kutochukua hatua dhidi ya Makonda inatua tafsiri kuwa ama wanamuogopa Makonda au wanathibitisha kuwa aliyoyasema Mhe Rais jana kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar ni maneno ya "uongo".

4. Kwa mara nyingine tena naitaka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma itimize wajibu wake wa kumchukulia hatua Makonda kwa makosa makubwa ya kimaadili aliyoyafanya kama ilivyofafanuliwa na Mhe. Rais.

Kinyume chake, Tume itakuwa ama imeamua kupuuza maelezo ya Rais kuhusu Makonda au itakuwa imemuogopa Makonda.

Mwisho, nasisitiza ...maneno ya Mhe Rais Magufuli hayatoshi. Makonda achukuliwe hatua.

Imetolewa Leo:
31/08/2018

Na. Henry Kilewo
Katibu wa Dar es Salaam Kuu (CHADEMA)

Sent using Jamii Forums mobile app
Huna kazi ya kufanya? Anza kushughulikia kwanza ruzuku hapo ufipa ambapo Mbowe na genge lake wanapiga ruzuku na mnaendelea kukaa kwenye kibanda cha kupanga hapo ufipa. Henry Kilewo
 
Mnahangika bure na bongo movie, mmechezewa chezo ili muone bab hana upendeleo.
 
Tujiulize ukubwa Wa makosa. RC kutangaza ripoti iliyo mezani kwake kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa anakuwa DISMISSED bila kupepesa macho. Kwamba hilo ni kosa baya sana.
Lakini RC kudanganya kwa nia ya kukwepa kodi na inapogundulika na serikali kutangaza kupiga mnada anamtukana waziri wa serikali yake na kuwaombea laana wanunuzi tena akiwa kanisani!
Hapo ndio unapokuja umuhimu Wa kupeleleza ile taasisi ya juu kabisa tuilaumu kama taasisi au MTU binafsi mmoja?
Maana kama taasisi ndio yaweza kuamua hivyo basi hiyo ni taasisi mbovu kuliko zote duniani, lakini kama in MTU mmoja binafsi basi hastahili kuendelea kutoa maamuzi. ATOKE au ATOLEWE hiyo ni nafasi ya umma sio binafsi, aliomba kwa unyenyekevu asitake kumtoa kwa njia zisizo busara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa kubwa kwa mtumishi wa umma ni kujaribu kwa namna yoyote kukwepa kulipa kodi. Ukibainika huruhusiwi hata kugombea uongozi wowote Tanzania. Kwa jambo hili. Bashite kapoteza sifa ya kugombea ubunge kwenye moja ya majimbo ya Dar es Salaam. Maana mazingaombwe yote haya ni kusafisa njia ya kugombea ubunge Dar mwaka 2020.
 
"Mimi sishauriki. Ukijaribu kunishauri ndio umeharibu kabisaaaaaaaa......"
 
Wanajifanya kuonea watu wengine kwa kuwatumbua,wakati vinara wa muhujumu uchumi ni wao
 
Kwa maandiko kama haya, Bashite atazidi kudunda tu. Jiwe hapendi kuonekana ameact kwa kulazimishwa
 
Huna kazi ya kufanya? Anza kushughulikia kwanza ruzuku hapo ufipa ambapo Mbowe na genge lake wanapiga ruzuku na mnaendelea kukaa kwenye kibanda cha kupanga hapo ufipa. Henry Kilewo
Tumegundua kuwa majambazi wanaongoza ofisi za umma
 
Yule mama alimwambia "huwezi nijibu hivi mimi" kilichofuata akamtumbua kwa kutokujua na kuwa na takwimu sahihi kwa muda ule; huyu ni mkwepa kodi ni zaidi ya jangili anabembelezwa alipe richa ya kuongopa kote huko
 
Nani alikwambia Makonda atatenguliwa uRC?
Kapewa FRIENDLY WARNING yaani nusu yellow card,bado nusu nyingine ya yellow card kabla ya red card!
Ushaambiwa na mkuu wa kaya kuwa hapangiwi japo anaweza kushauriwa.Mwenye kuteua na kutenguwa ni mwenyewe.
Bado Makonda ni tanzanite kwa siasa za Tanzania.
Alikuwa kwa Six,akapenyeza kwa Kikwete,akachomoa kwa Membe ili kumuunga mkono Magu.
Hapana chezea Makonda,ndio kwanza mpira unaanza.
Ila Dogo Paul mimi namsifu pamoja na madhaifu yake ni kijana ambaye amepambana sana kavuka milima na mabonde mpaka hapo alipo
 
NAWASHANGA NYIE JIJI, MKURUGENZI PAMOJA NA WAZIRI WENU.....................MTOTO KWA BABA AISEE.
 
