Maneno ya Karume kwa Wazanzibar wote

Maneno ya Karume kwa Wazanzibar wote

swagazetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
4,253
Reaction score
1,475
Ndugu wanajamvi napenda tutoe maoni juu ya maneno haya yaliyosemwa na karume akiwafariji wazanzibari walioonekana kupoteza imani juu ya muungano,tafakari maneno yake haya:
"...Ndugu wazanzibari wenzangu msisononeke wala kufadhaishwa na muungano huu kwa sababu Muungano ni kama koti unalivaa likikubana Unalivua..."

je karume alikuwa na dalili za kukata tamaa na muungano?
 
...Ndugu wazanzibari wenzangu msisononeke wala kufadhaishwa na muungano huu kwa sababu Muungano ni kama koti unalivaa likikubana Unalivua..."
Sasa hivi naona kama Koti Limebana - Elekeza macho yako kwenye TV uwaone wanavyopeana vijembe....
 
Koti limebana, lakini linalazimishwa na watanganyika kwa namna yoyote! Watanganyika wanawatisha na kuwahonga wazanzibar ili waisaliti nchi yao!
 
Sasa hivi naona kama Koti Limebana - Elekeza macho yako kwenye TV uwaone wanavyopeana vijembe....

Naona CCM wanachukua vipimo kwa kamba badala ya futi sijui likishonwa litawatosha?...kazi kweli kweli...
 
Kinachonishangaza matusi na vijembe vilivyokuwa vikitolewa kwenye mitandao ya kijamii dhidi wa Wadanganyika vilikuwa vinatutisha tu?Kwa nini leo wameanza kulumbana wenyewe kwa wenyewe?Imeshangaza wanatoleana kashfa,matusi na vijembe visivyo na hadhi ya kutolewa bungeni.

Kuaibishana ndiko kumekuwa ajenda na hoja kuu,na Katiba imeachwa,sasa sielewi yupi anasema ukweli na yupi anatafuta TONGE.Hebu tuelezeni Wazanzibar nini mnataka?
 
Nilikua sijui nini maana ya neno FYATA! Lakini kwakukaa kwangu na kupoteza muda wangu kwa kuangalia Bunge la Ze Comedy nimetoka na neno FYATA maana yake Ni Busha!

Bado naangalia TV
!
 
Nimemnukuu jamaa mmoja leo Bungeni anamjibu Mpemba mwenzake na kumwambia USITUCHANGANYE KAMA MBOGA YA VIAZI!

Nina hamu sana ya kufika ZANZIBAR NIKALE UROJO
!
 
Kama kuna mwana jamvi toka zenji tupatie hali halisi ya huko znz kufuatia mjadala wa katiba bungeni
 
KOTI kwa hivi sasa siyo limebana tu, bali limechakaa na kuchanikachanika sana.
 
Abedi Amani Karume angekuwa hai muungano ulitakiwe ufe kabla ya CCM kuzaliwa. Na leo tusingekuwa na ccm labda TANU ingekuwa na akili zaidi.
 
Abedi Amani Karume angekuwa hai muungano ulitakiwe ufe kabla ya CCM kuzaliwa. Na leo tusingekuwa na ccm labda TANU ingekuwa na akili zaidi.
 
Kinachonishangaza matusi na vijembe vilivyokuwa vikitolewa kwenye mitandao ya kijamii dhidi wa Wadanganyika vilikuwa vinatutisha tu?Kwa nini leo wameanza kulumbana wenyewe kwa wenyewe?Imeshangaza wanatoleana kashfa,matusi na vijembe visivyo na hadhi ya kutolewa bungeni.

Kuaibishana ndiko kumekuwa ajenda na hoja kuu,na Katiba imeachwa,sasa sielewi yupi anasema ukweli na yupi anatafuta TONGE.Hebu tuelezeni Wazanzibar nini mnataka?

Wakirudi kwao ndio wanahamasisha Watanganyika wachomewe biashara zao. Dodoma wanajidai wanaupenda sana muungano. WanaCCM Zanzibar ni wanafiki wakubwa kupata kuona hapa Tanzania?
 
CCM bila Muungano wa mbili haipo , kwani mbili ni TANU NA ASP sasa kama hakuna mbili maana yake ni TANU KWA TANGANYIKA naASP KWA ZANZIBAR ....HAWA NI WASAKA TONGE TU....
 
Wakirudi kwao ndio wanahamasisha Watanganyika wachomewe biashara zao. Dodoma wanajidai wanaupenda sana muungano. WanaCCM Zanzibar ni wanafiki wakubwa kupata kuona hapa Tanzania?

Ndiyo kinachoumiza ndugu yangu.Hawasemi ukweli.Ni bora wangeamua kuondoa kwa dhati kero za pande zote mbili.Kwa kweli ni bora tukarudi kwenye Katiba ya zamani,hii tumeshindwa kuijadili na kuitunga.
 
Abeid Amani Karume Sr.

Hatuna Karume mwenye jina lenye Sr. labda kama hujui matumizi yake! Maana Karume Mzee alikuwa anaitwa Abeid Aman Karume; mtoto yeye anaitwa Aman Abeid Aman Karume. Sasa Sr inatoka wapi hapo?
 
Wakirudi kwao ndio wanahamasisha Watanganyika wachomewe biashara zao. Dodoma wanajidai wanaupenda sana muungano. WanaCCM Zanzibar ni wanafiki wakubwa kupata kuona hapa Tanzania?

Hio ndio hali!Lakini kwa nini Watanganyika hamdai nchi yenu au atleast baadhi ya haki munazoona munanyimwa katika Muungano huu.Badala yake ni kulalamikia yale wanayoyapata Wazanzibari au ndio munataka Muungano wa Serikali moja? Wazanzibari hilo hawalikubali, Kama hamkudai munachotaka mutashtukia Katiba imepitishwa na Wazanzibari wamepata kila wanalolitaka kama maliasili kuwa si ya Muungano,kujiunga na mashirika ya Kimataifa nk mbali ya waliyonayo sasa hivi kama Katiba yao,Rais wao nk.Watanganyika daini haki yenu badala ya kulalamika kuwa Zanzibar inapata hichi na hichi katika Muungano.
 
Hatuna Karume mwenye jina lenye Sr. labda kama hujui matumizi yake! Maana Karume Mzee alikuwa anaitwa Abeid Aman Karume; mtoto yeye anaitwa Aman Abeid Aman Karume. Sasa Sr inatoka wapi hapo?

Asante mkuu kwa kunisahihisha hapo. Niliongeza mbwembwe ambayo inapotosha ukweli. Kumradhi kwa wote mliokwazika!
 
Back
Top Bottom