Maneno ya kuambiwa

Maneno ya kuambiwa

mumewanguu

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2018
Posts
261
Reaction score
259
Busara katika maisha huhitajika vinginevyo waeza fanya maamuzi magumu kwa kusikiliza maneno ya kuambiwa kumbe hayana ukweli wowote.

Jamaa kampiga risasi shemeji yake akijua anampiga hawara wa mkewe ,hii ni kwa sababu mfanya kazi wa ndani alimwambia kuwa kila ukitoka mkeo anaingiza mume ndani, jamaa akamwambia basi kesho akija tu nipigie nije nifumanie, kesho yake kama kawaida kaka wa mkewe alikuja asubuhi kwa dada yake kula jamaa akapigiwa kuja akafungua mlango na kurusha risasi akijua anamlenga mgoni wake kumbe shemeji yake,hii ni kwa sababu yule mfanyakazi alikuwa hamjui huyu shemeji yake na boss wake akadhan ni hawara wa mke wa boss hivo akasambaza maneno kuwa mke wa boss anamsaliti mumewe akitoka naye anaingiza mchepuko

Je, Ni Jambo gani ushawahi kufanya kwa kufuata maneno ya kuambiwa kumbe hamna ukweli wowote
 
Aisee hasira hasara...tujifunze kufuatilia kitu kabla ya kufanya maamuzi

Nashukuru Mungu sijawahi kurupuka..hata nikisikia neno hadi nilishuhudie mwenyewe ndio hufanya maamuzi
 
Hyo jamaa kichwa kibovu sana..yan mtu ujamuona kwa macho unampigaje risasi?

Hii stor sio yakuamini pia!
 
Back
Top Bottom