*Maneno ya Magufuli hayatoshi: Makonda ashughulikiwe.*

*Taarifa Kwa Umma*

Maneno ya Mhe Rais, John Pombe Magufuli, aliyoyatoa jana dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kuhusiana na sakata la Makontena, yamethibitisha angalau mambo manne muhimu:

1. Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, amepoteza sifa muhimu ya uongozi kwa kukwepa kodi, wakati kwa nafasi yake ya kuwa Kiongozi wa kiserikali alipaswa kuwa mstari wa mbele kulipa kodi. Rais alisema, namnukuu: *"Unaleta Makontena...unaambiwa ulipe kodi; kwanini usilipe kodi?"*

2. Mkuu wa Mkoa wa Dar ametumia madaraka yake vibaya kwa kuingiza Makontena nchini kwa maelezo kuwa ni samani za kusaidia walimu, wakati ni kwa maslahi binafsi zaidi. Rais alisema, namnukuu:
*"Shule zenyewe hata hazitajwi"* " *Walimu walikwambia wanataka makochi?* *Usiwatumie watumishi kwa maslahi yako binafsi*

3. Mkuu wa Mkoa wa Dar, amefanya udanganyifu wa makusudi (utapeli) wa kukwepa kodi na kuhujumu mapato ya serikali kwa kutaka Makontena yake yaingizwe nchini bila kulipiwa kodi yoyote huku akipuuza sheria za nchi na maadili ya uongozi na huku akijua fika kuwa samani zilizomo kwenye makontena hayo si kwaajili ya kusaidia walimu, bali ni kwa maslahi yake binafsi.

4. Hata baada ya serikali kuamua kuyapiga mnada, bado Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa dhamira ovu sana na bila kujali wajibu na maadili ya kiongozi wa serikali, aliyatumia vibaya tena madaraka yake ya Ukuu wa Mkoa kutisha wananchi wengine wasiyanunue, vinginevyo watapata laana ya kizazi kwa kizazi. Hapa pia Mkuu wa Mkoa alifanya jitihada ovu ya kuhakikisha kwa sauti ya mamlaka yake serikali ikose wanunuzi na mapato yanayolengwa kupatikana kwa kuuza makontena hayo.

Kwa mapungufu yote hayo makubwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili na misingi ya kiuongozi, nachukua fursa hii kutoa ushauri na msimamo ufuatao:

1. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kama kweli anamuheshimu Rais Magufuli na alimsikia jana wakati akieleza makosa yake makubwa ya kiuongozi na kimaadili;

Na kama kweli amekomaa kiuongozi na anataka kujirejeshea angalau heshima yake ndogo katika Taifa kutoka katika uozo wake mwingi unaofahamika nchini;

Basi mara moja achukue hatua ya kujiuzulu Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ili kuonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa Mhe Rais na uwajibikaji wa kiuongozi.

Vinginevyo, hatua ya Mhe Rais Magufuli kuyasema waziwazi makosa ya Makonda kama alivyoyasema jana, huku Makonda mwenyewe akiendelea kubaki madarakani bila kujali kuwa amemkosea Rais na ameikosea nchi;
Itakuwa ni sawa kabisa na Makonda kuonyesha dharau ya waziwazi kwa Mhe Rais, na itakuwa sawa na kumwambia Mhe Rais kwamba *wewe Mzee huwezi kunifanya kitu*

2. Mhe. Rais Magufuli anastahili pongezi angalau kwa kuweza kwa mara ya kwanza kuyasema hadharani makosa ya Makonda.

Hata hivyo, namuomba Mhe Rais ajue kuwa maneno yake dhidi ya Makonda hayatoshi. Taifa lilichoshwa na vitendo vingi vibaya vya Mkuu huyu wa Mkoa siku nyingi sana. Kwa hiyo, namshauri Mhe Rais kutengua mara moja uteuzi wa Makonda.

Vinginevyo, hatua ya Mhe Rais kuyasema waziwazi makosa makubwa ya Makonda huku akiendelea kumwacha madarakani, wakati wapo viongozi wengine ambao aliwaondoa madarakani huku makosa yao yakiwa hata hayajulikani; itatupa tafsiri moja mbaya sana kwamba *Mhe Rais wetu wa Nchi John Magufuli anamuogopa sana Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda*

3. Naitaka Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi na TAKUKURU wamkamate mara moja Mkuu wa Dar, Paul Makonda, wamhoji, wafanye uchunguzi wa kina na kuhakikisha anaulfunguliwa kesi mahakamani, kwa kosa la kufanya udanganyifu wa kukwepa kulipa kodi (utapeli) kwa madai kuwa ameleta makontena yenye samani za walimu huku akijua fika ni kwa maslahi yake binafsi kama alivyosema Mhe Rais.

Vinginevyo hatua ya vyombo hivi, Jeshi la Polisi na TAKUKURU, kutochukua hatua dhidi ya Makonda inatua tafsiri kuwa ama wanamuogopa Makonda au wanathibitisha kuwa aliyoyasema Mhe Rais jana kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar ni maneno ya "uongo".

4. Kwa mara nyingine tena naitaka Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma itimize wajibu wake wa kumchukulia hatua Makonda kwa makosa makubwa ya kimaadili aliyoyafanya kama ilivyofafanuliwa na Mhe. Rais.

Kinyume chake, Tume itakuwa ama imeamua kupuuza maelezo ya Rais kuhusu Makonda au itakuwa imemuogopa Makonda.

Mwisho, nasisitiza ...maneno ya Mhe Rais Magufuli hayatoshi. Makonda achukuliwe hatua.

Imetolewa Leo:
31/08/2018

Na. Henry Kilewo
Katibu wa Dar es Salaam Kuu (CHADEMA)

Sent using Jamii Forums mobile app
"John Mccain detested the abuse of power"
George Bush today at John McCain memorial service
 
Back
Top Bottom